ULITAKA NINI WAKATI UNAANZISHA UHUSIANO NA MWENZAKO?
Mpenzi wangu msomaji Ni kwa vipi uingie katika mahusiano na binadamu mwenzako halafu utumaini kila siku akufurahishe? Hiyo inawezekana vipi? Wewe unaweza kumfanya mtu kila siku akawa na furaha isitokee hata siku moja ukamkwaza?
Ni kweli hatutakiwi kuingia katika mahusiano tukiwa na tunajua fulani ni lazima atakuumiza. Haipaswi kuwa hivyo.
Lakini jiulize ni vipi unaweza kuishi na binadamu asikukwaze siku hata moja?
Haya sasa chukulia kuwa umeingia katika mahusiano na mtu ukiwa na tumaini la kuwa katika furaha ya kila siku, halafu siku ikatokea kakukwaza itakuaje?
Si mwanzo wa kuona kuwa umeingia katika himaya ya mtu asiye wa ndoto yako?
Si mwanzo wa kuanza kuangalia njia ya kutaka kujitoa hapo? Tafakari.
Siku zote ndiyo maana huwa nasisitiza watu waingie katika mahusiano kwa kigezo cha kupendana kwanza. Mengine ndiyo yafuate.
Ukiwa katika mahusiano na mtu umpendaye kwa dhati na akakupenda pia. Hapo ndipo kwenye furaha.
Hapo ndipo hata makosa yake utayatizama mara mbili mbili.
Ni mara chache itatokea kujialaumu ukiwa na mtu wa aina hii.
Hapa ndipo hata angalau matarajio yako ya furaha yatapatikana ingawa si kwa siku zote.
Binadamu si malaika bwana!
Kabla mtu hajaamua kuingia katika mahusiano ya kimapenzi ni vyema sana akajua amengia katika mahusiano na mtu wa aina gani? Ayajuae matarajio yake katika mahusiano husika.
Kuna umuhimu wa kuyajua hayo!
Maana kuna wengine wanataka kuingia katika mahusiano kwa ajili ya kutaka kupata faida kana kwamba ni biashara.
Wengi wameingia katika mahusiano na watu wa aina hiyo. Angalia mahusiano yao utajua ninachomaanisha.
Katika hali kama hiyo ni mtu mmoja tu atakuwa na furaha huku mwingine akihisi anatumika na kusagika.
Sasa hayo mapenzi au utumwa?
Unaweza kusema uko katika mapenzi kwa namna hiyo?
Kila mmoja ana nafasi ya kufurahia na kuona raha ya mapenzi.
Ila kitu cha msingi ni kuangalia na kumsoma mwenzako mapema.
Usije ukaingia katika mahusiano na mtu mwenye matarajio tofauti na kimapenzi.
Hali mbaya ya kimaisha imesababisha baadhi ya watu watumie mapenzi kama mradi. Wana uwezo wa kuigizia ukajua wanakupenda kumbe lengo lao ni kutaka kukutumia na mwishowe kukuacha kwenye mataa.
Kuwa makini.
Kwa wengi mapenzi yamegeuka mradi. Ukizubaa wanaweza kukufanya ndiyo mteja wao.
Kwa leo niishie tutakutane kesho panapo malaaliwa .
ILA BINAFSI NAIHUSIA SANA NAFSI YANGU .
Comments
Post a Comment