MWANAMKE ANAPOUMIA HAIMFANYI ASIPENDE TENA KWA SABABU KWAKE KUPENDA NI WITO JAPO TATIZO NI NAMNA GANI ATAAMINI BAADA YA KUUMIZWA🤷‍♂️


Maisha ya Mwanamke huchanua tangu angali msichana, namna nzuri ya kuamini juu ya UKOMBOZI WA MWANAMKE NI BAADA YA KUJENGWA KATIKA MSINGI WA KUJITEGEMEA MWENYEWE.
Familia zilizo nyingi zinamjenga BINTI katika kuiheshimu NDOA hata kama itakuwa haileti UKOMBOZI MAISHANI MWAKE na hilo ndilo anguko kubwa la maisha ya Mwanamke 😭😭
Mwanamke akiishi kwenye mafunzo ya kuiabudu NDOA basi hata awe mwenye ELIMU kubwa kiasi ATAISHI KAMA MTUMWA.
Mwanamke akijikomboa ki fikra kamwe hataishi kwa kuogopa:-
 JAMII.
 MUME.
 DINI.
 MWANAMKE MWENZIE.
Mwanamke aliyejikomboa kamwe hataangalia DUNIA ITASEMA NINI bali atakuwa YEYE na wala hataruhusu KITU AMA MTU aingilie UHURU WA NAFSI YAKE 
Wanawake wengi wameangamia kwa kuangalia DUNIA ITASEMAJE na kujikuta wameangukia kwenye NDOA zilizojeruhi maisha yao yote, Kila kukicha anashukuru MUNGU na kujisemea siku moja MUNGU ATALETA MUUJIZA KWAKE huku akisahau anguko lake lilijengwa na MALEZI YAKE😭😭
Elimu ya mzazi kwa binti yake hiyo inaweza kuleta UKOMBOZI ama UHARIBIFU wa Maisha yake, Kwa sababu ikiwa BINTI atajengwa katika msingi wa KUOGOPA JAMII kamwe hataona:-
 VIPIGO.
 FEDHEHA.
 UDHALILISHWAJI.
Mbaya zaidi anaweza kusoma vitabu vitakatifu akajua AGIZO LA MUNGU KWAKE NA KWA MUMEWE lakini hataweza kubaini kosa la yeye KUMLEA MWANAUME ambaye aliagizwa kula kwa jasho, KUTAFUTA kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake, Hali hiyo itatokana na WOGA WA KUACHIKA etiiii DUNIA isimcheke😂😂😂





Comments

Popular posts from this blog

SHANGAZI NAE ANATAKA-07

join sugar mumy and dating whatsapp group link