ONGEZA NA HIII................
UMEOA MWANAMKE SI MBUZI: Utamsikia mwanaume anajisifia kabisa “Mke wangu yeye hapendi hayo mambo, muelewa sana yule mwanamke, hivyo vitu anajinunulia mwenyewe, yeye alimradi chakula kiwepo mezani na watoto waende shule basi!”
Ndugu yangu labda kama umeoa Mbuzi na si hawa wanawake ninaowajua mimi. Hakuna mwanamke ambaye hapendi kudekezwa, hapendi umnunulie vizawadi, hapendi umtoe out siku moja moja, hapendi umsifie na kumsuprise kimapenzi mapenzi.
Wewe kuleta ugali mezani ni majukumu yako kama mwanaume, lakini kumtoa hata kula chips mtaani ni mapenzi, kumpelekea maua ni mapenzi. Kumpa hela ya kununua nguo ni majukumu, lakini kumnunulia nguo, ukamuambia ajaribishe, ukamsifia alivyopendeza ni ni mapenzi.
Utasikia mwanaume anasema “Mimi siwezi kuchagua nampa pesa achague mwenyewe..” Ndugu yangu raha ya zawadi ni kununuliwa na si kujinunulia. Ukimpa pesa akanunue maua yanakua maua ya mezani ila ukimnunulia wewe na kumpa yanageuka kuwa zawadi ya maua hata kama hayana harufu utaona anachekacheka na kuyanusa nusa…!
Ukimpa pesa akanunue chips mtaani inakuwa ni chakula ila ukimtoa sehemu mkaenda kukaa na akaagiza chips inakuwa ni mtoko ‘outing’ na atawasimulia na marafiki zake wote kuwa umlimtoa. “Au ulifikiri mkitoka out ndiyi anaenda kuagiza kuku wa mbinguni?”
Unajifanya hujui kuchagua, yaani hata kwenda dukani kununua dazeni za underwear na kumpelekea huwezi au hujui hata saizi ya kiuno chake! Ukimpa hela ya kununulia nguo anaweza akanunua hata kumi na zinakua nguo tu, lakini ukamletea nguo moja inageuka na kuwa zawadi na atawasimulia rafiki zake wote.
Badilika ndugu yangu, vitu vidogo vidogo ambavyo havigharimu chochote kwa mwanamke ndiyo mapenzi lakini vile vikubwa vinaitwa majukumu. Mkeo hata anajifanya hapendi kwakuwa ashakusoma anaona humjali hivyo ili tu kulinda ndoa na asiumie hujifanya kutokupenda.
Lakini hata kama angekuwa Raisi bado angetamani umuite Baby, umsuprise na maua ya elfu mbili na hata kacheni kampoja kakuoshea. Narudia labda kama umeoa Mbuzi si wanawake hawa ambao ninawafahamu!
Comments
Post a Comment