KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA MJUE MWANAUME WAKO?
Kama upo kwenye mahusiano ambayo unaona kabisa yapo siriasi na yanaweza kuelekea kwenye ndoa basi kuna vitu vidogo vidogo ambavyo kama mwanamke unatakiwa kuvijua. Wanawake wengi huharibu mahusiano yao kwa vitu vidogo ambavyo wanaamini wanavifanya kwa kujenga. Kwa mfano, kuvumilia, kuvumilia huua ndoa nyingi sana kwani wanawake huingia kwenye ndoa kwa kuigiza huku wanaume wakiingia kwenye ndoa wakidhani kuwa wanawake wao wanaridhika na aina ya maisha wanayoishi.
Labda niwape mfano mmoja, mwanamke anaweza kuwa na mwanaume Malaya ambaye anabadilisha wanawake kila siku, wakati wa uchumba asiongee chochote akisubiri wakati wa ndoa ndiyo aongee. Kwakua anabembelezea ndoa anaamini kuwa atabadilika, lakini baada ya ndoa tu mwanaume anaendelea kuwa Malaya huku mwanamke akianza kulalamika kuhusiana na tabia za mwnaaume. Unakuta ndoa ina miezi mitatu tayari washaenda ukweni zaidi ya mara tatu kushitaki.
Mwanamke kabla ya kuingia kwenye ndoa ni lazima umjue mwanaume wako na kujua namna ya kuishi naye. Ujue kuwa mwanaume habadiliki kwenye ndoa bali huharibikia kwenye ndoa hivyo ni lazima ujue namna ya kudili naye kabla ya kuingia kwenye ndoa. Wewe kwenda kumlalamikia kwa Mama yake, Baba yake haitakusaidia chochote zaidi ya kuwasumbua wazee watatu. Ni lazima ujifunze namna ya kuwa na furaha yako na namna ya kudili na matatizo ya mume wako bila kuwa mtu wa kulalamika na kulia kila siku.
Comments
Post a Comment