ACHA KUWA KIAZI, MKISHAACHANA MMEACHANA HAKUNA KUACHANA VIZURI!
Dada zangu hembu jitambueni hata kidogo hivi mwanaume ulikua naye kwenye mahusiano, kakutumia wee kakuchakaza, mwisho kakuacha kaenda kuoa mwanamke mwingine. Baada ya muda anakuja kwako na kukuambia kakukumbuka, unakubali unamrudia, kila siku unagombana na mke wake bila aibu unamuambia “Wewe umeolewa lakini mimi ndiyo napendwa!” Dada, kwa taarifa yako hata magunia ya deki yanapendwa ila yanaishia kufutiwa miguu tu!
Kama alikuacha kipindi hana mke sasa hivi anarudi kwako kufanya nini? Ukiona mwanaume kakuacha, kaenda kuolewa na karudi kwako basi jua kuwa anakudharau! Anaona kabisa kuwa wewe huna maisha bila yeye. Lakini wakati mwingine hata hamkuachana kwa kuchokana, hapana, mwanaume mlikua mnapenda, labda mkaachana kwasababu ya Dini au Kabila, wazazi hawataki, lakini nyie bado mnapendana.
Ameenda kaoa anarudi mnaendelea naye, aisee hakuna kitu kinapoteza muda kwa mwanamke kama kuendelea kufanya mapenzi na X wako ambaye mlikua mnapendana. Dada zangu, mwanaume mkiachana bila kujali sababu za kuachana basi kata mawasiliano naye, yaani hata akifa msiba wake usipost, achana na haya mambo ya hatukuachana vibaya, aisee inaharibu maisha yako.
Inawezekana kweli anakupenda kuliko mke wake, lakini yule ni mke. Inawezekana kuwa anakujali ila kama hamkuoana basi hamkuoana, yaani hamtakuja kuoana. Umekaa hivyo, baada ya muda unashangaa una miaka 40, mwenzako bado ni mume wa mtu, anafamilia yake, umemsaidia kafanikiwa, ana maisha yake, ila kumbuka hayo mafanikio ni ya wewe na mke wake. Itakula kwako acha huo ujinga, aisee, kuendelea kuwasiliana na mume wa mtu kisa wewe ndiyo unapendwa wakati alikuacha na kuoa huo ni UKIAZI!
Nishamaliza ila kasirikeni basi hata muache!
Comments
Post a Comment