Utafiti: Kutokula Kunarefusha Maisha
Utafiti uliofanywa nchini Marekani, umebaini kuwa kutokula kwa saa 16 hadi 18 au kufunga kula kila baada ya muda fulani ndani ya wiki kunarefusha maisha na kuzuia magonjwa kama shinikizo la damu.
kwa mujibu wa mamlaka hiyo ya tafiti za kisayansi, kufunga kula ni moja ya njia zinazopendekezwa kwenye matibabu ya kiribatumbo, kisukari na magonjwa ya moyo.
“Inapendekezwa mtu afunge siku mbili kwa wiki au kula kiasi kidogo cha chakula kila siku” imeeleza sehemu ya utafiti huo.
Utafiti huo uliofanywa kwa kutumia sampuli za binadamu na wanyama, umeeleza kuwa kurefusha maisha kunatokana na kuhuishwa kwa chembe hai za mwili.
Comments
Post a Comment