Posts

Showing posts from June, 2020

Breaking News! TAARIFA MUHIMU KWA WASOMAJI WETU NA WATUMIAJI WA APP YETU YA UTAMU KITANDANI

Image
TUNAPENDA KUWATAARIFU WASOMAJI WETU KWAMBA TUMEPATA HITILAFU KWENYE APP ZETU ZILIZOPO GOOGLE PLAYSTORE HIVYO KUSABABISHA APP ZOTE KUONDOLEWA KABISA KWENYE MFUMO WA GOOGLE PLAYSTORE  HIVYO TUNAPENDA KUWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAO JITOKEZA, KWA SASA TUNAJITAHIDI  KUFANAY MAREKEBISHO NA TUNAWAAHIDI  KWAMBA MUDA SI MREFU APP YAKO PENDWA YA  ' UTAMU KITANDANI' ITARUDI TENA HEWANI NA UTAENDELEA KUFURAHIA KAMA ILIVYOKUWA ZAMANI KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NASI KWA 0755542721 email ya  kingazimediatz@gmail.com Sms Tamu za kumtumia Mpenzi wako, ili kumuonesha kwamba unampenda.

ACHA KUWA KIAZI, MKISHAACHANA MMEACHANA HAKUNA KUACHANA VIZURI!

Image
Dada zangu hembu jitambueni hata kidogo hivi mwanaume ulikua naye kwenye mahusiano, kakutumia wee kakuchakaza, mwisho kakuacha kaenda kuoa mwanamke mwingine. Baada ya muda anakuja kwako na kukuambia kakukumbuka, unakubali unamrudia, kila siku unagombana na mke wake bila aibu unamuambia “Wewe umeolewa lakini mimi ndiyo napendwa!” Dada, kwa taarifa yako hata magunia ya deki yanapendwa ila yanaishia kufutiwa miguu t u! Kama alikuacha kipindi hana mke sasa hivi anarudi kwako kufanya nini? Ukiona mwanaume kakuacha, kaenda kuolewa na karudi kwako basi jua kuwa anakudharau! Anaona kabisa kuwa wewe huna maisha bila yeye. Lakini wakati mwingine hata hamkuachana kwa kuchokana, hapana, mwanaume mlikua mnapenda, labda mkaachana kwasababu ya Dini au Kabila, wazazi hawataki, lakini nyie bado mnapendana. Ameenda kaoa anarudi mnaendelea naye, aisee hakuna kitu kinapoteza muda kwa mwanamke kama kuendelea kufanya mapenzi na X wako ambaye mlikua mnapendana. Dada zangu, mwanaume mkiachana...

USIUDANGANYE MOYO WAKO KWAMBA ULIYE NAE MNAENDANA KISA ULIPENDA UWE NA MWENZA ALIYE SMART KESHO NI FUMBO 🤔

Image
Muonekano unaweza kupotea kwa hali ya maisha kubadilika ama ugonjwa na wakati mwingine umri nao ni sehemu ya badiliko la MUONEKANO. Unaweza kuamini kwa macho lakini ikawa sio vile NAFSI YAKO INAHITAJI na tatizo limewapata wengi, Unamtazama Mtu na kuamini kuwa ni yeye pengine ni kwa sababu tu ana sifa mbili kati ya zile ulipenda awe nazo MWENZA WA MAISHA YAKO 💑 Haja ya na fsi haitafutwi kwa majaribio, lakini pia kumbuka wazi ULIVYO LEO UNAWEZA KUWA BORA ZAIDI BAADAYE ukajikuta unamuona mwenza wako haendani nawe tena na hapo utanielewa nikisema MUONEKANO WA MTU SIO HITAJI LA NAFSI ila ni ukosefu wa utulivu wa HISIA ZAKO. Mchukuwe Mtu aliye chaguliwa na NAFSI YAKO halafu mjazie mapungufu yake, Mfanye awe kamili kama ulivyohitaji Mwenza wako awe, Ndo maana ni rahisi kwa Mwanaume kuwa na MWANAMKE WA NAFSI YAKE kuliko Mwanamke kuwa na Mwanaume wa NAFSI YAKE sababu ni ndogo sana:- ▪  Mwanaume kumuoa Mwanamke na kwenda kumtengeneza ni rahisi, kuliko Mwanamke kuchukuwa Mwanaume wa H...

Ijue tofauti kati ya UPENDO WA MWANAUME NA MWANAMKE;

Image
▪  Mwanaume akimpenda Mwanamke anamuweka akilini, yaani kama kuna VIONJO VIPO KI PEKEE atadumu nawe akilini mwake 😂  na wenye BAHATI wao mpaka moyoni huzama hao ndo humfanya Mwanaume hata KUJIUA kulikosa penzi la Mwanamke aliyempenda. ▪  Mwanamke akimpenda Mwanaume ANAMUWEKA MOYONI wala hapatakuwepo na Mwanaume mwingine ataweza kukuondoa hata awe na NGUVU GANI kwa hakika hataweza kumuingiza MOYONI ila ataweza kumuingiza akilin i kwa SABABU ZA KI MAISHA. Mpaka hapo ushajua kwanini MAPENZI YANA RUN DUNIA 🌎 Kila MBABE NA MBABE WAKE  😂  ila ukiona wewe unaonewa na Mtu umpendaye ujue kuna mahala nae ni FALA TU  🤣 🤣  anapelekeshwa mpaka mwishooo, Ndo maana halisi ya UPENDO  💞  UPOFU 🤔 Mheshimu akupaye AMANI YA MOYO  💖  vinginevyo utajitafutia MARADHI BURE  🤦‍♂️ Maana UTULIVU WA NAFSI UNATOKANA NA HITAJI LAKE kinyume chake utalazimisha kusahau kisichosahaulika mwisho kabisa UFE UNAJIONA  😭 😭 Sms Tamu ...

MWANAUME ANGEMPENDA MWANAMKE KWA MOYO 💖 WAKE WALA ASINGEACHA KURIDHIKA NA MWANAMKE MMOJA ⛔

Image
Mwanaume ni sawa na mgonjwa wa kisukari  😂 😂 😂 Yaani ni kweli AMEOA 👩‍❤️‍👨  ila kuacha kupata hamu kwa Mwanamke mzuri zaidi ya mkewe ni kama DHAMBI 🤦‍♂️ Ndo maana nikamlinganisha Mwanaume na mgonjwa wa kisukari, ni kweli ametakiwa kuacha vitu vitamu ila akiona FANTA anameza mate  😋 Tatizo sio UZURI WA MWANAMKE  ⛔  tatizo kubwa linawapata wanaume ni KUTOMKUBARI MWANAMKE ALIYE NAYE na kuamini katika FARASI 🦄  UKIMPANDA HAKUTISHI MIONDOKO wakati huo huo MWANAMKE aliyemfanya amdharau aliye nae kuna Mwanaume kamkinai hapo ndipo utanielewa TATIZO LA WANAUME SIO UZURI WA MWANAMKE  ⛔  tatizo lao kuu KIU 😂 😂 Muda wote wanatamani kuonja kila KISIMA bila hata kujua wataleta MADHARA gani kwa aliyepo 🤔 Visima vingine ukionja maji yake utahamia na hapo ndipo utanielewa kwamba KULIKO KUONJA ONJA CHIMBA KISIMA CHAKO MWENYEWE 🤝 Sms Tamu za kumtumia Mpenzi wako, ili kumuonesha kwamba unampenda.

USICHELEWE KUMUONYESHA UPENDO WAKO WA DHATI 💕 YULE ALIYEANDIKWA NAFSINI MWAKO⛔

Image
Kuna wakati upendo huo utakuwa hauna maana tena baada ya MAUMIVU MAKALI ULIMPITISHA NAYO akiamini huna UPENDO WA DHATI  💕  KWAKE. Na ndipo utajua ni kiasi gani inauma ikiwa UNAMPENDA MTU LAKINI HAJUI 😭 Maumivu yale aliumia MHITAJI hugeuka kuwa MAUMIVU YAKO na hapo ndipo utanielewa kwamba kuliko KUUFICHA UPENDO kwa kuogopa akijua UNAMPENDA atakuona wewe ni DHAIFU na huo ndo ujinga kweli kweli maana UDH AIFU NDIYO HUONYESHA UPENDO WAKO KWA MTU kwa kuuficha UDHAIFU wako tarajia kuonekana huna UPENDO WA DHATI  💕  na mwisho kabisa ni wewe kubakia MPWEKE kwa uzembe wako 😭 Onyesha UPENDO WAKO WOTE KWA YULE ULIYEMPENDA ili upokee AMANI moyoni mwako, Kumkosa uliyempenda ni HATARI sana lakini pia ni rahisi kukosa wa kumpenda duniani Kwani UPENDO WA KWELI NI KWA MMOJA  ❤️ Usijidanganye kuna mwingine ataleta MAPINDUZI NAFSINI MWAKO baada ya yule uliyempenda kuondoka maisha mwako, zaidi utaishi kwa Mahangaiko ya NAFSI kwa Kumkosa ULIYEMPENDA huku ukileta mateso ya...

MWANAMKE ANAPOUMIA HAIMFANYI ASIPENDE TENA KWA SABABU KWAKE KUPENDA NI WITO JAPO TATIZO NI NAMNA GANI ATAAMINI BAADA YA KUUMIZWA🤷‍♂️

Image
Maisha ya Mwanamke huchanua tangu angali msichana, namna nzuri ya kuamini juu ya UKOMBOZI WA MWANAMKE NI BAADA YA KUJENGWA KATIKA MSINGI WA KUJITEGEMEA MWENYEWE. Familia zilizo nyingi zinamjenga BINTI katika kuiheshimu NDOA hata kama itakuwa haileti UKOMBOZI MAISHANI MWAKE na hilo ndilo anguko kubwa la maisha ya Mwanamke  😭 😭 Mwanamke akiishi kwen ye mafunzo ya kuiabudu NDOA basi hata awe mwenye ELIMU kubwa kiasi ATAISHI KAMA MTUMWA. Mwanamke akijikomboa ki fikra kamwe hataishi kwa kuogopa:- ▪  JAMII. ▪  MUME. ▪  DINI. ▪  MWANAMKE MWENZIE. Mwanamke aliyejikomboa kamwe hataangalia DUNIA ITASEMA NINI bali atakuwa YEYE na wala hataruhusu KITU AMA MTU aingilie UHURU WA NAFSI YAKE  ⛔ Wanawake wengi wameangamia kwa kuangalia DUNIA ITASEMAJE na kujikuta wameangukia kwenye NDOA zilizojeruhi maisha yao yote, Kila kukicha anashukuru MUNGU na kujisemea siku moja MUNGU ATALETA MUUJIZA KWAKE huku akisahau anguko lake lilijengwa na MALEZI YAKE 😭 😭 Elimu ...

Mwanaume na Mwanamke usikose URAFIKI WA MAPENZI

Image
Mwanaume na Mwanamke usikose URAFIKI WA MAPENZI:- "boyfriend and girlfriend" kabla ya NDOA yako. Urafiki kabla ya ndoa huo ndiyo huibua TABIA HALISI YA MTU kwa vyovyote vile hupashwi kuingia kwenye ndoa kama hujawa na utambuzi wa tabia ya mwenza wako, Watu wengi wamejikuta wanaugulia MIOYO YAO baada ya wenza wao kutokuwa kama walivyo watarajia, Unajua kuna mambo mawili tofauti ila wengi hawajui kutofautisha ni kati ya; ▪  MAKOSA. ▪  UDHAIFU. Makosa yana eneo lake ambalo ni baada ya Mtu kujikuta kakosea iwe kwa kujua ama makusudi lakini akajua kwamba hakupashwa kufanya hivyo, Udhaifu ni ama uhalisia wa Mtu au ni kutokana na kushindwa kuhimili changamoto. Imagine unaingia kwenye ndoa na Mtu ambaye hujui madhaifu yake unajua unaweza kujua ni MAKOSA wakati ndo udhaifu wake, MFANO; Humjui mtu, Mmekutana ukitokea kwenye Mahusiano aliyoyapenda ila yakamuumiza, na wewe umeachwa ama kumuacha uliyempenda na nyote kila mmoja akitafuta FARAJA unafikiri atakuacha uende zako wakati...

WANAWAKE WENGI WAKISHAOLEWA HUDHANI MAISHA YAMEISHA, WANAJISAHAU.

Image
Wanawake wengi wakishaolewa hudhani kuwa maisha yameisha, wanajisahau kwa namna flani, ile dhana kuwa mwanaume yupo basi inawachanganya sana, inawaondolea ule mzuka wa kutafuta, ile hamu ya mafanikio, hasa wale wanawake ambao waume zao wanajali, wanahudumia kila kitu. Wanawake kama hawa wanajisahau sana katika suala la kutafuta, hawa ndiyo utasikia; (1) Nasubiri kwanza nimalize kuzaa ndiyo nitafute kazi au nifanye Biashara; Ukweli ni kuwa mume anahudumia sina haja ya kubeba m imba huku nikifanya kazi! (2) Mimba yangu inanisumbua siwezi kufanya chochote; Nikweli wakati mwingine mimba sinasumbua, lakini wanaacha kazi kwakua kuna anayehudumia, single mother angekomaa na bosi na maruhusa, angehangaika na mabarua mpaka basi, single mother asingefunga Biashara, angeajiri mtu lakini kila siku angefuatilia, simu zingepigwa mpaka basi. (3) Nasubiri mpaka mtoto akue, wanangu hawawezi kulelewa na Dada wa kazi! Wadada wa kazi siku hizi kupata shida; Hapo unakuta mtoto ana mwak...

USHAWAHI KUKUTANA NA WALE WADADA WANAOUZA BIRIANI PEPONI?

Image
Hakuna wanawake ambao wanajisikia raha kama wale wanawake ambao anatembea na mume wa mtu, halafu mwanaume anamshirikisha kila kitu. Mwanaume hawezi kufanya kitu cha maendeleo, iwe ni Biashara au kujenga bila kumuambia na kutaka maoni yake. Wanajiona sana aisee, yaani ukiwasikia wanavyojisifia kuwa, ananipenda kuliko mke wake, mke wake hana akili,a lifunguliwa duka akalila lote. Basi unaweza udhani ni wale wadada wa pep oni amabo wanapika Biriani kila Jumanna (Biriani la kule ni Jumanne). Hasa ukute mke wa jamaa ni Mama wa nyumbani aisee watasumbua mpaka basi. Lakini ukweli nikuwa hakuna wanawake VIAZI kama hawa. Yaani tena ni vile viazi ambavyo unakuta vimetobolewa, ukikipika unakuta ni kichungu. Wako vizuri na wana akili ya kutafuta, wana mawazo mazuri lakini ni viazi kwenye mapenzi. Najua washaanza kutoa povu kuwa Kaka iddi anatukana hivyo ngoja niwakumbushe tu kidogo. (1) Anakuambia anakupenda na una akili kuliko mke wake. Mawazo yote ya baishara unatoa wewe, lakini biash...

UNAUSHUHULIKIAJE MOYO ULIOUMIZWA??

Image
Tunaumizwa ktk mazingira tofauti sana Tunaofautiana namna ya kuumia na hali ya kukabiliana na maumivu Inauma zaidi ikiwa aliyekuumiza ni mtu wa karibu na wewe Unafanyaje??? 1. Jitie moyo kwamba utavuka tu 2. Ongea na mtu anayejali, usijifungie au kuficha. Mwone mshauri ikibidi 3. Wewe ni binadamu ruhusu maumivu na machungu, usiyafiche au kuyakataa. Muda huponya. 4. Kama unaimani, peleka moyo wako uliyoumia kwa Mungu wako. Omba ila usilalamike 5. Jipe muda wa uponyaji (acha kuvuta hisia za mumivu) 6. Jifunze kitu kwenye tukio zima 7. Tafuta kitu cha kushukuru au kuwa positive hata kama ni kidogo 8. Kama kuna cha kusamehe basi samehe na achilia Mtu wa kwanza mwenye mchango mkubwa wa kukutoa hapo ulipoumizwa ni wewe mwenyewe # Sms Tamu za kumtumia Mpenzi wako, ili kumuonesha kwamba unampenda.

NAJUA MTATOA MAPOVU SANA ILA TOENI LAKINI HUU NDIYO UKWELI!

Image
Wanawake wengi wanadhani kuwa wanaweza kumpangia mwanaume namna ya kulea mtoto wake ambaye alizaa nnje ya ndoa, namna ya kuwasiliana na Mama wa mtoto, namna ya kumhudumia Mama wa mtoto wake ila ukweli nikuwa hawawezi. Mtoto akishazaliwa anakua na haki zote sawa na mtoto wa ndani ya ndoa, ni mtoto wake na kiwango cha DNA ni kile kile. Unapokubali kuwa mume wako, mpenzi wako au mchumba wako kazaa na mwanamke mwingine b asi kubali pia kuwa, huyo mwanaume ataendelea kuwasiliana na huyo mwanamke aliyezaa naye mpaka wanaingia kaburini. Yaani mawasiliano yao yatakoma pale ambapo mmoja wapo kati ya watatu anakufa, awe ni mwanaume wako, mtoto au mwanamke. Ubaya ni kwamba, huwezi kumpangia mwanaume eti asiongee na Mama wa mtoto wake, eti asiende kumuona mtoto, eti asimpost mtoto, asimsomeshe na vingine vingi. Ukipata mwanaume anayejielewa basi jua atajiheshimu, atawasiliana na huyo mwanamke mwingine kimya kimya na hatakuambia chochote. Ukipata ambaye hajielewi basi jua kuwa atakua anaongea...