MWANAUME KUJITAMBULISHA KWENU HAIMAANISHI KUWA ATAKUOA.
Dada zangu ambao kila mkitongozwa mnaanza kusema “Kama unanipenda kweli twende ukajitambulishe kwetu ndiyo tufanye mapenzi!” Dada nikuambie kitu wazi tu, kama hutaki kufanya mapenzi kwakua una imani ya kidini hapo nakuelewa, subiri mpaka ndoa na naamini kwa imani yako Mungu atakufungulia na kukupa mume sahihi siku moja. Lakini kama hutaki kufanya mapenzi eti mpaka mwanaume ajitambulishe au akuoe basi utatambulisha wengi sana na ndoa utaishia kwenye kutoa michango tu labda nikufafanulie kidogo.
(1) Asilimia kubwa ya wanaume, wanapotongoza huwa wanataka ngono tu, na mwanaume wa namna hii atafanya chochote ili akupate, hata kujitambulisha kwenu atakuja na tabia atabadilisha ili tu kukupata ila akishakupata ndiyo anapotea kabisa.
(2) Kuna wanaume kweli wanakuja kwa nia ya kuoa, ila mwanaume ambaye humjui vizuri, labda hukukua naye, hakua rafiki yako, hujui maisha yake ya nyuma, umekutana naye tu miezi miwili anatangaza usikurupuke na kudhani una ngekewa, kweli kuna ngekewa lakini mara nyingi wanakua na matatizo. Moja ya matatizo nikuwa ametoka kuachwa na X wake kaolewa hivyo anataka kuoa ili kulipa kisasi. Ni kicheche sana wanawake zake wanamuacha au hawataki kuolewa naye hivyo anajua akichelewa utajua madhaifu yake.
(3) Hii sababu sasa ni kubwa, tena hii mfano mwanaume kama si mlokole au mtu wa dini sana, hapa nazungumzia wale watu akitembea ananukia dini kabisa sio wale wa kanisani au msikitini mara moja, akikuambia kuwa msubiri mpaka ndoa, au akakuomba mechi ukakataa ile sitaki na taka lakini yeye wala hakusisitizia. Anajidai kuwa hataki akuchezee atafanya na wewe mpaka ndoa, tena akakuambia kabisa kuwa lengo nikuoa lakini mecho hamna basi kuwa makini sana na mtu huyu.
(4) Sio wote na sikuambii hivi ili mutest ila wengi wanakua hawana nguvu za kiume au mechi kwao shida. Narudia wengiii, yaani wadada wanaonipigia simu ndoa za zima moto wengi wamefika wamekuta yaliyomo hayamo. Wanaume hawa wanakua hawataki kufanya kabla kwani wanajua kuwa ukijaribu tu utakimbia, wana hofu. Sikuambii utest ila una akili zako zitumie vizuri acha kukurupukia ndoa, mtu anakuja kwako ana miaka 35 anakutangazia ndoa unapaparika kana kwamba eti hajawahi kuona mwanamke mwingine huko nyuma akataka kumuoa wewe uko peke yako!
(5) Kuna tabia nyingine kama ulevi, kupiga na vitu vingine vingi. Hivyo hata hata kama kweli unataka kusubiri mpaka ndoa basi chunguza kidogo, umjue, ishu si kujuama miezi miwili ishu ni unajua nini kuhusu huyo mwanaume tofauti na alichokuambia yeye. Mnaweza kukaa mwaka lakini kama humjui, hujui familia yake vizuri, hujui maisha yake ya nyuma, kwanini aliachana na X wake, hata kazini kwake hujawahi kufika na hupajui, hujui hata ndugu yake mmoja, kabla ya kuingia kichwa kichwa tulia kwanza jua mambo.
(6) Ushauri wangu tu ni kwamba kama sio mtu wa dini, kama kinachokuumiza kichwa ni kuchezewa na kuachwa basi angalia vigezo hivi! Je anakuvutia, je anakuheshimu, je ana afya njema mmepima na wote kujijua hali zenu, je dini zenu zikoje, wewe upo tayari kubadilisha na ndugu zako watakuruhusu kubadilisha? Nasema wewe kwakua wanaume ni wachache sana wanakubali kubadilisha na ishu ya dini ni kubwa sana, haikuhusu wewe tu bali inagusa na wazazi, mengine ni mbwembwe tu, usitake mtu aje kwenu kujitambulisha ili tu umpe mwili wako!
Comments
Post a Comment