Maajabu ya Wanawake Yaliyowashinda Hata Wana Falsafa Kuelewa
*Naomba msipanick walimu,🙌🏼* *Ukinipinga pinga kwa hoja.* Wanawake ni binadamu wa ajabu sana katika uso huu wa Dunia yaani hawa watu ni next level, kuwaelewa ni ishu iliyowashinda hata wana falsafa, Newton na uwezo wake wote linapokuja suala la wanawake lazima atoke kapa na (ndio maana haieleweki hata kama akioa). Manabii na busara zao zote walishindwa kuwaelewa wakaishia kushauri ya kwamba tuishi nao kwa akili. Sasa najiuliza ni jambo gani unaweza fanya bila kutumia akili?, hapa ndipo napata ushahidi kwamba kumbe wanawake walishindikana tangu zama za mwanzo kabisa!. Wanasaikolojia wanasema kuwa kama utamuoa/kuishi na mwanamke mwenye miaka 25 basi itakuchukua miaka 25 mingine kumuelewa huyo mwanamke angaalau kwa 90% maana hawa kila siku hubadilika na kuwa wapya kimatendo na kifikra. Mwanamke unaweza mnunulia BMW X6 akatoka nayo kwenda kutembea, akiwa njiani akaombwa lift na kijana akampa akipitia sheli hela ya mafuta ikawa haitoshi, yule kijana akaamua kumuongeza ata elfu 20 b...