USIVUNJE UHUSIANO/NDOA YAKO KWA SABABU YA PENZI ULILOKUWA UNALI-WISH⛔️

ULIYE NAE NI ZAIDI YA ANAYEKUJA KWANI STAREHE YA KITANDANI NI KWA DAKIKA LAKINI UPENDO NI WA KUDUMU💯
Mapenzi ni kama kupenda taarifa za habari ama matukio kupitia GAZETI, INSTAGRAM, FACEBOOK na MENGINEYO Muda mwingine unahitaji taarifa tofauti kwa uandishi lakini maana ya UJUMBE NI ILE ILE🤦‍♂️
Ila UPENDO ni jambo adhimu mnooo, Ndo maana Wengi tunajikuta TUNALILIA WATU kisa Mapenzi😂😂
Hatari kubwa DUNIANI ni kumpoteza Mtu uliyejenga nae DHAMANA MOYONI halafu kisa eti hakupi raha unayoisikia kwa mashoga ama marafiki💯
Wakati unamuacha automatically ataumia sana, Pengine hata akaanza kutengeneza namna nzuri ya kujiponya, wakati huo wewe utakuwa umejipa TUMAINI LA PENZI ULITAKALO huku ukiwa umepofuka kwa mahaba ya mpito, Niamini hakuna Mtu mke ama Mtu Mme anampenda Mke au Mume wa Mtu⛔️
Anayesaliti penzi ni FISADI WA MAPENZI ametawaliwa na ubinafsi pamoja na tamaa kwa lugha fupi ANA HISIA ZEMBE😂😂
Madhaifu hata YAWE makubwa kiasi gani kwenye MAHUSIANO ama NDOA yako uyabebe kama yalivyo, Maana tayari umeingia penzini huna sababu ya kutoka kwa sababu kuna Mwingine anasema yale uliyahitaji awe nayo mwenza wako, Maana siku zote AJAYE NI MPYA lakini ukimjua atakuwa ZILIPENDWA📌
Gharama ya kulifufua PENDO lililokufa ni WEWE KUFA je ukifa kuna haja ya kulifufua?
BAKI NJIA KUU hata ukipotea ni rahisi kupata msaada, Kuliko kupita NJIA YA MKATO lilikupata la kulitafuta usijelalamika😂😂
Wengi wanapenda vilivyoundwa ila hawajari aliyeunda kwani wanaamini ALIYEUNDWA HAJUI THAMANI YA MHUNZI ila kwa sababu wanataka kuona uundwaji ule WATAPITA nawe utabakia na majuto yako👋
Maana hakuna kizuri hakina mwenyewe, ila kwa hali ya Mahusiano na Ndoa za Sasa wengi TUNATUMIANA na mtu akijua anakata tamaa, Kuliko kumuacha mtu kwa sababu ya Mtu mwingine basi JIFUNZE hili:-
👉 TAFUTA SABABU YAKO BINAFSI UNAYOAMINI HIYO NDIYO CHANZO CHA WEWE KUWAZIA KUACHANA KWANI ITAKUPA NGUVU YA KUTOKUJUTIA UTAKAPOACHANA NAE💯
Haya mambo ya Mahusiano ama ndoa mpya kisa uliyenae anasumbua UTAKUJA KUJUTAAA kwani hujamaaliza tatizo unaanzisha tatizo jingine😆😆
utamuwote





Comments

Popular posts from this blog

SHANGAZI NAE ANATAKA-07

join sugar mumy and dating whatsapp group link