Chunga sana kitu hiki kwenye mahusiano yako ya ndoa
Miongoni mwa mambo yanayopelekea mahusiano mengi ya ndoa kuvunjika ni pamoja na kutoa baadhi ya vitu, maneno au matendo yanayoihusu ndoa yenu kuwapelekea watu wengine ambao si wahusika wa ndoa hiyo.
Wapo baadhi ya watu waliopo kwenye maisha ya ndoa wao hata uwafanyie nini basi wao kukaa kimya huwa huwawezi, wao ni wazuri sana wa kusimulia kila kitu kinachondelea kwenye ndoa.
Utawasikia wakisema mara mke wangu jana kaniletea hiki, mara oooh mume wangu anapenda hiki, mara wengine mke wangu jana sijui kafanya kile na maneno mengine kama hayo. Kitendo hiki kwa upande wako huenda ukakiona ni cha maana ila ukweli uliyo wazi kitendo hicho si kizuri hata kidogo.
Kitendo hicho si kizuri kwa sababu unapoweka wazi kila kitu ambacho kinaendelea kwenye mahusiano yako ya ndoa basi unatengeneza mianya ambayo mbeleni hupelekea mahusiano hayo kufa kabisa.
Unapowasimulia watu wengine kile kinachoendelea kwenye mahusiano yako unawapa nafasi watu wengine wayajue mahusiano hayo hususani suala la madhaifu ya ndoa yenu.
Pia wakati mwingine inakuwa ni rahisi kwao kuweza kutoka hata kimahusiano na yule uliyenaye kwenye mahusiano hii yote kwa sababu wewe mwenyewe umeamu kuyaweka bayana yale yanayoendelea.
Hivyo ewe mwanandoa unapaswa kuyalinda mahusiano yako ya ndoa ili yasivunjike kwa kuhakikisha unalinda taarifa zinazohusu ndoa yako kuwasimulia wale wasiyohusika.
Na; Benson Chonya.
Comments
Post a Comment