ANZA MAISHA UPYA, KATAA MAUMIVU KARIBISHA FURAHA NA AMANI
Mpenzi msomaji, kwa sababu ya amani na furaha ya maisha yake.
Kama upo katika uhusiano wa amani na furaha, unatakiwa kuamua kuwa bora zaidi ili amani na furaha yako iweze kuendelea.
Ni vigumu sana kuendelea kufurahishwa na mwenzako ikiwa unafanya matendo ya kumuudhi na kumuumiza.
Kuanzia leo, kama unataka kuona amani na raha uliyo nayo katika uhusiano wako inaendelea, kuwa mtu bora na mwafaka katika maisha yake.
Kwa kila kitendo unachotakiwa kufanya hakikisha unakifanya kwa namna inayotakiwa, ila pia kwa kila jambo unalotakiwa kukaa nalo mbali hakikisha unaliepuka ili uweze kumfanya kuwa na amani na utulivu wa nafsi.
Kwa maendeleo ya furaha yako, amua kumpa amani na raha mwenzako.
Katika uhusiano, raha huwa ni kitu cha kusababishwa, hasa mkiwa mnapendana.
Yaani kama unataka akupe raha na amani, inabidi umsababishe yeye kuwa na amani na furaha.
Kiasili, binadamu ana tabia ya kutaka kulipiza kisasi.
Kama ukimfanyia ujinga leo, kuna hatari hata yeye kukufanyia ujinga kesho.
Hali hii kwa wengi inaweza isionekane leo au kesho.
Wewe kila siku unaweza kumfanyia mwenzako matendo yasiyostahili na ukadhani hajali, ila tambua kuna kitu kitakuja.
Siku atakayosema hapana, na kila kitu katika maisha yako kitabadilika.
Kwa mahitaji ya amani yako ya kesho, anza kumpa amani yeye leo.
Wengi wenye furaha na amani katika maisha yao ya kimahusiano walianza kutoa amani kwa wenzao kwanza. Walikuwa wapole na wenye maneno mazuri, wakawa bora katika nyanja za kimahusiano na hatimaye wamewafanya wenzao waanze kuwatizama katika namna inayotakiwa.
Huna amani katika uhusiano wako?
Kila siku kwako ni ugomvi na karaha, hakuna thamani wala maana ya kuwa katika uhusiano? Umejaribu kila kitu kwa ajili ya kuleta amani katika uhusiano wako umeshindwa?
Umekuwa mpole, ukawa mnyenyekevu, ukajifanya pia mjinga ili ajue thamani na hadhi yako katika maisha yake ila ameendelea kuwa tofauti?
Kataa kuendelea kuwa katika uhusiano wa namna hiyo!
Kila mmoja anahitajika kuwa na mtu anayempenda na kumheshimu.
Amjali na amthamini kwa kiwango cha kipekee na namna iliyo bora.
Mapenzi hayapimwi kwa maneno, ili iwe kweli anakupeda inabidi aoneshe kwa matendo na wakati mwingine kuthibitisha kwa kauli.
Sasa kama anakutesa na kila siku anakusababishia maumivu ni kwa namna gani tuseme anakupenda?
Kuwa makini. Anza kumsoma mwenzako vizuri. Chunguza matendo yake kwa kina kuujua ukweli.
ITAENDELEAA..
Comments
Post a Comment