Posts

Showing posts from April, 2020

KINA DADA NIONGEZE SAUTI WAU MTAJIREKEBISHA

Image
Usibebe mimba mtu ajielewi leba sio mlimani city πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ™πŸ½ πŸ™πŸ½ πŸ™πŸ½ Umebeba mimba badae unasema huyu mwanaume kanitumia kanidanganya..sasa dada angu unabeba mimba ya mtu kasema tena kwa mdomo tu ntakuja kwenu nakupenda siwezi kukuacha yaani hata uakika wa maisha nae una unatoa zamana ya mwili kuingia leba nusu kufa kule kisa mwanaume mweu tu ambaye katumwa na shetani bomoa maisha yako

NAOMBA UFAHAMU HILI

Image
Kwenye maisha kila mtu anapitia maumivu na magumu ya hali ya juu........ Ijapo kuwa kila mmoja anapitia maumivu na magumu kwa muda wake lakini mwisho wa siku hupita na maisha lasmi huendelea lakini bado haija tufanya kuya sahau magumu hayo na maumivu. Kuna muda mtu analia kwa kuwa ame achika katika ndoa yake kisa kazidisha chumvi kwenye mboga, kuna muda mtu analia kwa kuwa amefiwa ,kuna muda mtu analia kisa kutelekezwa na mimba ama mtoto pia wapo wanao lia kwa kuona msiba kw ao lakini sababu inayo wafanya walie marehemu ndiye alitakiwa kuwa muandaaji na msimamizi wa msiba huo. NAOMBA UFAHAMU HILI: Siku zote katika maisha hakuna mwanadamu anaishi kwa raha tu na starehe hapana, ili uwe binaadamu ulie kamilika lazima tu utapitia mambo tofauti tofauti na mengi ya kukufanya uumie ila uimara wako ndio kitu pekee kitakacho kufanya uishi kwa kujiamini ni uvumilivu wako.

KWA WALE WANAOTARAJIA KUOA/KUOLEWA

Image
*Usioe wala kuolewe kwasababu ya sex. *Usioe wala kuolewe kwa sababu tu umri wako unakuruhusu. *Usioe wala kuolewe kwa sababu umechoka kuwa single. *Usioe wala kuolewe kwa sababu umempa/umepata mimba. *Usioe wala kuolewe kwa sababu ni mzuri au anapesa sana. *Usioe wala kuolewe kwa sifa. *Usioe wala kuolewe kwa sababu tu unapenda harusi. *Usioe wala kuolewe kwa sababu eti marafiki zako wote wameoa/wameolewa. But: -Get married, because you want to fulfil destiny. -Get married because you want to be a helpmate to an imperfect person who loves & accepts you for who you are, not who you pretend to be! -Get married becos you want to fulfil your promises. MY PRAYES FOR YOU: *Mwenyezi Mungu akushike mkono ktk kufanya

USIOLEWE ILI UKATUNZWE:

Image
Usijione kwa sababu Wewe ni Mtoto wa Kike ndio unastahili kuwa pangu pa Kavu, ACHA UJINGA. Usifanye KUOLEWA ndio SULUHISHO la Matatizo yako, ndio SULUHISHO la UCHUMI wako. Kuna mabinti sijui ni Uchovu au kukata tamaa, utawakuta wanalia na kuomba “Bwana YESU nipe mume nataka kuolewa, anachana Nywele kwa Mtindo mbalimbali ili Vijana wamuone, huo ni UJINGA. USIOLEWE ili UKATUNZWE, OLEWA ili Kutimiza MAKUSUDI YA MUNGU, HUOLEWI ili Mtu AKUTUNZE, Unaolewa kwa sababu unataka kutimiza RATIBA YA MUNGU, Sio Unaolewa kwa sababu unaona pale Nyumbani WAMEKUCHOKA au maisha ni magumu, HAPANA. OLEWA kwa sababu UNATIMIZA Makusudi na Ratiba ya MUNGU kwani Yeye amesema si vema mtu awe peke yake.

Njia 10 za kujenga uwezo wa kujiamini

Image
1. Kuchagua mavazi Ingawa mavazi hayatafsiri moja kwa moja hali ya mtu, lakini katika lugha ya mawasiliano yasiyokuwa na sauti uvaaji wa mtu ni utambulisho wake. Hivyo kama mtu hazingatii uvaaji unaokubalika katika jamii anakuwa katika wakati mgumu wa kujiamini, hasa kama akilini mwaka yeye mweyewe atatambua kuwa amevaa vibaya. Hii ina maana kwamba kama mtu anataka kujenga hali ya kujiamini, lazima achague mavazi yanayoendana na mazingira na yawe ni mavazi ambayo mwenyewe akiyafikiria yahatamfanya ajione ni wa tofauti kwa wenzake. Mavazi hujenga muonekano, ukionekana vizuri mbele za watu utajiamini, hivyo kuwa makini na uchaguzi wa mishono ya nguo unazovaa kila siku. 2. Kutembea haraka Njia rahisi ambayo imethibitika kuweza kumuondolea mtu hali ya kutokujiamini ni kutembea kwa mwendo wa haraka. Haipendezi unapokuwa njiani kutembea kama mgonjwa, uliyechoka. Ukiwa hivyo ni rahisi sana kuwafanya watu wakukodolee macho ambayo yatakufanya wewe uhisi tofauti. Utemebeaji wa haraka una...

KAMA WEWE NI MWANAUME NA UKO HIVI UJUE BADO HUJAKAMILIKA.

Image
Kama wewe ni mwanaume ambaye umekuwa ukijijali mwenyewe kwa kujihudumia mahitaji mbalimbali kama vile kujinunulia pafyumu, boksa, nguo na vinginevyo halafu mwenza wako wala humjali, ujue wewe bado hujakamilika. Unakuta mwanaume anaweza kununua nguo za zaidi ya laki moja, lakini hakumbuki kumnunulia mwenza wake japo sidiria au kufuli la shilingi elfu moja na mia tano. Kwa mantiki hiyo, ni kama mapenzi umeyafanya yazoeleke, umemfanya mwenza wako kama ndugu yako wa damu. Unapoac ha kumhudumia mwenza wako kwa kumnunulia nguo za ndani, unategemea nani amnunulie? Usishangae mwenza wako akaingia kwenye mtego wa kuchepuka kwa mtu ambaye anamnunulia au kumpa zawadi hizo mara kwa mara na kumuona kama ni mwanaume ambaye anamjali. Mwanaume aliyekamilika ni yule ambaye yupo tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo kumjali, kumlinda na kumpenda mwenza wake. Unawezaje kusimama mbele ya umati na kujiita mwanaume rijali wakati ni dhahiri huna vigezo kwa sababu huwezi hata kumnunulia...

✍️SOMO✍️PETE YA NDOA.

Image
Nawasalimu Watumishi Wa Bwana Katika jina la Yesu Inawezekana ndio Mara ya Kwanza kujiunga Ukurasa huu wa Moto wa Yesu Naitwa Pastor Richard Nipo Morogoro Veta Dakawa Nakukaribisha kujua historia ya Pete ya ndoa Wengi Tunavaa Pete huwa bado hatuelewi Pete ya ndoa ilianzia wapi na kwanini unapofungishwa ndoa unavishwa Pete hususa kwa wakristo wote. Tufunue Biblia Zetu Tusome;Kutoka;26;29 Luka;15;22-32 Yakobo;2:2-7 Mwanzo;38;18 isaya;3;20-22 ✍️ ✍️ Lengo la SoMo;Tujue Pete za ndoa umhimu wake na historia Yake. ✍️ ✍️ DHIMA YETU MOTO WA YESU: Tujue kweli na kweli ituweke huru. ✍️ ✍️ HISTORIA YA PETE YA NDOA ✍️ ✍️ Pete ya ndoa iliazishwa kuvaliwa na Watu wa Agano la kale katika Falme mbalimbali wakati huo Pete ilikuwa ikivaliwa mkononi kumtambulisha mtu Kama Ni mtawala na mwenye Amri juu ya kitu fulani. Pete hii katika Agano jipya Tunaona Anavishwa mwana mpotevu ikiwa ishara ya kumtambulisha Mwanae kuwa Tena kuwa SI Mtoto aliyekosana na Baba Yake kwa upendo baba Anaamua aangize Al...

UNAMRIDHISHA MKEO/MPENZI WAKO KITANDANI AU UNAJIULIZA KWANINI ANAKUDHARAU WAKATI UNAJIONA UKO SAWA?

Image
Kwenye tendo la ndoa mwanamke anahitaji mwanaume mwenye uwezo wa kumpoteza kwenye hii dunia kwa muda mchache kwa raha za kuzidi!!! Anahitaji mwanaume anayeweza kuwa too emotional kwenye tendo la ndoa SIO KAMA KUKU jogoo anapojisikia anamkurupusha jike akishamaliza anasepa huyoooo.... Sio kila kitu unasubiri maelekezo kama upo chumba cha mtihani. Mwanamke hatakiwi kukupa maelekezo ya nini anataka bali wewe kuwa mbunifu wa kumpa raha zaidi ya anavyotaka mpaka aseme baaaasiii inatosha sasa wewe subiri akuulize kwani ndio umemaliza ujibu ndio uone dharau zake!!!.... Kuwa na body supplies na kuzifikia sehemu ambazo hata yeye mwenyewe alikuwa hajui kama zinaweza kumpeleka dunia nyingine...... Mume inabidi uwe creative/mbunifu sio kila siku uelekeo wako unajulikana ni mashariki tu..... Huna unachokiongeza kila siku unafanya marudio tu..eti unauliza nikushike wapi?! Nifanyaje!!!! My brother kuna muda wa theory na muda wa practical..sasa wakati wa practical unaanza maswali mpaka mtu ...

NAONGEA NA WEWE!!!!

Image
Wewe ambaye miaka mitano (5) ya uchumba, ushamfunuafunua mtoto wa watu kama Sufuria la Pilau msibani utege masikio yako tena uamke kitandani ukae kitako unisikilize vizuri.... Unamjua mwili wake kama unavyojua mabeti ya wimbo wa Taifa, mtoto wa watu amewakataa wanaume kibao wenye malengo nae kwa ajili yako kwamba utamuoa kama ulivyomuahidi. Amepoteza muda wake kwaajili yako Amekuamini wewe. Ametulia anajua ndoa inafuata hivi karibuni halafu wewe ghafla tu unakuja kumzingua na kutangaza ndoa na mtu mwingine. Akikuuliza sababu ya kumuacha yeye unasema siwezi kuoa Mwanamke hajui kukatika kitandani nataka kuoa fundi wa kumiliki kitanda, Ulimfundisha? Kwani unaoa mke wa kujenga nae Familia au unaoa mke wa kwenda kufungua bendi ya kukata viuno? Maana kama nia yako ni kupata mke anayekatika basi ungeenda kuoa Wanenguaji kwenye bendi ya Akudo Impact. Mnaumiza watoto wa watu kibwegebwege na sababu za kijinga, Kwani utakula kiuno all ur life? Au mtajenga uchumi ...

Kama mwanaume, uko tayari kulipa gharama za mahusiano Bora?

Image
UNAPOWASIKILIZA wanaume wengi wakizungumzia kile wanachodhani wao kinawagusa wanawake kwenye mahusiano, utashangaa orodha ya vitu hutawala mazungumzo. Kwa mwanaume wa kawaida, mwanamke anahitaji vitu ili akupende. Utasikia, "Ah, mwanamke pesa. Ukiwa na hela zako bwana, basi." Imani ni kwamba wanawake wanahitaji sana vitu na hivyo ndivyo vinavyowavuta na kuwabakiza kwenye mahusiano. Pamoja na ukweli fulani kwamba vitu navyo vina nafasi yake kwenye mahusiano, hasa kwenye kizazi hiki cha sasa kinachotanguliza thamani ya fedha kuliko kitu kingine chochote, bado huwezi kuthamanisha moyo wa mwanamke na fedha, ingawa ni kweli anazihitaji. Kudhani kwamba baada ya kuhakikisha mwanamke amepata kila anachokihitaji kwa maana ya vitu, basi unaweza kuendelea na shughuli nyingine kwa kuamini umemaliza kazi, ni kutokuelewa mahitaji halisi ya kihisia ya mwanamke. Najua wapo wanawake wasiohitaji kingine chochote kwa mwanaume zaidi ya fedha na vitu. Mahitaji ya kihisia tunayoyazungumzia wa...

USISEME HAKUNA WANAUME WA KUOA AMA WANAWAKE WA KUOLEWA

Image
Jamii tunayoishi imejaa watu tuliokata tamaa na mbaya zaidi tuna wakatisha na wengine tamaa juu ya suala la kupata mwenza wa ndoa na maisha ya ndoa kwa ujumla. Unakuta wanaume tunasema hakuna wanawake wanaofaa kuolewa labda kama kumpa wa kuwapa mimba ili kupata watoto tu.tuna dai wanawake wanapenda pesa tu. wanawake nao wanataka wanaume wa kuwapa mimba tu.Hawataki kuolewa kwa kuamini ndoa ni ngumu na wanaume wote ni sawa,hakuna mwema yaani wote hawafai. Nadhani wengi wana macho lakini hawaoni,wana masikio lakini wanasikia habari mbaya tu.Yaani ndoa zote zinazofungwa kila uchwao alafu wao wanasema hakuna waoaji ama waolewaji !!!??? .Yaani wanaangalia ndoa zenye zilizoharibika badala ya ndoa zilizosimama na kumpa Mungu utukufu. Swali la kujiuliza ni kwamba, ukiangalia mabinti,vijana/wanawake ama wanaume unaona nini? Unaona mtu anayefaa kuwa mume ama mke? Au unaona watu kama miti tu?. Wakati wengine wakiona fursa ya wake wema na waume wenye akili katikati ya mazingira yaleyale ...

*MZAZI NI MTU WA AJABU SANA!!!*

Image
* ➖ Mzazi siku zote hufurahia mafanikio ya mwanae kuliko mtu yeyote yule* * ➖ Mzazi ni ngumu sana kumlilia shida mwanae kwa sababu anahisi kuwa anaweza kumsumbua au kumuharibia mipango yake.* * ➖ Mzazi ni mtu pekee anayeweza kufurahi kulala njaa ili hali mwanaye ameshiba* * ➖ Ukiona mzazi anataka msaada toka kwa mwanae ujue anayo shida haswa na siku zote hujitahidi kupunguza ukubwa wa shida yake kwa mwanae ili asimpe usumbufu* * ➖ Mzazi akikwambia Γ nashida ya elfu 5000 jua shida halisi ni 20000 au zaidi ila atafurahi kwa kuipata hiyo elfu tano* * ➖ Mzazi akikwambia anaumwa kidogo, jua kuwa kweli anaumwa, huwa hawahitaji kabisa kuona mwanae akisumbuka kwaajiri yake.* * ➖ Mzazi akikwambia mkono unauma, inaweza kuwa amevunjika kabisa ndio maana kakwambia, akisema amevunjika jua hali ni mbaya sana* * ➖ Mzazi amebeba baraka za moja kwa moja kutoka kwa Mungu* * ➖ Mzazi akifurahi moyoni mwake kwa mtoto wake, jua mtoto huyo lazima abarikiwe, na akihuzunishwa inakuwa kinyume chake y...