Posts

Showing posts from December, 2019

MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU UNAPOACHANA NA MPENZI WAKO

Image
Watu wengi, wanaume kwa wanawake wakiachwa na watu wanaowapenda kitu cha kwanza kufanya ni kuangalia kasoro zao.  Kujiangalia wamekosea wapi na wanamapungufu gani ambayo yamewapelekea kuachwa. Hali hii huwafanya kutokujiamini na kujiona kama wana  kasoro flani hivyo kuwawia vigumu wanapoingia katika mahusiano mapya.  Lakini hembu nikuulize kama ulishakutana na hali hii je ulishakaa kitambo kidogo na kujiuliza labda tatizo sio wewe. Kwamba kweli kakuacha lakini inawezekana kakuacha kwakua hakuwezi na sio kwamba hufai. Kwamba ingawa wewe unamuona wamaana, unamuona anajiamini lakini yeye hajiamini kuwa na mtu kama wewe. Anajidharau na anaona kama akiendelea kuwa na wewe ipo siku utamuacha na ataumia sana. Sasa nikuambie kitu Kama mpenzi wako kakuacha Kwa matusi, kejeli na vitu kama hivyo. Kuna uwezekano mkubwa hajiamini au alishaona dalili kuwa unaelekea kumaucha na kaona akuche mapema ili aibu iwe kwako. Kwamba usije ukaringa kuwa umemuacha kwakua yeye ndiyo ka...

Kifo Mikononi Mwangu (Sehemu ya 10)

Image
ILIPOISHIA WIKIENDA… NILIPOSHUKA tu nikamuona mwenyekiti akichungulia mlangoni. Aliposikia gari linasimama nyumbani kwake akachungulia. “Vipi afande?” Akaniuliza. “Mlipoondoka nikakumbuka kwamba nilisahau kitu.” “Kitu gani?” “Nilisahau kumuonesha picha za watu wawili ambao tunawashuku. Huenda huyo aliyemuona akawa mmojawapo.” “Sasa ameshakwenda nyumbani kwake.” “Tafadhali nipeleke anakoishi.” Ingawa hapakuwa mbali na nyumbani kwake, mwenyekiti huyo alinipeleka nyumbani kwa msichana huyo. Nyumba aliyokuwa anaishi ilikuwa ikitazamana na nyumba aliyokuwa akiishi Matilida. SASA ENDELEA… N ILIVYOPIMA zile nyumba zilivyo, niligundua ni kweli ulikuwepo uwezekano wa Salma kumuona Matilida akishuka kutoka kwenye teksi. Hata hivyo, kwa vile ilikuwa usiku inakuwa ni vigumu kuigundua sura ya mtu. Pengine ndiyo sababu alishindwa kunitambua. Mwenyekiti aliposhuka kwenye gari na mimi nikashuka. Mwenzangu alitangulia kufika mlangoni, akamuita Salma. Mpaka mimi nafika kando ya mlango huo,...

Kifo Mikononi Mwangu (Sehemu ya 9)

Image
“NIMEKUWA na shaka naye sana. Katika pitapita zangu nilipata habari kwamba huyu Mabruki alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Matilida. Nilisikia siku aliyouawa Matilida, Mabruki alikuwa ameegesha gari lake nyumbani kwa akina Salma, huyu msichana niliyekuja kumuonesha picha.” Nikaendelea kumwambia. “Sasa wasiwasi wangu isijekuwa kulikuwa na mambo ya kufumaniana kati ya Mdachi na Mabruki na kusababisha Mabruki amuue yule msichana….” ILIPOISHIA IJUMAA… Sikukumbuka kwamba usiku ule niliporudi na Matilida niliona gari hilo kwenye ile nyumba. Lakini kama lilikuwepo, basi ni Azzali Mabruki aliyemuua Matilida. Alituona wakati tunashuka kwenye teksi na akatambua kuwa nilikuwa ni mimi. Baadaye akaja kubisha mlango. Matilida alipomfungulia, akampiga chupa ya kichwa na kuondoka. Hili suala nisingeweza kulichunguza peke yangu. Ilinipasa nitengeze hoja ya kulifikisha kituoni ili Mabruki akamatwe. SASA ENDELEA… BADALA ya kurudi kituoni nilikwenda Gofu kwenye Baa ya Nane Nane, nikamuona yule ...

Utafiti: Kutokula Kunarefusha Maisha

Image
Utafiti uliofanywa nchini Marekani, umebaini kuwa kutokula kwa saa 16 hadi 18 au kufunga kula kila baada ya muda fulani ndani ya wiki kunarefusha maisha na kuzuia magonjwa kama shinikizo la damu. Matokeo ya utafiti huo yalichapishwa na jarida la New England Medicine, na kubainisha kuwa kula ndani ya saa sita hadi nane kwa siku na saa zilizobaki kukaa bila kula kunaongeza nguvu ya kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. kwa mujibu wa mamlaka hiyo ya tafiti za kisayansi, kufunga kula ni moja ya njia zinazopendekezwa kwenye matibabu ya kiribatumbo, kisukari na magonjwa ya moyo. “Inapendekezwa mtu afunge siku mbili kwa wiki au kula kiasi kidogo cha chakula kila siku” imeeleza sehemu ya utafiti huo. Utafiti huo uliofanywa kwa kutumia sampuli za binadamu na wanyama, umeeleza kuwa kurefusha maisha kunatokana na kuhuishwa kwa chembe hai za mwili.

UKIKOSA SABABU; USIVUMILIE KWENYE MAPENZI

Image
N IMEWASIKIA  washauri wengi wakisema uvumilivu ni kitu muhimu katika mapenzi! Bila shaka hata wewe umewahi kuambiwa na wazazi au rafiki zako “vumilia tu” ukiaminishwa kuwa ndoa au mapenzi yana changamoto nyingi zinazohitaji uvumilivu. Kama hujui, uvumilivu ni mzigo mzito; ukikubali kuvumilia, lazima uwe na sababu ya kufanya hivyo. Ukikosa sababu ya kuvumilia katika mapenzi hutakuwa tofauti na mtu aliyebeba furushi zito kichwani halafu hajui alipeleke wapi na wakati gani atalitua na kwa faida gani. Kamusi ya Kiswahili inaeleza maana ya uvumilivu kuwa ni; “Hali ya kustahimili machungu.” Huku kamusi hiyohiyo ikitafsiri ‘machungu’ kama matatizo makubwa yanayosababisha masikitiko. Ukiambiwa vumilia maana yake uwe tayari kustahimili matatizo makubwa yatakayoleta masikitiko ndani ya moyo. Kwa kisingizio hiki kuna baadhi ya wanawake wanakesha wanalia kwa manyanyaso yasiyokoma kutoka kwa wapenzi wao. Ukiwauliza kwa nini hawaachani na matatizo hayo makubwa watakuambia; “Tunavumilia.” La...