ONGEZA NA HIII................
UMEOA MWANAMKE SI MBUZI: Utamsikia mwanaume anajisifia kabisa “Mke wangu yeye hapendi hayo mambo, muelewa sana yule mwanamke, hivyo vitu anajinunulia mwenyewe, yeye alimradi chakula kiwepo mezani na watoto waende shule basi!” Ndugu yangu labda kama umeoa Mbuzi na si hawa wanawake ninaowajua mimi. Hakuna mwanamke ambaye hapendi kudekezwa, hapendi umnunulie vizawadi, hapendi umtoe out siku moja moja, hapendi umsifie na kumsuprise kimapenzi mapenzi. Wewe kuleta ugali mezani ni majukumu yako kama mwanaume, lakini kumtoa hata kula chips mtaani ni mapenzi, kumpelekea maua ni mapenzi. Kumpa hela ya kununua nguo ni majukumu, lakini kumnunulia nguo, ukamuambia ajaribishe, ukamsifia alivyopendeza ni ni mapenzi. Utasikia mwanaume anasema “Mimi siwezi kuchagua nampa pesa achague mwenyewe..” Ndugu yangu raha ya zawadi ni kununuliwa na si kujinunulia. Ukimpa pesa akanunue maua yanakua maua ya mezani ila ukimnunulia wewe na kumpa yanageuka kuwa zawadi ya maua hata kama hayana harufu utaona an...