Mambo 8 mwanamke anapaswa kufanya kabla ya kufunga ndoa
Kufanya mambo haya kutakupatia maarifa na kukufanya uwe na uwezo wa kufanya uamuzi bora zaidi maishani. Ni jukumu lako kama binti asiye katika uhusiano kufanya mambo mazuri zaidi maishani kabla ya kufunga ndoa. Kufanya vitu hivi kutakusaidia kuwa mwerevu zaidi na kujua mambo unayo na usiyo paswa kufanya. Soma makala yetu ya mambo ambayo mwanamke anapaswa kufanya kabla ya kuingia katika ndoa!
1. Jifunze jinsi ya kupika
Tofauti na imani za watu kuwa kila mwanamke anapaswa kujua kupika ili ampikie bwana yake, kujifunza kupika kwa mwanamke kuna umuhimu tofauti. Ukiwa peke yako bila mchumba, una wakati mwingi, kwa hivyo katika wakati huu, utaweza kujipikia vyakula vinavyo kufurahisha zaidi. Pia, unapo pata wageni utaweza kuwa burudisha na ustadi wako wa mapishi.
2. Fanya vitu vinavyo kupendeza katika wakati wako wa ziada
Unapokuwa peke yako, una wakati mwingi wa mapumziko, ni vyema kufahamu vitu unavyo vipendelea, katika wakati huu, utaweza kuvifanya badala ya kubaki kwenye nyumba ama kulala wakati wote. Kufahamu mambo yanayo kufurahisha kuta kusaidia kuto mngoja mchumba wako wakati wote ili mfanye mambo pamoja. Ni muhimu sana kuwa na maisha yako kando na maisha yenu pamoja kama wachumba.
3. Kuvunjwa moyo
Ni kawaida kuwa na hofu ya kuvunjwa moyo, lakini usipo ingia katika uhusiano na kugundua mambo usiyo paswa kumkubalisha mpenzi wako afanye, huenda ukafanyiwa mambo haya na wakati huo hauna chaguo la kutoka kwa ndoa ni ya muda mrefu.
4. Kufahamu maoni yako kuhusu watoto
Katika siku za hapo awali, ilikuwa lazima kwa mwanamke kupata watoto katika ndoa. Ila siku hizi mambo yame badilika na wanawake wana weza kuchagua ikiwa wangependa kupata watoto ama la na pia idadi ya watoto ambao wangependa. Unapo fanya hivi, utakuwa wazi na mchumba wako na kugundua kama mna maono sawa, ili kuepuka vurugu za kuwa na maoni tofauti kuhusu mada fulani.
5. Zuru
Kuzuru kuna kusaidia kuona pande tofauti za dunia na kupatana na watu mbalimbali. Kufanya ziara peke yako kuna kusaidia kuwa jasiri zaidi. Huenda ikawa vigumu kufanya hivi unapo ingia kwenye uhusiano na baadaye kupata watoto kwani una majukumu zaidi na hauna wakati tosha. Kwa hivyo, hakikisha unafanya hivi ungali peke yako kabla ya kuingia kwenye uhusiano.
6. Soma mambo tofauti
Ni kawaida kuwa na mambo machache ambayo ungependa kufahamu jinsi ya kuyafanya na hata kupata vyeti zaidi. Ungali peke yako, una wakati tosha wa kufanya hivi. Kwa hivyo hakikisha unapata vyeti zaidi katika kipindi hiki.
7. Tengeneza malengo yako ya kifedha
Ni rahisi kuwa na majaribio ya kutumia fedha zako kiholela holela kwani wakati huu hauna majukumu mengi. Fahamu umuhimu wa kuhifadhi pesa hasa katika kipindi ambacho mambo yanaenda mrama. Unaweza anza kuwekeza baadhi ya kiwango cha fedha zako.
8. Anza kufanya mazoezi
Mazoezi haya kusaidii kuwa na mwili unao pendeza tu, mbali kuwa na afya nzuri ya kiakili na kihisia. Kwa hivyo hakikisha kuwa umejiunga na darasa za kufanya mazoezi.
Comments
Post a Comment