Simulizi : Binti Wa Raisi Sehemu Ya Tano (5)

Vichwa vya habari vya magazeti,viliendelea kugonga bongo za raia huku zikileta viulizo vya aina yake.
Gazeti la Mwanachi katika chanzo chake makini liliidaka habari hiyo na kuanika kichwa cha habari kilichosomeka 'Kikosi cha ukombozi cha binti wa Raisi chasambalatishwa'
Wakati gazeti la Mtanzania lilichapa kichwa chake cha habari ya tukio lile na kuteka hisia za watu wengi 'Hatimaye team ya uokoaji binti wa raisi yaishia mdomoni kwa mamba'.
Mmoja wa watu waliovuta hisia za vichwa vya habari vile ni Geza ambaye alikuwa kimya kwa muda huku asijue nini cha kufanya baada ya sakata lile kutokea wiki moja nyuma..
Akanuna
Akachomoa noti ya shilingi elfu moja na kununua gazeti la Mtanzania kisha akatafuta sehemu iliyo tulivu aisome vizuri ili aelewe kitu gani zaidi kilichowapata wale askari mpaka wakakutwa na maswaibu yake ilhali wakiwa wazoefu wa oparesheni nyingi zilizozaa matunda kwa taifa.
Iweje hii ikawa ngumu namna ile?
Akapata seheme tulivu chini ya mti mmoja ulio na gogo la wastani shinani kwake.Akaketi na kufunua moja kwa moja katika habari husika.
Hakuna na muda wa kupoteza.
Baada ya dakika chache tu,akajikuta anakunya lile gazeti na kikinja uso kwa ghadhabu.Macho yamemuiva pima kama nyanya maji.
Anatafakari jambo fulani na ndipo alipoinuka na kuweka gazeti lake mfukoni,akaondoka zake kuelekea sehemu aijuayo.
……
Zaidi ya mara tano sasa Geza ulole anajaribu kupiga simu ya Swedy bila mafanikio ya kuipata,jambo ambalo lilimfanya apande na hasira sana.
Kwanini huyu jamaa asipatikane?
Akahamanika na kuhisi kuna jambo limemtokea la ghafla.Ndipo alipochukua uamuzi wa kuharibu pesa kwa kufanya nauli mpaka Moroko,mtaa ambayo alielezwa tangu awali kuwa amehamia huko.Kama kawaida yake,aliweza kuimaki maelekezo ya ramani aliyoambia na hatimaye kufika mahali hapo lakini ajabu mlango ulikuwa umefungwa.
Wasiwasi ukamzidi..
Alipotazama huku na kule hakuona kitu zaidi ya wapita njia pekee.Akiwa katika hali ya viulizo,sauti ya vishindo ikasikika masikioni mwake toka nyuma yake.Ndipo alipogeuka na kukutana na binti wa makamo ambaye alimzidi kwa kiasi kikubwa kwa umri.Binti yule alishuka toka kwenye taksi na kuanza kukimbilia ndani ya nyumba ile ambayo Geza anatazamana nayo toka mlangoni.Yule binti akampiga kwa kasi sana Geza na kufungua nyumba ile na kuingia ndani huku akimuacha Geza akiwa mdomo wazi.
Hajaelewa kabisa pale.
Huyu nani?,anaingia ndani kufanya nini? Au nimekosea nyumba?
Hapana hii si ndio nyumba ya kumi na sita toka konani kule kwenye barabara kuu?
Geza akajipa zoezi la maswali yasiyokuwa na ufumbuzi kabisa,ilitakiwa maswali yale akutanane na yule mlengwa mwenyewe.Ndipo aliposigea karibu na ule mlango huku akiwa na shahuku la kumuona tena yule binti ili ampige maswali yaliyoonekana yanamtatiza.
Ni nani huyu?
Anahusikaje?
Na mengine kemkem.Akiwa katika hamaniko lile,yule binti akafungua mlango na kutaka kutoka ndani mle lakinj ghafla akapigwa na moyo Paaah!.
Sura ya kuogopesha imemsimamia mbele yake hata hivyo Geza alitambua nini kilichompa hofu binti yule na kughairi kufunga ule mlango.


Wakatazama.
Na Geza akavunja ukimya kwa kuanza kumtwanga swali la kwanza akitanguliza salamu.
"Habari,wewe ni mwenyeji wa hii nyumba...na dogo Swedy yupo au unahusikaje humu?" Akayafumua maswali yote kwa mkupuo huku akimuacha yule binti ambaye ni Rayana akiwa ameduwaa,hakuelewa aanze kumjibu swali gani Hatimaye akamjibu na kumtaarifu jinsi Swedy alivyokamata na watu wasiojulikana jana usiku akiwa anarudi nyumbani kwake pale.
Ghafla Geza akakunja uso na kughadhibika mno.Wakaongozana na kuingia mle garini huku wasitambie kipi wanaenda kukifanya kwa muda huo.
"Tupeleke Mbezi Beach" Rayana akang'aka kwa sauti yenye wasiwasi mwingi.Ndipo dereva akaondoa gari kwa kasi sana na kutokomea.
--
Yalikuwa majira ya saa tatu za usiku,swedy akiwa amechelewa kurudi kwenye makazi yake mapya huko Moroko kutokana na kutawaliwa na kazi nyingi zilizoambatana na foleni kubwa iliyomkalisha barabara kwa muda wa saa zima.Wakati huo hakujua kuwa alikuwa anafuatiliwa kwa uzuri kutoka kule ofisini kwake.Aidana na Gomesa wakiwa na jamaa yao mmoja walipakiana kwenye gari lengo lilikuwa ni kumfundisha adabu Swedy kufuatia kile kitendo cha kumpiga Aidan ufukweni na isitoshe kulipa kisasi kwa kumchukua msichana wake Rayana ambaye alimsaliti hapo awali
Duh!
Baada ya gari kuruhusiwa ndipo swedy akakanyaga moto na kuondoa gari yake.Mpaka anafika maeneo karibu ya nyumba yake,kabla hajaifikia kabisa eneo lililo na uwazi wa kutosha likiwa halina mwanga wowote zaidi ya kiza ,ndipo gari lile la wakina Aidan likampita Swedy kwa kasi na kusimama kwa breki kali huku yule jamaa aliyeketi nyuma akiwa amevaa nguo nyeusi alipoepa kutoka garini na kulikimbilia gari la Swedy kiumakini.Wakati huo gari ya Swedy ilikuwa imefunga breki kali tena ya nguvu na kusimama huku akimakinika kuitazama ile gari ya mbele iliyomkata kwa kasi ya ajabu na kumzibia njia.
"Shiitt" Swedy alibwata kwa tahamaki huku akimtazama yule jamaa aliyekuwa anakuja kwa kasi.
Kengere ya hatari ikalia ubongoni kwake na hakuwa na jinsi zaidi ya kukaa kwa tahadhari kuikabili ile hali.Kweli yule jamaa alikuja moja kwa moja mlangoni kwa Swedy ila kabla hajakivuta kile kitasa akaachia ukelele mkali wa maumivu huku akijishika pajini katika uso wake.
Laaah!.
Jamaa alipigizwa usoni kwa ule mlango uliosukumwa kwa kasi na Swedy na ndipo ufito wa mlango ulipompata vizuri kichwani.Hapohapo jamaa akaghadhibika na kuswaga mbele kwa kasi ila akakutana na ngumi ya tumbo kwa mara ya pili akatoa sauti hafifu ya maumivu.
Gomesa aliposikia kelele ya jamaa yake kule garini akashuka kwa kasi huku akiwa ameshika kisu na kukimbilia mahali husika kwa kasi ya aina yake ila aliingia kichwa kichwa sana.Akajikuta alipigizwa na teke la mkono na kisu kile kikamporonyoka mikononi mwake.
Akabweka kwa ghadhamu kama dume la nyani huku akimuendea kwa kasi na nguvu zote.Swedy akiwa anapambana na yule jamaa akahisi kitu kizito kinamsomba kwa kasi na kumbabatiza ubavuni mwa gari.Yowe likamtoka.Gomesa alimbana kisawasawa pale garini hata pale alipojaribu kifurukuta akashindwa kabisa.
Jamaa lina nguvu za ajabu sana.
Hakuwa na ujanja tena zaidi ya kukubali matokeo.Wakamsukumizia garini mwao na kuchomoka kwa kasi.
Mateke,ngumi,makofi na vichwa vikachukua nafasi yake kutekeleza vipigo mwilini kwa Swedy huku wale jamaa wakiwa wameghadhibika sana.
Aidan wakati wote huo anatabasamu kwa kejeli huku akimtazama Swedy aliyefungwa mikono kwa nyuma.Damu zinamvuja usoni kwa kasi kama maji.
Duh!
Ndipo wale jamaa walivyositisha vichapo na kumkalia mbele yake wakiwa wenye hasira mno.
"Aah nadhani unanikumbuka sasa...." Aidan akauliza huku akiachia tabasamu la dharau kisha akaendele "... we ni bondia hatari sana,hivi umejifunza wapi? maana nahisi kama upo label kwa MayWeather hivi!" Aidan akatania kwa kejeli huku akilichanua lile tabasamu lake.
"Mnataka nini nyie mabwe..." Wala hajamalizia lile neno lake,akatoa ukelele wa maumivu huku akijinyonganyonga pale mbele kama mcheza 'Sindimba'
"Ebanaaa eeeh kumbe na wewe ni dancer wa haya magomba ya Sindimba?,sikujua aisee" Gomesa akadakia ilhali Swedy akijikaza maumivu yaliyokuwa yanamtoka begani kwake kufuatia na pigo la yule jamaa aliyembabatiza mlangoni garini kwake.
Akhaa!
Swedy akawatazama tena kwa hasira huku akimakinika pembeni yake ambapo kulikuwa na kisu ambacho awali alikiona kule hekahekani ya kutekwa.Akaghadhibika mno pale alipojaribu kuutoa mkono wake mmoja ili achukue kile kisu.
Shiiit!
Akajikalipia kwa hasira baada ya kubaini amefungwa mikono yote kwa nguvu.
"Aah labda nikuulize swali moja tu ndugu yangu...Umeanzaje kuwa na Rayana?" Aidan akauliza ila Swedy akapiga kimya.
"We fala si unaulizwa?" Gomesa akadakia lakini bado Swedy aliwatazama kwa mshangao.
Aidan akachomoa simu yake na kuitafuta namba ya Rayana kisha akaipiga mara moja,simu ikaita na kupokelewa na sauti nyororo ambayo haikuwa ngeni kabisa ukasikika.
Ikamchoma moyo wake.
Simu hiyo ikamueleza Rayana jinsi gani walivyomteka Swedy na sasa wanae(akaeleza wapi walipo).
"Njoo umchukue mala...." Aidan alipotangaza tusi hilo akajikuta anaachia tusi la nguoni huku akifumba jicho lake moja.Mate yenye mnato ya Swedy yakatua jichoni kwake kwa kasi sana.Hakika Swedy alikereka na lile tusi vibaya sana.Hata pale alipotema yale mate kwa mara nyingine akahisi macho yanamuia mazito sana,yanamlazimisha afumbe ilhali hataki kitendo hiko kitokee,muda huo huo akawa anahisi maumivu makali kutoka kisogoni kwake na sasa shingo ikalegea huku kichwa chake kikimuia kizito sana.Hatimaye akajipigiza pale mezani kama zigo na kupoteza fahamu.
Akha!

______

Hali ya hewa ilichafuka kwa kiasi chake usiku ule huku milio ya risasi ikisikika kila kona ya maeneo yale ya Mbezi Beach nyumbani kwa Bosco.
Wameingiliwa!!
Jamaa mmoja aliyekuwa ameishika bastola moja akimimina risasi kama njugu huku akimakinika sana kule anakojibizana na wale mahasimu wake,wakati pembeni yake kuna msichana akiwa amemshika jamaa jwa nguvu akionekana hajiwezi kabisa.Walitaharuki pale kwenye kichapa kidogo cha maua huku wale wanaojibizana nao wakiwa wamejibanza ubavuni mwa gari zao wakitupa njugu bila kujua yupo wapi adui yao.
Yule jamaa wa kwenye kichaka cha ua alifanikiwa kuwaangusha wawili upande ule walipo huku kwa mahesabu yake ya haraka yalisoma uwepo wa watu kama watatu hivi,lakini akajiuma midomo yake na kutukana kwa hasira mara alipobaini kuwa risasi zake zinaelekea kuisha ilhali wale jamaa bado wakijibu mapigo na milio ya bunduki zao hazikusikika kama bastola yake,zile zilikuwa zenyewe haswaa "Mashine Gun".http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akasonya kwa ghadhabu.Kilichokuwa kinamsaidia sana huyu jamaa ni ule mwanga unaowaonesha wale mahasimu wake ila katika hali ya kutotegemea taa zikazima ghafla.
Akasonya tena kisha akaacha kurusha risasi na kuwatazama wenzake.
"Tukimbie basi" yule msichana akazungumza kwa sauti hafifu iliyo na woga.
"Utakimbiaje hapa kwa mfano?,huoni uchochoro uko mbali nasi?" Jamaa wa kichaka akazungumza.
"Ka..ka Ge..za pa..mbana nao ni wale ulio..kuwa una..wasaka kwa muda m..refu" hatimaye yule aliyeshikwa na msichana akazungumza kwa tabu sana.
Geza akamakini kule kunako mahasimu wake,ndipo alipomuona jamaa mmoja akiwa kwa kasi sana upande walipo.Hapo hapo akatuma risasi ikamsalimie yule jamaa lakini haijafikia lengo kwani yule jamaa alibetuka na kujirusha hewani kama aliyepiga mbize hivi,ile anatua tu chini,akatua moja kwa moja na kuanza kutoa ukelele wa maumivu.Geza hakufanya ajizi alimdungua risasi ya pajani.Jamaa akabweta kwa maumivu.
Geza akatuma nyingine ila sasa akatukana kwa sauti hafifu.
"Risasi zimeisha!" Geza akahamanika.Alipotazama kule mbele kutoka pale kichakani akaona jamaa mmoja anajongea nae akiwa na bunduki kubwa.
Tumekwisha.
Wakabigwa na bumbuwazi,walipotazama ule mchochoro waliopaswa watokomee nao ulikuwa mbali sana na lazima wangelipigwa na risasi za wale wajamaa.
Khaaa!
Wakati wanamakini na yule bwana anayekuja kwa kasi pale walipo,Geza akafyatuka na kumrukia yule jamaa kwa teke zito lililomkubwa mpaka chini.Akainuka kwa kasi na kumshindilia teke la kifuani.Jamaa akatoa ukelele wa maumivu ilhali akitupa bunduki yake pembeni.Yule jamaa mwenye jeraha pajani akajivuta na kufanikiwa kuitia mikononi bastola yake kisha akageuka na kumtazama Geza kule aliko,akamkuta ndio anamshindilia teke la kifuani swaiba wake.Risasi mbili zikafoka na kutoka pale tunduni lakini kitu asichokitegemea yule jamaa,akamuona Geza akaruka kwa kasi ya ajabu kama mpiganaji wa mieleka.
Ebwana eeeh!
Zile risasi zikasalimia hewa huku zikiambua patupu,jamaa akataka kutuma zingine ila bahati haikuwa yake kabisa kwani Geza aliruka mithili ya mchezo wa "LONG JUMP" na kumfikia kifuani yule jamaa.
Akapiga kelele tena.Geza hakujari ndipo alipoinua ile bunduki na kumpiga pajani pale kwenye jeraha kwa kutumia kitako cha bunduki ile.
Jamaa akalia kama mbwa koko.
Kwa uharaka wa aina yake Geza akajibwaga chini na kumgeuza yule jamaa huku akimtupia ngumi zito la kisogoni.
Akafoka kama joka jangwa na kupoteza fahamu.Yule jamaa mwingine alipoona mwenzake katulia pale chini akataka kuchomoka kurudi alikotoka ila Geza alikwishashtuka ule mchezo,akabinjuka serakasi moja na kumkodeka miguu yake.
Akajibwaga chini kama pipa la plastiki kisha akamfanya kama alivyomfanya yule mwenzake naye akazimia pale pale.
Akabaki mmoja.
Yuko wapi?
Geza Ulole akawa anaburuza tumbo lake kuelekea kule kwenye gari ambako wale jamaa walipata kujificha na kutoa mashambulizi.Akafanikiwa kuifikia gari moja na kuingia uvunguni kwa mtindo ule ule wa kuburuza tumbo chini.
Umeme ukarudi.Kutoka pale alipojibanza Geza akaweza kuona jamaa wawili toka getini wakija kwa kasi sana pale yalipo magari huku wameshika bunduki zao.Hakukawia kuwaona kabla wale jamaa wawili wa kwanza kuifikia mlango,akamakinika na watu wengine walijivisha vitambaa usoni ilhali mikono yao ikiwa imefungwa kwa nyuma.
Eeh!
Walikuwa wanne waliovalia namna hiyo kabla hajaonekana jamaa mmoja wa mwisho mwenye bunduki yenye uwezo kama ile aliyoishika pale uvunguni mwa gari ambayo aliichukua mikononi mwa mmoja wa wale jamaa aliokuwa akipambana nao.
Yule wa nyuma alivalia kofia aina ya "Kepu" nyeusi.Akamsukuma yule wa mwisho mweka mkono nyuma aharakishe kutoka nje.
Geza akaachana na yule bwana mwenye Kepu.Akarudisha macho yake kwa wale jamaa wa kwanza waliotangulia,akawaona wakifungua mlango huku bunduki zao wakizielekezea mbele kwa umakini sana.
Walijua kuna adui pale nje...
Mmoja wa wale jamaa vitangulizi akaitupa risasi moja kule sehemu waliopo yule msichana aliyekuwa ameketi na mwanaume aliyezungumza kwa shida,walikuwa Swedy na Rayana.
Risasi ile ilipotumwa tu ukelele ukatokea,ukelele wa maumivu tena ule wa kiume.
Duuh!
Kimya kikatanda baada ya ukelele ule kutokea ndani ya sekunde tano tu.
Geza akapatwa na wakati mgumu kule chini huku akipigwa na maswali yasiyo na majibu.

"Gezaaaaaaa" Swedy akabweka kwa ghadhabu huku akitazama huku na huko na hapo akasikia sauti ya Geza ikiwa mbali nao ikiitikia .
"Uloleee,IGA UFEEEEE" Geza akajibu.
Aka!
Geza nini anakifanya?
"Mijitu mingine ya ajabu basi tu." Swedy akafoka kwa ghadhabu. Haikuchukua muda mrefu Geza akarudi akiwa na koleo kubwa litumikalo kuvunjia kufuri au waya mgumu.Akaelekea moja kwa moja mlango wa nyuma wa gari ile na kulipachika koleo lile lilalualo vitu vigumu.
Akafanikiwa.
Hapo ndipo wale mateka walipopata mwanga hafifu tofauti na ule wa mwanzo ijapokuwa walikuwa ndani ndani ya mizula myeusi waliofunikwa usoni.
Akaanza kuwachomoa mmoja mmoja mpaka wakatimia wanne.Akipowafunua mizula ile akahamanika kupita kiasi.
Dayana na Mercela hawapo..
Geza akatukana tusi la nguoni kwa ghadhabu lakini akajifariji kuwakomboa watu wale.
Askari ambao walitakiwa warudi na mabinti wawili wa maraisi ambapo wakajikuta wakiambulia maumivu yasio kifani,lakini leo wanajikuwa wako huru chini ya usimamizi wa Geza Ulole,mtu asiyependa maovu katika dunia hii.
"Asante sana Mr.Umetusave vilivyo,Sorry sijui unaitwa nani?,mimi ni afande Gakka" askari mmoja akazungumza huku akiyavua yale majoho waliyopatwa kuveshwa na wale watekaji.Geza akatabasamu tu bila kujibu,akatoka na kuwafuata wakina Swedy ambao muda wote walipigwa butwaa pale waliposimama.
"Aaah! Kumbe nimewadaka watu sio,wanajitamba na vyeo vyao hapo.Tuondokeni hapa sasa hivi" Geza akazungumza na kuanza kupiga hatua ndogondogo kuelekea gizani huku wakiwaacha wale askari pale garini.
______
Baada ya Geza na Rayana kupakia kwenye ile taksi kule moroko,wakafikishwa moja kwa moja Mbezi Beach wakiwa na nia moja tu,kumtoa Swedy kwa wanaharamu waliomteka.Geza alikuwa na hamu kubwa ya kumpa taarifa Swedy juu ya habari aliyoisoma kwenye gazeti lakini pia Rayana alihitaji kumpata Swedy kwa sababu ya mapenzi yake kwake.
Kabla hawajafanya kitu chochote kile wakatafuta sehemu ya tulivu na kuketi huku wakipanga mipango jinsi gani wanaweza kumtia mikononi Swedy wao.
"Sasa kule ndani ulifuata nini?" Geza akauliza.
"Kulikuwa na bastola yake,nikaichukua ili nije kupambana nao vizuri"
Geza akacheka kicheko cha ajabu.
"Unajua inatumikaje hiyo?" Akatokwa na swali ila Rayana hakulijibu.Walikaa sehemu ile kwa muda wa masaa kama mawaili hivi kutoka saa kumi na mbili mpaka saa mbili ndipo walipotoka na kuelekea sehemu husika,sehemu ambayo walielezwa kuwa ndipo alipo Swedy,kwa hiyo Rayana alitakiwa ajisalimishe mbele ya wakina Aidan kabla hawajamfanya kitu chochote Swedy.
Giza limekwishatanda na sasa mianga ya taa mbalimbali za majumbani kwa watu ikachukua nafasi yake.Geza akiwa na Rayana wakashuka kwenye kijimteremko kidogo na kupandisha tena huku wakiziendea ngumba kadhaa zilizoko kwenye kimlima hiko.Njiani hakukuwa na mwanga mzuri ambayo labda wangefanikiwa kutazama vizuri na kuona mbele zaidi lakini haikuwa hivyo.Bastola aliyokuwa nayo Rayana sasa ameikamatia Geza.Wakachanganya miguu mpaka walipoifikia nyumba moja kubwa yenye geti jeusi,ilikuwa imezingukwa na taa.
Hawakuitilia maanani..
Wakaingia kwenye mchochoro huo ambapo Geza akasita kidogo na kutazama kichaka kidogo chenye maua ya kuvutia,kilitawaliwa na giza kali kutokana na uwingi wa miti pale kichakani.
Wakaipita nayo na kumaliza ule mchochoro,wakakata kona na kuingia ndani zaidi lakini wakasimana ghafla baada ya kusikia watu wakizungumza,sauti zilipenya dilishani na kumfanya Geza ainue Shingo yake,akatazama.
Ndipo alipowaona.
"Nisubiri hapohapo" Geza akanong'ona ila Rayana akaanza kulalamika huku akiogopa kubaki peke yake pale nje ilhali pako kimya na hakuna mwanga wa aina yoyote zaidi ya ule utokao dilishani pale ambapo Geza alichungulia.Baada ya kubishana kama sekunde kumi hivi Rayana akaafiki lakini kwa shingo upande mno.
Geza Ulole akaingia ndani mle kupitia ule mlango wao ambao ulikuwa kuukuu sana kiasi kwamba Geza alitumia sekunde mbili tu kuuvunja na kuingia nao ndani.
Ni kitendo cha ghafla sana kilichofanywa na Geza,Aidan na wenzake wakapiga yowe kali ila Geza alishamfikia jamaa yule mmoja na kumpa ngumi mzito,jamaa akaanguka chini na kuzimia.
Duh!
Ngumi kali ya taya ikamzimisha yule jamaa,sasa walibaki Aidan pamoja na Gomesa.Geza akatupa ngumi nyingine na kupiga hewa kwani Gomesa aliikwepa vizuri sana.
"Heeee!" Geza akabweka kwa ukali.Akarusha
teke,hili likampata Aidan shingoni naye akayumba kabla hajatua chini na kutweta kwa nguvu.
Sasa Gomesa alibaki peke yake.Hakuishia hapo baada ya kumuweka chini Aidan,akaruka juu ya meza na kurusha teke la nguvu ila Gomesa naye akaiona na kuipisha,teke likagombana na upepo.
"Pumbavuu zako" Geza akatokwa na tusi la ghadhabu.Akashuka chini ya meza na kuruka kwenye pembe ya chumba kile.Akasimama kimya ilhali mikono yake ameifunga mfano wa waumini wa kiislamu wafanyavyo katika Swala.Akamtazama kwa sekunde kadhaa Gomesa ambaye alikuwa katika steili ya aina yake kama wale wacheza "JUDO".
"Huna uwezo wa kupigana na mimi bwana mdogo,njoo basi (akamtukania mama yake) wewee" Gomesa akajitapa kwa dharau.
Muda huo huo Aidan aliinuka na kuyumba kidogo kabla hajaanguka tena.
Teke la mtu mzima Geza linamtoa nishai.
"Unadhani mimi ni kama wa kabila lako?" Geza akazungumza ilhali akiwa vilevile na ile mikono yake.
"We kabila gani?" Gomesa akauliza.
"Hapa hatukuja kuulizana ukabila bwege wee" Geza akafoka na Kumfanya Gomesa acheke na kutoka katika steili yake ile ya Judo.
Kosa kubwa hilo..
Geza akajirusha kwa nguvu na kumtupia teke la nguvu ambalo lilimfukisha Gomeza ukutani kwa kasi,alipotaka kuinuka akakutana na ngumi kali ya pua na kuigandisha pale pale puani kisha akasema "Mimi ni msukuma halisi kabisa mdogo wangu" aliposema hivyo akamtwanga ngumi ya pili ya pua na damu zikamruka mithili ya maji.
Aidan akanywea zaidi hasa pale alipomuona Gomesa amechuruzikwa na damu puani.Wakati anamakinika kwa Gomesa akashtusha na teke kali la kifuani na hapo akachia mguno wa maumivu.
Akaninama na kumbeba Swedy begani na kutoweka nae mbele ya macho ya akina Aidan.
Nje akamkuta Rayana akiwa amejikunyata kwa woga sana.Giza lilizidi sasa.
Wakaanza kutembea kwa kasi huku Geza akiwa na Swedy begani.Baada ya kumaliza kile kichochoro cha kwanza na kuingia kwenye ile nyumba yenye taa kwa wingi,wakaziona gari.
Moja ilikuwa kama zile za kubebea wafungwa au waarifu,ya pili ilikuwa gari ndogo tu mfano wa Toyota Mark II.Hawakuyatilia maanani kabisa.Wakaongeza mwendo.
"Hey!" Sauti kutoka upande ule wenye gari mbili ikasikika.Wakahamanika ilhali Geza akiwa na Swedy begani na bastola mkononi.
Jamaa mmoja akatokea akiwa na bunduki yake,alivalia fulana iliyombana vizuri,ilikuwa nyeusi,mikono yake alijivesha glovu nyeusi.Akatembea kwa kasi kuja pale walipo wakina Geza ilhali bunduki yake ikiwa mbele kwa tahadhari.
Akawakirubia sasa.
"Nyie wakina nani?, halafu nyoosheni mikono juu haraka sana" jamaa yule akazungumza kwa sauti ya chini na bunduki yake ikiwalenga wale watu wake.Geza akachezwa na akili ya haraka na hapo ndipo alipobaini jamaa yule alikuwa na pua kubwa iliyojibandika usoni kwake.
Nikimpa ngumi ya pua huyu hatazimia?
Geza akajihoji kimoyomoyo huku akiendelea kumchunguza yule mtu.Rayana akawa anatetemeka pale aliposimama huku taratibu akimuacha Swedy agote chini kwa ulegevu.
Katika kumchunguza kwa muda mfupi Geza akabaini jamaa kuwa,yule mtu alikuwa na kidude kilichoivimbisha shingo mbele ya koromeo lake.Geza akafurahi rohoni na kujisemea,endepo atamkung'uta ngumi moja ya koo sidhani kama atapona 'akipona akapike sadaka kuwarehemu babu zake'.
Geza akamtazama tena kwa hasira yule jamaa na kengere ya hatari ikalia kichwani mwake.
"Mikono juu aisee hamni......" Hapo hapo hajamalizia maneno yake badala yake akajijuta anaitupa bunduki yake chini na kujishika shingoni kwa mikono miwili ilhali magoti yakiuisha nguvu kwa kasi,macho yalimtoka pima na ulimi wake ukiwa nje mithili ya mbwa akimbizwaye na adui wake.
Duh!
Jamaa yule akawa anabishana na israel mtoa roho.Akapiga magoti huku akikoroma mkoromo hafifu mara kabla hajaanguka chini na kugalagala.
Hapo ndipo wakina Geza walipomchukua tena Swedy na kuendelea na safari yao ila hawajachukua hata hatua kumi wakasikia tena sauti za watu kutoka pale pale kwenye gari.Bila kusita wakatumia nafasi ile kukimbilia pale kichakani,kichaka cha maua kwani ndio ilikuwa sehemu pekee ya kujikinga kwa wakati ule.
Wakakoswa risasi kadhaa na hapo wakaanza kujibizana mpaka walipofanikiwa kuwatia nguvuni wale jamaa walioongozwa na Bosco,Mzee wa Kepu, na kuwatorosha mateka.Wakaja kustaajabu baada ya kuwakuta mateka tofauti na wale waliowategemea kuwakuta ambao ni Dayana Mercela.


Katika nyumba ya kifahari ambayo ipo mahali penye ukimya sana nje ya Jiji la Dar es Salaam maeneo ya Kibamba.Gari mbili zilionekana zikiwa katika mwendo kasi sana kuliendea jumba hilo.Zikafunguka breki na vumbi jingi likatanda kwa muda kidogo kabla geti la nyumba hilo kufunguliwa na gari zote zikaingia ndani.
Kabla gari ya kwanza haijasimama sawa katika maegesho maalumu ya "Packing" mle ndani,Mzee mwenye suti kali iliyoendana sana na kofia ya "Pama" yenye ufito mweupe.Kutoka sehemu ta Packing,mzee huyu akatumia sekunde tano tu na kuvuta mlango kwa uharaka ilhali jamaa zake wakimchapukia nyuma yake kwa mwendo ule ule.
Wakafika sebleni lakini yule mzee hakuketi kwenye masofa ya thamani yaliyopo sebleni pale badala yake akawa anatamba sebule mzima huku akijikuna pasipowasha.
Lol!
Hakika mzee huyu amevurugwa kupiga kiasi sana.Baada ya kama dakika mbili akatokea mtu mwenye mwili mkubwa,hakuwa na aina yoyote ya nguo zaidi ya bukta kubwa tu,kifua kilikuwa wazi.Jamaa huyo alionekana akiwa na jasho jingi sana,kwa kumuangalia harakaharaka yawezekana alitoka mazoezini muda mfupi uliopita.
Wakatazamana kwa mshangao pale sebleni..


"Kuna kheri kweli mzee?" Jamaa yule mwenye mwili mpana akauliza na mzee akajibu kwa wasiwasi sana "MK mambo si shwari kwanza mabinti wako wapi?"
"Wapo room,nimewapiga sindano za usingizi wamelala wa pono Inspekta" MK akajibu.
Wakapiga hatua kuongozana kule walipo wale mateka wao huku Inspekta Makurumla akiwa na hasira za wazi kabisa.Hatua kadhaa kabla hawajakifikia chumba kile mlio wa simu ukasikika toka mfukoni mwa Inspekta Makurumla.Alipoitazama namba haikuwa ngeni kabisa na ilihifadhiwa kwa jina la Bonnie.
Akashtuka.
Namba ile ilikuwa ya mfuasi wa MK ambaye aliuawa na Geza siku iliyopita kule Mbezi beach wakati anajaribu kuiondoa gari ya mateka zao kabla hajachomolewa toka garini.
"This man still alive?" Inspekta Makurumla akashangaa na kutokwa na maneno yenye viulizo akiwa na maana ya kuwa yule mtu anayepiga bado alikuwa yupo hai?.
Lakini hawakujua kuwa anayepiga sio wanayemdhania tena.Alikuwa Geza ulole ambaye siku ile alipomkaba yule dereva anachuku bunduki pamoja na simu ya mkononi.
Inspekta Makurumla akaipokea na kuiweka sikioni na hapo ya Geza ikawa inaguruma sikioni kwa Inspekta huyu mwenye wadhifa mkubwa katika jeshi la polisi nchini Tanzania.
"Naitwa Geza,Geza Ulole,nakutafuta kwa muda mrefu sana Inspekta,tena nitakutia mikononi mwangu mimi mwenyewe bila kushirikiana na mtu yeyote na lazima unueleze kwanini unatumia wadhifa wako kuvunja sheria na taratibu za kazi yako.Nitakuwa mgeni wako usiku wa leo" Geza akakata simu na kumuacha Inspelta Makurumla katika hamaniko la aina yake.
Mtu ambaye hajapata kumsikia wala kumuona iweje anamchimbia mikwala namna ile kama mtoto mdogo?
EBBOO!
Inspekta hakuamini kabla na muda huo huo nguvu zikawa zinatoweka mwilini mwake na hatimaye akajikuta akiibwaga simu yake chini kabla ya kudakwa na mmoja wa jamaa wale waliomzunguka.
Mgeni wangu usiku wa leo!?
Inspekta anahamanika mno.
"Vipi mzee kimetokea nini?" MK akauliza kwa shauku akihitaji ufafanuzi zaidi.Inspekta hakuzungumza zaidi ya kuchukua simu na kwenda kwenye "Call Recorder" na kufungua maneno ya Geza.
Wote wakahamanika baada ya kusikiliza maneno hayo.
Wakaingia ndani na kuwakuta mabinti wa raisi wakiwa wamelala usingizi mzito sana katika moja ya kitanda cha pale chumbani.
Dayana akiwa hajitambui kabisa,Inspekta Makurumla akamshuka sehemu pajani upande wa mguu wa kulia na kutomasa kwa sekunde chache huku akitabasamu,tabasamu la uchu wa paja lile ila sio kwa uchu wa ngono hapana.
Akatoa mkono wake na kuelekeza kwa Mercela mtoto wa raisi wa Rwanda ambaye walikuwa safari moja kuelekea Bagamoyo katika hifadhi ya SADAN.Akaivuta ile shuka iliyozuia kiungo kile adhimu na kutomasa tena paja kama alivyomfanyia Dayana.
Akipojihakikishia amewatomasa vya kutosha akawageukia wakina MK na kuwatazama kwa dakika chache kisha akasema.
"MK na Bosco nawaomba tafadhari"
Inspekta makurumla akazungumza kwa utuli wa aina yake.Inspekta Makurumla,MK,Bosco pamoja na washiriki wenza wakaweka kikao kifupi kilichohusiana na mikakati ya kumaliza kazi iliyowaweka katika tete kwa muda mfupi namna ile.
Baada ya kumaliza kikao hicho wakakubaliana,wakatawanyika.Inspekta akarudi garini akiwa na watu wake aliofuatana nao hapo awali na kugeuza kabla hawajatokomea pale ngomeni.
______

Geza akiwa nyumbani kwake huku mezani kwake akiwa na kisu kidogo cha kufyatua bila kusahau ile bastola ya Swedy aliyowahi kuitumia katika msako wa masahibu wa Swedy na wale watekaji huko Mbezi. Kichwani alikuwa na pama jeusi ili mwili ukizuiwa na suti ya bei rahisi sana.
"Hahah kama waziri fulani vile" akajikuta akitabasamu huku mbele yake kioo kikubwa kilimchoresha dhahiri.Ni kawaida yake sana kwa mtu huyu kuzungumza na kujisifia peke yake akiwa ndani kwake.
Ni saa tatu ya usiku sasa,Geza anapanga azma yake ya kumtembelea Inspekta Makurumla huko Mbezi mara baada ya kubaini kuwa anajihusisha na mambi yasio ya kawaida katika nchi anayoipenda kwa dhati.
Tayari alikwishajiweka sawa na alichokifanya na kutoka nje na kufunga mlango wake,akakodi taksi ambayo ilimtoa kwao Mwananyamala siku ile na kuelekea Mbezi ya Kimara.
Haikumpa shida kwani Inspekta Makurumla alikuwa askari maarufu sana mjini Dar es salaam na ndio chanzo cha Geza kuweza kupafahamu hata nyumbani kwake anapoishi japokuwa Inspekta mwenyewe hafahamu kama kuna kiumbe kinaitwa Geza.
Baada ya kama lisaa hivi,gari ikapaki mita kadhaa kutoka pale jumbani kwa Inspekta.Akalipa pesa ya taksi na kuanza kujongea taratibu kwa mwendo wa upole sana.Akalifikia geti lile na kubisha hodi.
Likafunguliwa..
Mlinzi aliyevalia mavazi ya ugambo akatokeza kichwa chake na kukutana na mtu mwenye suti iliyoenda sanjari na kofia aina ya Pama kichwani kwake.
Akamtazama kwa sekunde chache kabla hajamtupia swali "Wewe ni nani?" akauliza na Geza akatabasamu kidogo kisha akatoa kitambulisho chake cha kupigia kula na kukilingisha kwa vidole viwili vya mkono wa kulia na kusema "...Mimi ni I.G.P Kibongori kutoka jeshi la polisi,namuhitaji Inspekta Makurumla haraka sana" Geza akakiweka kitambulisho chake baada ya kuhakikisha mlinzi yule hajakiona vizuri na kutokana na lile giza la pale getini ikamuia vizuri ule uongo wake kuaminika na yule mlinzi.
Khaa!
Bila kutarajia mlinzi yule akaanza kutetemeka huku woga ukimtawala vilivyo.Cheo hiki alichojitambulisha jamaa aliye mbele yake ni kikubwa sana katika jeshi la polisi.
Akanywea.
"Mkuu bosi kaniaga na mke wake wanaenda kulala hoterini.Hapa ha..wapo" mlinzi akazungumza kwa mbababiko wa aina yake.Geza akachekea rohoni huku sura yake ikiwa katika hasira za wazi kabisa.Zikamzidishia mlinzi woga wa kutosha.
"Hoteli gani?" Geza akatupa swali.
“Sifahamu mkuu"
Geza akapandwa na hasira sana huku akilijia kosa lake alilolifanya.Kitendo cha kumpa taarifa juu ya ujio wake pale nyumbani kwake kumemfukuzisha Inspekta huyo.
Akageuka na kuanza kupiga hatua chache kutoka getini pale huku mara kadhaa mlinzi yule akimchungulia I.G.P Kibongori muongo akipotea mbele ya mboni zake bila kuaga.Ile Geza akapotea mbele ya yule mlinzi,huku nyuma gari moja ikafunga breki kwa kasi na watu wapatao wanne wenye miili mipana wakashuka na kumuendea yule mlinzi muoga.
"Kuna mtu wowote alifika hapa?" Jamaa mmoja akauliza kwa ghadhabu ilhali pembeni yake kukiwa na jamaa wengine wenye miili ya kutisha.
"Nyi..e wakina na..ni?" mlinzi akauliza kwa woga kabisa ila akakunjiwa uso na jamaa yule kiasi kwamba akajikuta anajibu swali lake "....alikuja I.G.P Kibongori muda si mrefu" mlinzi akanena na watu wale wakatazamana kwa mshangao.Hawakuwa wanamfahamu kabisa mtu anayeitwa I.G.P Kibongori.
"I.G.P Kibongori ndio nani?" Akauliza
"Simjui hata mimi"
"Shiiit!"
Jamaa yule akaghadhaibika na muda huo huo akatoa simu yake kabla hajaitumia akauliza tena.
"Kaelekea wapi huyo I.G.P?"
"Njia hiyo" mlinzi akanyoosha kidole njia ambayo Geza katokomea nayo.
"Na gari aina gani?"
"Eeh! kwa miguu tu"
Wakatazamana tena na hapo yule jamaa akaanza kutembea kuelekea kule alikoelekea Geza.Ni katika mchochoro uliotenganisha nyumba ile ya Inspekta Makurumla na nyumba nyingine.Kichochoro kilikuwa na giza haswaa!.
Geza baada ya kutoka pale getini akajibanza katika uchochoro ule mara baada ya kusikia mngurumo wa gari nyuma yake kabla halijatia nanga pale getini na hapo akawa anawafuatilia jamaa wale walioshuka na garini.Akakichomoa kisu chake na kukishikilia kiukamilifu sana mara tu baada ya kusikia kishindo cha mtu kikielekea pale alipo.
"AYAAAA!"
Ukelele wa maumivu ukavuta kule uchochoroni.Geza alikwisha muweka kitanzini yule jamaa huku kisu chake kidogo amekikandamiza kooni kwa njemba lile.
"Tulia,umekutana na I.G.P kibongori hapa,utanieleza haraka sana wapi aliko binti wa Raisi.Nyie ndio wavurugaji amani hapa nchini" Geza akakoroma kwa ghadhabu huku akiongeza ukali wa roba ya kisu kile kidogo.
Jamaa akatoa mguni hafifu.Kisu cha Geza kikamchanja pale kooni na damu ikaanza kuchukuruzika.
"Nataka uniambie binti wa raisi yuko wapi?"
"Si...jui mi..mi" akazungumza kwa shida.Geza akaongeza roba.Sasa akawa anakoroma kama fisi.
Ghafla akatokea njemba mmoja konani na kwa kasi ya ajabu Geza akamtupa yule wa kwanza na kumrukia yule aliyetokezea kwa teke kali,naye akatua chini kama zigo huku ukilalamika.Geza akajitoa tena na safari hii alikunja ngumi mzito ambayo inaelekea shingoni kwa yule jamaa.
Akakwepa kiutamu na ngumi ya Geza ikatua mchangani.Akageuka kwa kasi sana,hata yule jamaa aliyepata kupigwa kabali na Geza akashangaa jinsi gani Geza alivyo mwepesi namna ile.Akasimama wima na kufungwa swala kama sio yeye huku wakiwakata jicho la ghadhabu wale majamaa.
"Wewe ndio I.G.P fala fala?" Jamaa aliyekwepa ngumi ya Geza akauliza na Geza akabaki akimtazama kabla ya kusema chochote.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nipo hapa kujua wapi walipo mabinti mliowateka?" Geza akauliza kwa upole kama sio mtu hatari kwao.
"Hahah mabinti! Sasa wewe ndio mzazi?,wewe ndio mama yao?" Jamaa akauliza maswali yenye dharau kejeli na vijembe kwa Geza.Laiti kama alingelijua Geza mtu wa aina gani asingelisumbuka kufunua kinywa yake na kuzungumza maneno kama yale.
"Nakuuliza wewe(akamtukania mama yake) I.G.P fa..." Kitendo cha haraka mno ambacho hakuweza kutaraji kufanywa kwa muda ule,kwani Geza alijirusha kwa kasi na kumkumba yule mropokaji.Safari hii Geza alichomoa bastola ya Swedy na kumuweka mdomoni.Macho yakamtoka kama panya mtegoni.Yule aliyechanjwa kisu na Geza pale chini akajizoazoa na kufanikiwa kukikamata kwa shida sana na sasa akamtazama Geza aliyekuwa bize ya mwenzake na wakati huo jamaa mwenye kisu alipewa mgongo na Geza.
Hatari hii.
Geza hajui kinachoendelea nyuma yake kwa muda huo.Kisu chake kinaelekea kumtoa nishai waziwazi.

.
"Tulia hivyo hivyo" Geza akazungumza kwa ukali huku tundu la bastola la kutema risasi likiwa mdomoni mwa yule jamaa. Kwa akaichomoa haraka bastola na kumsukumia nyuma akitumia mkono wake mmoja wa kushoto.
AAAH!.
Akapiga kelele ya maumivu ya aina yake. Baada ya Geza kumsukuma jamaa yule kwa kasi za ajabu akakutana na kisu cha kifuani kilichotumwa na
Mwenzake.Wote wakaanguka chini kama mizigo.Kutoka kule getini wale wenzao wakaja kwa kasi na bila kuuliza wakaanza kurusha ngumi zilizokwepwa na Geza na kuambulia visago takatifu sana.Mpaka dakika kama kumi hivi Geza alishawazimisha wale jamaa kwa ngumi mzito sana na kubaki mmoja ambaye alimkaba kabali la kisu hapo awali.Akachukua kisu chake na kumsogeza yule jamaa kisha akamkandamizia ukutani.
"Haya niambie haraka mabinti wa raisi wako wapi?" Geza akauliza kwa ghadhabu sana ila jamaa hakuzungumza kitu zaidi ya kukodoa macho ya uchungu tu huku mikono yake ikiwa pake jerahani kwake.
"Kama husemi nakuchinja leo,semaaa" Geza akaendelea kumkoromea jamaa lakini bado alishikilia msimamo wake ule ule wa kutosema.
Geza akaghadhibika, alichokifanya ni kufyatua kisu chake na kumchomo pajani.Mguno mkali wa maumivu ukamtoka huku.
Akamziba mdomo na kumtupia tena swali lile lile.Kutokana na maumivu kuwa makali sana,hakuwa na budi kusema ukweli.
"Wa..le mabi..nti wamelazwa ndani ya jumba moja hu..ko Kiba..mba Comrade na...omba uni..ache mkuu.."
Jamaa anazungumza kwa uchungu sana.Geza akamkata jicho la hasira na hapo akamuuliza tena akitaka kujua jumba hilo lipo upande gani na sehemu gani?
"..ukifika Ki..bamba uta...kuta njia ya vumbi ya..." Kabla jamaa hajamalizia kuongea Geza akamtwanga ngumi na kupotea eneo lile haraka sana.

_______

UFUKWE WA COCO BEACH JIJI DAR ES SALAAM.

Saa kumi na moja za alfajiri,gari aina ya Hyundai yenye rangi ya kijivu iliegeshwa katika ufukwe huo upendwao na watu wengi kubarizi sehemu hiyo.Alfajiri hiyo ilikuwa kabisa gari hiyo ilifunga breki mchangani na dereva aliyevalia fulani yenye kola ndefu zilizoishia juu ya shingo yako huku sura yake ikiwa imefunikwa na kitambaa cheusi,kichwa chake kilifunikwa kwa KEPU nyeusi kabisa.Mkononi alishika bastola iliyonata vizuri kwenye glovus zake.
Kutoka pale garini, gari nyingine aina ya VTZ ya kaki ikapaki pembeni na yule jamaa mwenye Kepu akajongea mpaka kwenye Vtz.
Wakakutana.
Wakawa wanateta jambo fulani ambalo halikudumu ndani ya dakika tano kabla ya jamaa mmoja mwenye kipara kuliendelea lile gari la Hyundai.Akafungua mlango wa nguma na kuingia ndani kabla hajatoka nje tena.Akaifunga milango na kunyoosha mkono wake juu na kidole gumba kikatoa ishara ya kuwa mambo yanaenda kama ilivyopangwa.Baada ya kutoa ishara ile,jamaa wa Kipara akatokomea majabarini mita kadhaa kutoka pale garini.
Yule jamaa wa Kepu na wenzake wakaingia garini,gari ya Vtz,na kuondoka zao.Gari ya Hyundai ikabaki peke yake pale pale ufukweni.
Kwanini?

Jua likaanza kuchomoza kwaa mbali sana huku kigiza kiliikaribisha siku nyingine kikaanza kutoweka.Ufukwe ule ulitawaliwa kwa kelele za mawimbi hafifu kabisa na maji yakiwa yamepungua mno kutoka upande wa juu wa ufunde ule kiasi kwamba kimo cha maji huweza kufikia magoti au kiunoni mwa mtu mwenye urefu wa futi kama tano na nchi kadhaa.Kutoka upande wa kulia wa ufukwe ule kuna wavuvi kama wawili waliojishugulisha na shuguli yao.Wakivua samaki kwa kutumia nyavu zao na kujizolea dagaa wadogowadogo waliosukumwa na mawimbi kutoka katika kina cha bahari.
Ndipo walipoona!
Wavuvi hao waliojishugulisha na uvutaji wa nyavu yao wakashtuka baada ya kuiona gari kwa mbali ikiwa imesimama.Wakajiuliza maswali mengi kwanini gari lile limekuja mapema sana ufukweni pale tofauti sana kama ilivyo kawaida ya watu kuja eneo lile?
Utata..
Kwa mara ya kwanza wakalipuuzia jambo lile lakini baada ya dakika chache tu ndipo gari za polisi ziliazo ving'ora zipatazo sita zikafunga breki kali na kwa kasi ya ajabu polisi wake wenye vikinga risasi "Bullet proof" pamoja na element za usalama kichwani bila kuacha sponji za magotini wakalizunguka gari lile la Hyundaoi huku mitutu yao ikiwa imetazamishwa mbele.
Akatokea polisi mmoja aliyevalia sare tofauti na wenzake na kuanza kulisogelea lile gari kwa umakini sana.
Katika masuala kama haya,jambo lolote linaweza kutokea,ni vema kujiami na kujivesha umakini mkubwa pamoja na asilimia ya kuamini kile kitu unachokikusudia ziwe chache sana.
Kama walivyo hawa polisi waliaza kulizunguka gari lile kwa kasi sana huku mmoja wao akiliendea kwa umakini wa hali ya juu.
Akalifikia na kwa kutumia mkono wa kulia wenye glovus na kuanza kuvuta taratibu mpaka ukafunguka.
Akawaona.
Wasichana wawili waliolala ndani ya gari lile wakiwa hawajitambui kabisa.Yule askari akafanya hima kuwaita wenzake ambake ambao walifika wakiwa na machela zao mbili.Wakawapakia wale mabinti.
Dayana na Mercela walipakuwa ndani ya machela na kuinguzwa kwenye gari ya wagonjwa ambayo ilianbatana na gari hizo za polisi. Ikageuza kwa kasi na kuondoka eneo lile likisindikizwa na gari za polisi mbili.
Askari waliiosalia wakalikagua gari lakini hawakukuta kitu chochote Hawakujua kama kulikuwa na mtu anawachora kutoka kwenye majabari pale ufukweni. Jamaa wa Kipara.
***
Gari ya wagonjwa iliyowabeba mabinti wa raisi ikachuku uelekeo wa hosptali ya Aghkan huku ikiwa katika mwendo wa kasi sana .Gari zote zilikaa pembeni kuipisha gari hiyo ichukue nafasi. Na kweli kama nusu saa baadae ukafunga breki katika hospitali hiyo na wauguzi waliopewa taarifa ujio wa gari hiyo wakafanya kazi yao mara moja.
Hazijapita dakika kumi msafara wa raisi ukiambatana na raisi wa Rwanda ukaingia hosptalini hapo.Wote walichanganyikiwa mno.
"What's wrong?" Rais Noel Mkwakwacha akauliza ilhali jasho likimvuja na hofu kubwa ikimtanda.
"Tulia moyo mheshimiwa mambo yataenda sawa tu" George Mbasho akamtoa wasiwasi kwa kumpa maneno ya kutia matumaini.
Haraka Madaktari wa hosptali hiyo maarufu jijini wakavalia ngwanda zao na kuanza hekaheka za kuwahudumia mabinti hao.Cha kwanza walichokifanya ni kuchukua vipimo kwa kila binti na kuingia maabara na baada ya dakika kumi wakarudi na majibu yaliyoeleza kuwa,mabinti hao walidungwa sindano zenye sumu ambayo zitakuwa zinawatafuna taratibu kwa siku kumi na nne. Aidha daktari huyo akaeleza jinsi ya gani wanaweza kuwaponya mabinti hao. Hakuwa na tiba kabisa kwani waliiwachoma sindano hizo ndio wenye dawa ya kuiondoa sumu hiyo mwilini na hapo walipozungumza sumu hiyo ilikwishaenea mwili mzima na sasa kilichobaki ni kuanza kuua viungo taratibu sana.
Duh!...
Kazi palepale.Kazi ya kuwasaka wale watekaji ikawawia tena upya huku ikiwalazimu kutumia njia yoyote ili waweze kuwanusuru mabinti zao.
"Doctor you can't to treat my daughter No! Usiniambie kabisa" Rais Noel Mkwakwacha akabwata kwa uchungu huku akiwa maana tosha ya kumtahadhalisha daktari asishindwe kumtibu mwanae.
"No! way Comrade President,hao jamaa wametumia sumu ya aina yake ambayo haiwezi kutoka mwili bila kuwa na dawa hiyo walioitengeneza kuiondoa sumu hiyo but..." Daktari akamtazama Noel Mkwakwacha na kuendelea "....nachofahami mimi hawa watu mheshimiwa wanapenda pesa tu hakuna kingine."akanyamaza na kumtazama raisi.
Hali tete!
Katika wodi waliofikia mabinti hao wakajikuta wakiamka na kujikuta wakiwa chumbani. Chumba kilichozungukwa na mitambo michache sana huku mbele yao ukutani kukiwa na kioo kikubwa kilichowaonesha mwili wao mzima kwa ndani.Walipotazama kwa umakini wakabaini hakuna mtu yeyote chumbani mle.Dayana alilazwa upande wa kulia na Mercela upande wa kushoto wote wakatazama kwa muda kabla hawajainuka na kuketi kitako vitandani mwao.
"Tupo wapi!?" Dayana akauliza huku akishangaashangaa mle ndani bila kugundua kitu chochote. Hakuna aliyefahamu kabisa. Alichunguza kwa umakini ndipo alipobaini kuwa ni hospitali. Ni baada ya kuyaona mashuka pamoja na harufu kali za madawa mle chumbani. Hakuweza kuednelea kuchunguza sana, ndipo alipohisi kichwa kizit. Akajilaza kwenye kitanda kile na kubaki akitumbua macho tu.
Dakika kama tano mbele, mlango wa chumba kile ukafunguliwa na madaktari wawili waliovalia sare zao huku wakiambatana na rais akiwa na mke wake pamoja na George Mbasho. Mke wa rais alikuwa na hofu kubwa na muda wote alikuwa analia kiasi kwamba macho yake yakabadilika rangi na kuwa mekundu. Akakimbilia pale alipo mwanae na kumkumbatia kwa nguvu huku akitokwa na kilio cha kwikwi. Muda huo huo akaingia tena rais wa Rwanda. Naye akiwa na mke wake pamoja na mtu mwingine wa karibu yake. Walihamanika kwa muda pale ndani kabla hawaondolewa na madaktari.
Hakukuwa na kufanya kuwaponya wale mabinti zaidi ya kupanga mikakati ya kuwanasa waliofanya kitendo kile mara moja. Wale mabinti, Dayana na Mercela wakachukuliwa kutoka pale hosptalini na kupelekwa ikulu. Wakti huo mipango ya kuwaponya ikiendelea kwa kasi.

_____
Siku iliyofuata, ilikuwa na habari mpya kabisa kwa Geza Ulole. Akiwa nyumbani kwake ameketi kwenye kiti cha plastiki. Pembeni yake akiwa Swedi. Waliumiza kichwa ni namna gani wanaweza kuwatia mikononi wale jamaa hatari walioongozwa na Inspekta Mkurumla. Na ndipo kichwa cha Geza kilichocheza na fikra kwa uharaka sana. Akaja na jibu kwa Swedi. Swedi akaketi vizuri na kuanza kumsikiliza Geza kile kitu alichofikria kwa muda ule.
Geza akakohoa kidogo na kumtazama Swedi.
“Unaweza kupigana kwanza?” Geza akamuuliza swali kabla hajaendelea kumfafanuliwa kile kitu kilichoanza.
Duuh!
“Sio sana. Kwanini unaniuliza swali kama hilo?” Swedi akajibu huku akitoa swali kwa Geza.
“Kama ulivyoisoma hiyo habari, ila achana na hayo…” Geza akajikalisha vizuri na kuendelea kusema. “…hakuna njia nyingine zaidi ya kupambana ili kupata kitu tukitakacho mdogo wangu. Na ili ujinga huu utokomee basi lazima tuwe imara kabisa katika hili. La sivyo tunaweza kuwa kwenye hatari kubwa. Ila sio kwa mimi. Hah! Labda wewe.” Geza akazungumza huku akitabasamu. Hakuwa ameeleweka kwa Swedi. Akabaki akimtumbulia macho tu.
“Sijakuelewa kaka”
“Utanielewa tu ndugu yangu”
Geza akaendelea kufafanua hoja yake. Alimwambia Swedi kuwa, ili kuipata ile dawa ambayo ingeliponya uhai a mabinti wale wawili, basi lazima wawe makini katika kuzipata dwa hizo kutoka kwenye mikono ya wale jamaa katili. Ilitakiwa iwe hivyo ili tu wajipatie donge nono. Tukio hilo liliwapasa walifanya kabla watu kutoka serikalini waanze kuingia kwenye msako wa wale wanaharamu na hatimaye kukosa nafasi ya wao kuipata ile dawa yenye umuhimu sana.
“… hivyo basi lazima tufanye hima kuliko upande ungine, na ndio maana nikakuuliza unaweza mkono? Wale jamaa hawana mzaha kabisa ati!” Geza akaweka kituo na kumtazama Swedi.
Macho yalimdondoka tu.
Ile ni hatari nyingine sasa.


Kuwaingia wale watu wenye uhatari ilikuwa ni shughuli nyingine sana kwa Swedi. Pale alipoketi akajikuta akiwaza mbali sana mpaka Geza anakuja kumchapa kibao na kushtuka.
“Dogo unawaza kitu gani haswa khaa” Akamkoromea. Swedi akakubali kwa shingo upande na hapo mikakati ikaanza kwa uharaka. Ndani ya siku ile wakafanikiwa kutambua kituo kinachofanyiwa kazi na Inspekta Makurumla.
Ni jumatano tulivu kabisa. Katika ofisini ya Inspekta Makurumla bado aliendelea kufanya kazi yake za kila siku. Ni baada ya nusu saa mbele baada ya uhitmu sa saba za mchana, ndipo alipopata mgeni. Mgeni alivaa nguo za heshimu huku akitoa tabasamu murua mno. Ilikuwa Swedi na kwa muda ule alionekana peke yake pale ndani. Akakaribishwa na mzee huyo naye akaketi.
“Ehee kijana habari yako?” Insp akasalimia kwa bashasha.
“Safi…” Swedi akaitikia na muda huohuo akazama mfuko wake wa suruali na kutoa simu. Akaingia kwenye upande wa video na kumuonesha ile simu Insp Makurumla.
Hakuamini alichokiona kwenye ile simu. Video fupi iliyoanza kumtoa jasho pasi na kujua kitu gani kinaendelea pale ofisini kwake. Tukio analoliona kwenye ile simu, linampeleka mbali sana kuhusu familia yake. Kwani Swedi alikuwa amemuoneshea ile video iliyomuonesha mke wa Insp akiwa amefungwa kitambaa mdomoni huku akihema kwa shida sana. Macho yalimtoka kwa woga. Kutoka pale kwa mke wake, kamera ikazunguzwa na kuwaoneshwa watoto wake wawili anaowapenda sana. Moyo ukamdunda. Akiwa bado haamini kile kitu cha mbele yake, mara akawekewa bastola kwenye paji la uso na Swedi.
“Nini sasa we bwana mdogo?...unavamia kituo cha polisi na kuleta huu ujinga wako eeh?” Insp akapayuka kwa jazba sana lakini hicho kitu hakikumpa wasiwasi Swedi.
“Taratibu mzee, ni mambo ya kuwekna sawa tu haya” Swedi akazungumza kwa upole kama jambo analolifanya ni la kawaida tu.
“Nini pumbavu we mtoto unatoke…” Akakwamishwa kwa pigo la kitako cha bastola.
“Kelele basi, unaona hii bastola ina kiwambo, kwahiyo nitakumwaga ubongo kimya kimya kama ukiwa msumbufu kiasi hiki” Swedi akakoroma na Insp akakaa kimya huku sura yake ikiwa imekunjika kwa hasira. Akamrishwa aketi kwenye kiti na yeye akafanya hivyo. Mada ikakaa mezani mara moja.
“Tutaiachia familia yako kama ukileta hiyo dawa ndani ya masaa 48” Swedi akanena.
“Familia yangu mmeipeleka wapi nyie kenge? Na hiyo dawa mnayosema mbona siwaelewi?” Akafoka kwa hasira.
“Utatoa ushirikiano au?” Swedi akauliza swali fupi na kupuuzia maneno ya Insp Makurumla.
“Nijibu kwanza swali langu”
“Sikuja kubishana hapa mzee wangu aah!” Swedi akamaka kwa hasira sana na hapo akajikuta anainuka na kuto asimu yake tena ilhali bastola yake ikiwa mbele ya Insp Makurumla. Akabonyeza kibenyezo kadhaa na kuiweka sikioni.
“Kaka hili lizee kibishi aisee, hebu ua kwanza mtoto wake mmoja” Swedi akazungumza na ndipo Insp Makurumla alipomaka kwa ghadhabu huku macho kayatoa.
“Aaah usi…fanye huo ujinga ki..jana wangu tuyamalize tu daah” Akatoa lai kwa pupa baada ya kusikia sauti ile mkwala ule wa kuuawa kwa mtoto wake.
“Kaa chini taratibu mjinga wewe” Swedi akafoka na Insp Makurumla akaketi chini kwa upole.
Alikuwa ameshikika kwa kweli.
Baada ya kitisho cha Swedi akijifanya kama anaongea na mtu wakati hakufanya hivyo, akakata simu yake na kumtazama mzee wa watu pale kwenye kiti akiwa anavunjwa na jasho japokuwa kulikuwa na feni juu lakini haikuonesha msaada kwake.
“Tumekupa masaa mangapi vilee?” Swedi akauliza kwa kebehi.
“Arobaini na nane dogo” Insp akajibu.
“Sasa ukijifanya kuleta ujanja nitaanza na yule mtoto wako yule, halafu nafuata mkeo, kisha wa mwisho wake sawa?”
Inspekta Makurumla hakujibu kitu zaidi ya kumtazama tu yule kijana anayemsemesha. Muda huo huo Swedi akafungua mlango na kuondoka zake mle ndani.
Hali ilikuwa tete kwa upande wa Makurumla, hakujua aanze wapi kufanya hiyo kazi. Akajikuta anatoka nje ya ile ofisi na kuingia garini kwake kisha akapotea eneo lile. Njiani aliongea na wafuasi wake kitu kilichomkuta muda mfupi uliopita. Akiwa anaongea kwa ubishani fulani baina yake na yule anayezungumza nae, kulimpa hofu kubwa sana kwake. Uamuzi aliouchukua ni kukata simu na kuiweka pembeni. Bado alikuwa kwenye gari, alikanyaga moto mpaka nyumbani kwa Mbezi. Hapo akakutana na mlinzi akiwa hana wasiwasi kabisa.
“Mke wangu yupo humu” Makurumla akauliza kwa sauti ya hofu na jibu alilopata kutoka kwa mlinzi wake lilimpa wakati mgumu kabisa.
“Aaah bosi mbona mama katoka na watoto tangia asubuhi. Ameaga kuwa wanaenda huko sijui wapi… Jang..wani sea…bureze” Mlinzi akajibu huku akilitafuta sehemu iitwayo Jangwani Seabreeze bila kuipatia vizuri kimatamshi.
“AAAH!” Makurumla akamaka. Akaanza kukimbilia ndani kwa pupa huku akimuacha mlinzi njia panda pale getini.
________
Mikakati ya Geza na Swedi ikaishia kwenye kilele na kugawana kazi iliyotakiwa ikamilike ndani ya wiki ileile. Walipanga waiteke familia ya Makurumla ambayo ndio furaha yake maishani mwake, na kutokea hapo wataweza kupata njia nyingine ya kujua wapi ilipo ile dawa na nani alishikilia. Ilitakiwa wajue wanaiteka vipi ile familia na ndipo walipokubaliana waende mpaka Mbezi kwa Insp huyo. Huko ndiko walipokutana na bahati. Walipofika tu nje la nyumba ile mita kadhaa kutoka pale getini, gari ndogo likatoka ikiwa ni majira ya saa nne za asubuhi. Kwa kuwa gari hiyo haikuwa na vioo vyeusi, waliweza kuona nini kilicho ndani ya ile gari. Mke wa Makurumla akiwa na watoto wake wawili walioketi nyuma, walichukua uelekeo wa upande wa kushoto mwa nyumba ile wakiwa kwenye mwendo mdogo. Swedi akageuza gari yake na kuanza kuwafuata kwa nyuma bila ya wao kujua.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni kama mwendo wa masaa kadhaa ndipo gari ile ya mke wa Makurumla iliposimama nje ya duka moja. Akashuka na kuingia dukani hapo kisha baada ya dakika kama tatu hivi akarudi akiwa na maji makubwa.
Eeeh!
Kitendo kile cha kuingia dukani na kurudi kwenye gari yake, akakutana na tukio la kushangaza sana. Mle ndani aliacha watoto wake wawili tu, aliporudi idadi yake ikaongezeka, sasa walikuwa watatu. Jibaba mmoja alikuwa amewawekea bastola wale watoto huku akiwa amekunja sura kwa hasira sana.
“Tulia hivyo hivyo mama” Yule jamaa akafoka kwa sauti yenye ghadhabu.
“We nani jamani?” Mke wa Makurumla akamaka kwa mshangao huku akiwa na hofu sana.
“Naitwa Geza Ulole, nakuomba endesha hii gari mpaka sehemu nitakayo kuelekeza. Geza alifoka na mama yule hakuwa na jinsi tena zaidi ya kukubaliana na hali halisi.
Geza alikuwa haraka kweli kweli katika kila hatua anayoipitia kwenye shughuli zake. Hakuacha hata siku moja nafasi za kizembe zipotee kwa namna ile. Ni baada ya kuifuatilia ile gari mpaka pale nje ya duka lile, na ndipo walipomuona mke wa Makurumla akishuka kutoka pale garini. Geza akamuarisha Swedi asimamishe gari na muda huohuo akachomoja na kupiga hatua kubwa na kali mpaka alipofungua mlango wa nyuma wa ile gari ya yule mama na kuufunga. Akiwa humo akaitoa bastola yake na kuwawekea wale watoto waliokuwa mle garini.
Mama huyo akaanza kuiondoa gari taratibu na kwa kufuata maelekezo ya Geza.
_______
Ni mwendo wa dakika ishirini hivi, Makurumla akafanikiwa kufika Kimara kwenye jumba lao la siri. Huko akakutana na MK pamoja na watu wake. Makurumla alidhamiria kitu kimoja tu. Ni kuchukua ile dawa ya kuwaponya mabinti wa marais wawili ili airudishe familia yake iliyotekwa na watu asiowajua. Alichanganyikiwa haswa, hata akashindwa kufikiria kama kuna njia nyingine mbadala tofauti na ile. Uamuzi wa Makurumla haukuwa sawa kwa MK, haukumuingia akilia kabisa.
“No, siwezi kufanya huo ujinga. Nimepoteza muda wangu mwingi kufanya huu mpango… halafu leo unakuja kuniambia hayo mambo, non sense” MK akafoka huku akiwa amemtumbulia macho kwa hasira.
“Anko, huwezi kuiacha familia yangu iangamie hivihivi wakati kuna njia aisee…” Makurumla akalalama.
“Sasa kwanini ulinihusisha na huu mpango?”
“Wewe ndio jembe langu anko kwanini nisikuhusishe?”
Wakati hayo yote yanazungumzwa pale sebuleni, Bosco alikuwa anayasikia kutekea chumba kingine ambako alilala. Akainuka na kukiendea chumba cha MK, huko kulikuwa na chupa mbili za dawa zilizowekwa mezani. Chupa moja ilikuwa na dawa yenye rangi nyekundu na ya pili ilikuwa na dawa yenye rangi ya bluu, zote ziliwekwa kwenye hiyo meza na pembeni yake kukiwa na mabomba matatu ya sindano. Bosco akachukuwa chupa hizo na kuzificha kwenye mfuko wa koti lake, akafungua mlango na kuanza kutoka taratibu. Kilichokuwa kinampa wasiwasi kuhusu jambo lile ni baada ya yale malumbano baina ya MK na Inspekta Makurumla. Alihofia kutosa vyote kwani yule jamaa anayejiita MK hakuwa akimuamini katika mpango ule. Alijikuta akimtilia shaka tangia yupo kule Bagamoyo. Hakuwa na amani naye kabisa. Bora azichukue zile dawa akatengeneze pesa peke yake pasi na mtu yoyote kujua.
Hivyo baada ya kuzificha zile dawa akapita kwenye kordo la kwanza na kuzama mlango wa nyuma huku akiwa kwenye mwendo wa kunyata. Akaufikia na kujaribu kuufungua ila akagutuka kuwa mlango huo ulifungwa. Akarudi tena kwa kunyata mpaka sehemu ambayo funguo za nyumba hizo huwekwa. Akazichukua funguo husika na kuanza safari ya kurudi tena kwenye ule mlango lakini alihisi kitu kigumu kikimzibiti nyuma ya kisogo chake, na ndipo alipogeuka kwa upole huku mwili wake ukimtetemeka haswa.



“Tulia kama ulivyo Bosco na kisha eleza kwanini unavizia vizia namna hiyo” Ilikuwa sauti ya mmoja wa wafuasi wa MK aliyekuwa anazifuatilia nyendo za Bosco tangia anazichukua zile funguo kutoka pale kwenye kiwiko cha funguo.
“Kwani vipi babu, navia navia kitu gani” Bosco akafoka huku akitoa mdomo wa bunduki ulioelekezewa kwake.
“Acha ujinja nitamuita Master aje aku kill oh…” Jamaa huyo hajamalizia kusema tu, aliachiwa ngumi kali ya uso mpaka akahisi kelele fulani la wadudu zikimtembea masikioni. Mbele hakuona kitu zaidi ya nyota pamoja mwanga hafifu sana. Hata hivyo kelele yake ilisikika sebuleni na hapo wakagutuka. Wakakimbilia hadi kwenye ule mlango, ulikwishakuwa wazi kabisa, Bosco alichoropoka na kukimbia kwa kasi lakini hajafika mbali.
Kutoka kwenye ule mlango wale wafuasi wakamshuhudia Bosco akiparamia ukuta akijaribu kupingukia kwa nje lakini akajikuta akijibwaga chini nay owe kali likamtoka. Risasi iliyofyetuliwa na mmoja wa wafuasi wale ilimpata pajani na kuanguka chini kama mzigo. Hatiamye wakamzunguka na kuanza kumhoji. Hakutoa jibu hata moja japokuwa alipigwa mara kadhaa.
“Pumbavu kachukuwa dawa huyo fala, mkamateni mleteni huku ndani” Sauti ya MK ilinguruma kutokea pale mlangoni huku akiwa kwenye ghadhabu ya aina yake. Wakaanza kumkokota kwa nguvu bila kujari kilio chake.
Akawekwa chini huku mdomo wa bastola ya MK ukiwa kwenye utosi wake.
“Leta hizo dawa fala wewe…” Akafoka kwa jazba. Makurumla alijikuta akakunja uso huku hali kuchnganyikiwa ikiwa imemtanda mno.
“Sija…chukua mi..mi kwa kwe..li” Bosco alijitetea lakini kitako cha bastola kilimtatisha usemi na kumuibua yowe la uchungu. Damu zikaanza kumchuruzika taratibu kutoka puani na mdomoni.
“Usilete huo ujinga, na nikiingia mifukoni mwako, walai utajuta kuzaliwa” MK akangurumana na hapo Bosco akaanza kutetemeka kwa hofu. Alijua vyema shughuli ya MK.
Bila kukawia, MK akazama kwenye mfuko wa Bosco upande wa kushoto na hapo akakutana na chupa nyekundu.
AMA!
“Eheee, braza, unajaribu kutusaliti sisi?” MK akamaka kwa ghadhabu sana, hata hivyo hakuziacha ghadhabu zake zipite kirahisi rahisi namna ile wakati msaliti wake yupo mbele ya macho yake anamuona dhahiri. Akarusha juu mguu wake wa kulia na kuutulisha pajani mwa Bosco, kwenye jeraha la risasi. Yowe likamtoka. MK alifanya vile kama mara tatu na kilichoendelea hapo kwa Bosco ni kupiga kelele mpaka sauti ya mwisho huku akijipigiza chini kama mzigo ilhali yowe likiwa kwenye kasi ile ile.
“Muache basi Anko aah!” Makurumla akamkatisha MK baada ya kuona anaendelea kumshushia kipigo Bosco.
“I’m not your Anko still now” MK akamfokea Makurumla kwa jazba la aina yake huku akimaanisha hana ujamaa nae mpaka wa kuitana wajomba kama alivyojitutumua kutamna neon lile la “ANKO”.
Khaa!
“Eeh vitu Anko una nini sasa, okay anyway, familia yangu unaisaidiaje sasa?” Makurumla akafoka huku akitoa msisitizo juu ya familia yake tekwa.
“Maliza mwenyewe hayo masuala yako sitai kusikia pumbavu zako. Unataka kuleta ujanjaujanja hapa ebo!” MK akakoroma.
Makurumla akachanganyikiwa. Usaliti juu ya lile swala linaenda kumtokea muda si mrefu kuanzia hapo. Wafuasi walikuwa wametengeneza duara mle ndani huku wakiwaweka kati Bosco, MK pamoja na Makurumla. Makurumla hakutaka kuona hali kama ile inakuja kujitokeza na kuikosa familia yake kwa wale watu asiowajua kabisa. Kisa pesa.
Pesa zipo tu ila sio kupoteza familia. Nimetumia miaka mingi sana kutengeneza familia, iweje leo niiache ikitoweka. Hii amani ya moyo itakuwa wapi?
Swali kali lilipita kichwani mwake huku akipima Upendo na Pesa, ikiwa ni kama jaribio kwake la kuchagua kitu kimoja. Ndipo alipoamua kuchagua Upendo tu. Pesa zipo na zitakuwepo lakini sio amani na faraja la moyo, likipotea sio rahisi sana kulipata tena na hata likipatika basi halitakiwa na mashiko zaidi ya lile la awali. Kutokea hapo akajikuta akichomoa bastola yake na kumuelekezea MK huku macho yakiwa yamembadilika rangi na kuwa mekundu kwa hasira sana.
“Nipe hizo dawa Anko” Makurumla akafoka kwa nguvu ilhali meno yake ameyaumanisha kudhibiti hasira zilimpande sana. MK akacheka kwa dharau huku akimtaza kwa mbwembwe zote
. “Unache…” Makurumla alipojaribu kusema kitu hakuweza kumalizia kwani kisogo chake kilimtambaa maumivu kwa kasi sana. Mkono wake wa kulio ulioshikiria bastola ukamuwia mzito sana na bastola yake ikamtoka na kuanguka chini. Sio mkono tu peke yake uliomzidi uzito bali hata magoti yake pamoja na kichwa, vyote vilimuwia uzito usiosimulika. Hatimaye akaanza kwenye chini akiwa ametepweta kama alimwagiwa maji.
Kitako cha bunduki kundi ya mfuasi mmoja kutoka nyuma yake, kilitua vizuri kisogoni kabla hajajiandaa na madhila hiyo kabisa. Pale chini Bosco alikuwa kimya sana, ilikuwa ishara tosha ya kutambulika kama amepoteza fahamu.
Master Killer au MK kama anavyopenda kuitwa kufuatia na kazi zake haramu anazofanya, wakachukua zile dawa na kuondoka pamoja na wafuasi wake huku wakiwaachia Makurumla pamoja na Bosco nyumba yao. Hisia za kutegeneza pesa vichwani mwao zikawajia, walipanga wasafiri siku na kwenda mkoani Tanga na huko wangelichukua boti la kuwasafirisha Somalia ambako mara kadhaa washirika wao wanakopatikana.
________
Simu ilipigwa zaidi ya mara kumi mzima bila kupokelewa. Kitu ambapo kilimkasirisha sana Geza ambaye alikuwa ameishirikia simu na namba iliyosomekwa kwa jina la Inspekta MAKURUMLA. Hakutaka kuamini kama mzee huyo ameamua kuitoa sadaka familia yake kwa uchu wa fedha za kuiibia serikali ilhali yeye ni muajiriwa katika jeshi la polisi akiwa na cheo cha juu kabisa cha uisnpekta.
“Tunachezewa mdogo wangu” Geza akanguruma kwa sauti kubwa. Akaitazama ile familia na mama na watoto iliyojilaza kwenye kapeti ndogo la mle ndani huku wakiwa wamefungwa kamba mikono na miguuni pamoja na kuzibwa midomo yao kwa vibandiko maalumu alivyokuwa navyo Geza mle ndani kwake.
“Tunafanyaje sasa kaka?” Swedi akahoji, naye alikuwa amechoka kuketi pale ndani kwa muda mrefu sasa. Alitamani awepo nyumbani wake na mpenzi wake Rayana.
“Hebu subiri hapo kwanza dogo,nipe funguo zako za gari, nitakuja baada ya saa moja” Geza akazungumza na Swedi akachomoa funguo za gari yake na kumpatia Geza. Hakuwa na shaka juu yake kwani alijua fika vitu anavyovifanya Geza.
Geza akafungua mlango na kutoka zake nje ila kabla hajaingia garini, akakumbuka kitu. Akarudi na kufungua mlango huku akiwa nusu nje nusu ndani akamwambia Swedi.
“Dogo wacheki hao watu kwa umakini sana, usiwaachie.”
“Sawa”
Alishika uelekeo wa barabara kuu ya Morogoro. Alikuwa kwenye mwendo kasi huku damu ikimchemka kwa kile kitu anachoenda kukifanya. Alitaka kujua sehemu ambayo aliambiwa na mmoja wa vibaraka wa Makurumla kule kwake Mbezi baada ya kuwanasa na kuwazimisha. Ni maeneo ya kimara ndiko alikokutilia maanani kwa muda huo. Alitaka kujua huko kwenye hiyo nyumba kuna kitu gani zaidi, labda ndio mbinu zao za kuwageuka zitaanzia huko. Hivyo alipanda akacheze nao huko huko kabla hawajafika kwenye himaya yao.
Baada ya muda wa dakika ishirini hivi, ndipo alipofika Kimara maeneo ya ndani ndani kabisa. Aliifuata ile njia ya vumbi huku akiwa makini kabisa na maelezo aliyopewa na mfuasi mmoja wa Makurumla. Kwa mwendo dakika kama kumi hivi, alikuwa kwenye muinuko mdogo ambao ulimuonesha nyumba nyeupe iliyopkwa chokaa huku ikiwa na geti jeusi kwa mbali. Akateremsha mteremko ule kwa mwendo wa taratibu na kuanza kupandisha tena mapaka alipofika nje ya jumba hilo.
Kitu cha kwanza kukiona ni mishirizi ya dama za gari pale nje ya geti. Akatoka nje ya gari huku akiwa na bastola yake. Mazingira yalikuwa shwari sana kwani maeneo yale yalikuwa mapya kwa watu, na ndio kwanza watu walianza kununua viwanja na ni wachache waliojenga na nyumba hizo hazikuwa zimeisha, kwa hiyo hakukuwa na mtu anayeishi zaidi ya ile nyumba aliyokuwa anaitazama kwa macho. Akafungua geti taratibu sana, akaingia ndani na kurudisha geti lile akiwa makini sana. Kutokea pale alipokuwa akaweza kuona gari moja tu kwenye maegesho upande wa kushoto. Pia aliweza kuona malngo wa kuingilia sebuleni hakuwa umefungwa, hivyo akakimbia haraka bila kutoa sauti ya kishindo na kuwashtua wale walio ndani. Akajificha pembeni ya malngo ule na kuchulia pale sebuleni. Hapo ndipo alipowaona.
Walikuwa wamejilaza huku mmoja damu ikimtoka kuanzia puani mpaka mdomoni, pia sakafu ililowa damu tupu iliyonaza kuganda ilhali pajani mwake kukiwa na jeraha kubwa. Geza akaanza kupekua chumba kila chumba ila hakukuwa na mtu yoyote. Lakini kile chumba cha mwisho kukagua akakutana na kitu kilichomchezesha akili.
Mabomba ya sindano yaliyokuwa kwenye meza. Akaamini kabisa kuwa dawa za kuwaponya mabinti wa marais zitakuwa mle ndani. Akaanza kukagua tena ila akajikuta akijisonya mwenyewe na swali likamvaa kichwani mwake.
Kama dawa zipo humu ndani je, ni nani aliyewazimisha hawa watu humu? Ina maana kuwa hao watu wamezichukua dawa na kuondoka huku wakiwazimisha wenyewe dawa.
Swali hilo likamfanya atoke kwenye chumba kile na kurudi sebleni kwake. Alipomkagua yule mzee alilala kifudifudi akakutana na simu ndogo ya kiganjani. Ilikuwa imewashwa na kulikuwa na missed call zaidi ya kumi.
“Nini shida Inspekta Makurumla wakati una cheo kikubwa kabisa? Sasa ona wamekuzimisha wenzako” Geza akazungumza kuwa kama anazungumza na ule mwili usiokuwa na fahamu. Akaifungua simu kwenye upande wa namba alizopiga muda mfupi. Akakutana na namba iliyoahifadhiwa kwa jina la Anko. Akamakinika na hiyo namba kwa muda kidogo kisha akarudi kweny upande wa ujumbe. Akakutana na jina lile lile la Anko. Alipoingungua ujumbe wa mwisho kutumwa akajikuta akiachia msonyo wa ghadhabu.
“ANKO INSP PAMBANA UITOE FAMILIA YAKO AISEE, TUACHE SISI TULE HIZI PESA. NA SASA TUPO TU HAPA KATI NAKULA MAISHA KABLA SIJASEPA”
Ni ujumbe wa Anko ulikuwa umesomeka hivyo. Akachukuwa uamuzi wa kuipiga ile namba ila haikupokelewa.
Yupo kati wapi?
Swali hili lilimkaa kichwani Geza bila ya kupata jibu. Aliketi pale sofani na kuwaza mara kadhaa lakini hakupata jibu lolote na ndipo simu ya Makurumla ilipoanza kuita.



Alipoitazama akakutana na jina la Anko. Akatabasamu na kuipokea kisha akaiweka sikoni bila kuongea. Baada ya sekunde chache mtu kutoka wa pili akaanza kuongea.
“Inspekta… Inspekta…” Jamaa kaanza kuita ila Geza akatulia tu.
“Huongea sasa we mzee?” Akafoka na tena na safari akamtukania mama yake.
“Uko wapi?” Geza akaluliza kwa sauti kavu.
“Sikia mimi sio MK mzee wangu… nakuomba tuonane sasa hivi na haraka sana kabla huyu jamaa hajafanya mambo yake. Dawa zote kaziacha hapa”
“Jibu swali basi.. uko wapi?” Geza akaghafirika.
“Nipo kwenye hotel moja inaitwa SUN ANGEL huku katikati ya jiji” Akajibu. Hakujua mtu anayeongea nae ni mtu wa aina gani. Kumpa ramani ya wao waliko kungewaletea shida sio ya kitoto.
“Unakuja?” Jamaa akauliza na Geza akaitikia kisha muda huo huo akatoka nje na kuingia gari. Akakanyaga moto kwa kasi kuelekea Sun angel hotel iliyopo katikati ya jijini.
_______
Hoteli ya Sunangel ilikuwa na magari mengi yaliyoegeshwa kwenye eneo husiku huku baadhi ya watu wakiingia na kutoka kwenye hotel hiyo. Geza alipaki gari yake pembeni kabisa upande wa kulia mwa hotel ile. Hapo akaitoa simu yake na kusoma ujumbe amba ulikuwa umeingia wakati akiwa kwenye mwendo kutoka kule Kimara. Alipoisoma akakutana na maelezo aliyopewa na yule jamaa. Aliambiwa chumba namba hamsini ghorofa ya pili. Haraka Geza akatoka huku akiwa na wahka mno. Akapitia mapokezi na hapo hapakuwa na shida kabisa tbaada ya kutoa maelezo. Akaanza kupandisha ngazi kwa mwendo wa haraka mpaka alipofika kwenye ghorofa namba mbili isha akaanza kuhesabu vyumba mpaka akakifikia chumba husika.
Kilikuwa chumba namba hamsini, akagonga lakini kimya kingi kikatanda. Akagonga zaidi ya mara mbili na hapo akachukua uamuzi wa kusukuma mlango. Ulikuwa haujafundwa, ndipo alipojikuta akiangukia ndani na kutua chini. Akastaajabu sana baada ya kuona kitu ambacho alitakiwa kuona lakini sio katika hali aliyoitarajia.
Yule jamaa ambaye alikuwa anazungumza na alikuwa anavuja damu pale sakafuni, ubongo wake ulikuwa nje.
Geza akashikwa na butwaa…
Alipotazama vizuri akamkuta alikuwa ameshikiria simu yake. Akajiinua haraka na kutaka kutoka kwenye chumba kile, huku akiamini kuwa inaweza kuwa mtego na kshikiliwa kwa kesi ya mauaji bila kutarajia.
“Washenzi hawa” Akahamanika mno.
Akaichomoa bastola yake na kuanza kunyata ili atoke nje.
LO!
Alijikuta akitupwa ndani na kutua chini kama mzigo, kufuatia kwa teke lililotumwa na MK kutokea kule mlangoni. Risasi mbili zikatumwa na hapo Geza akajipindua kwa tabu pale chini na risasi zikachimba kwenye sakafu.
Eeh!
Bastola ya MK ilikuwa inakohoa kimya kimya kutokana na kiwambo kilichowekwa kwenye bastola hiyo. Ilikuwa ni hatari mno. Wakati huo MK, Master Killer alikwishaingia ndani kwa kishindo na kurudisha mlango kwa nguvu. Sasa walibaki wawili walio hai mle ndani na yule jamaa ambaye alikuwa akiwasiliana na Geza akiwa watatu lakini hakuwa na uhai.
“Kama mwanaume basi achia hiyo basto…” Kabla Geza ahajamalizia kusema, akashindiliwa teke la nguvu na kumfanya apepesuka ila hakuanguka. Hajatulia vizuri, aliiona ngumi ya MK ikija kwa kasi kwenye uso wake ila hiyo akaiona na kuikwepa kwa kumvuta mkono ule ule uliokunjwa ngumi, wakati anamvuta alikuwa amemtegea mguu kwa chini ambao MK hakuuona. Akajikuta akipigwa gwala na kujitupa kwa nguvu sakafuni. Yowe likamtoka.
Bado tifu lilikuwa change kabisa kwa mahasimu wawili hawa. Muda huo huo baada ya Geza kumkata gwala MK, akajipindua na kumgeukia kule jamaa alipo ila kwa wepesi wa MK, akafyatuka kwa nguvu huku akiwa amekielekeza kiwiko cha mkono wake mbele ilhali yowe la hasira likimtoka. Geza aliiona hali, kwani nay eye akavivuta pembeni na kumpisha jamaa yake. MK akajikuta akijikita kwenye sakafu peke yake. Hapo hapo Geza akamuangukia juu na kuing’ang’ania shingo ya MK.
“Tulia basi…” Geza akakoroma ila MK hakuyajari hayo. Geza akaendelea kuongea “…haya nina uwezo na kuivuta hii shingo yako kuelekea upande mwingine na huo ndio utakuwa mwisho wako braza, sasa sitaki tufike huko nioneshe tu chupa za dawa kabla maamuzi hayajafikia penyewe” Geza akafoka ila MK hakujibu kitu, alikuwa anashindana na ile roba ya nguvu iliyomkabili.
Geza akaongeza ladha ya kumkaba shingo na hapo MK akaanza kukoroma kwa uchungu kama samba dume lingurumalo nyikani. Akalegeza na jamaa akaanza kukohoa kama mgonjwa wa kifua kikuu. Kulegeza kwa roba ile lilikuwa kosa sana kwani MK ajikitupa kiwiko chako kwa nyuma na kumtandika nacho Geza tumboni. Akaachia ukulele wa maumivu huku akijaribu kujiinua pale chini ila ngumi kali ya kichwani ikamfanya aone nyota mbele yake.
“Bado mtoto mdogo sana wewe khaa!... haya dawa ulizokuwa unazitaka chukua sasa (akamtukania mama yake) wewe!”
Kitu ambacho kinamkera sana Geza katika maisha yake ni kutukaniwa mama yake wakati hata hausiki na varangati lile. Geza akajikakamua na kuyafumba macho kabla hajayafumbua tena na hapo akafyatua kama mshale. Akamvaa MK kwa nguvu zote, hii ilikuwa inashuhudiwa kwenye mieleka tu lakini Geza aliingiza kwenye ugomvi ule na hapo akajipatia pointi za bure. Akamsuka na kumkutanisha kwenye ukuta kwa nguvu. MK akaachia kelele ya maumivu huku akijizoazoa pale chini mtoto mdogo. Kabla hajajiweka sawa Geza akamtundika teke kali ya shingo na kumshindilia kwa nguvu ukutani. Akatulia kimya.
‘Shaini wewe!”
Geza akatoa pumzi ya ngguvu huku akimtazama yule hasimu wake mwenye sura yenye ukatili sana.
“Sura mbaya utadhani kitu gani, yaani hata mimi mwenyewe handsome” Geza akajiongelesha peke yake akiwa amesimama. Alipogeuka kushoto akakutana na kioo kikubwa. Akajitazama na hapo akatabasamu huku akijivuta nywele zake zilizovurugana ovyo. Ilikuwa dalili tosha ya kuwa nywele zake hazikupata kuonana na kichanio kwa siku nyingi tu.
Akiwa kwenye ubize na kile kioo ghafla mlango wa chumba kile ukagongwa. Akajikuta akishinkwa na wahka na hapo akirudi kwa kasi hadi nyuma ya mlango na kujibanza hapo. Mlango baada ya kugongwa mara tatu ukafunguliwa na mtu ambaye kwa haraka ile hakumfuahamu. Yule mtu alipokuta hali sio shwari akajikuta akitoa bastola yake kwa pupa huku akitoa sauti ya mfoko. Geza alikwishaliona tukio na hakufanya ajizi. Akamrukia kwa teke kubwa na kumwaga chini kama mzigo wa kuni. Akamshika kwa nguvu na kuanza kumtandika ngumi kali za uso hadi damu ikaanza kumvuja. Akaona haitoshi kabisa, akamgeuza na kumvutia kwake na kumtupa kwa nguvu huku akiwa amekilelekeza kichwa cah huyo jamaa ukutani.
PAAAF!
Jamaa akajikita utosini kwenye ukuta na damu ikaruka sentimeta kadhaa kutoka kwake. Ukuta ukalowa damu. Hakika chumba hivyo namba hamsini katika hoteli ya Sun angel kilikuwa ni chumba cha damu haswa.
Geza hajatulia tu akakoswakoswa na risasi ya mguuni na alipotazama inakotoka akakiona kitu kinapita kama upepo mbele yake.
Eeeh!
Alikuwa ni msichana aliyevalia kininja huku akiwa na kisu mkono wa kushoto na wakati huo mkono wake wa kulia ulikuwa na bastola yenye kiwambo. Msichana huyo akaruka kwa uzuri na kuigonganisha miguu yake kisha akageuka kwa kasi baada ya kudunda kwenye ukuta ule mithili ya mpira wavuni.
E bwana eeh!
Geza akalaza chini kwa uwepesi na yule msichana akapita juu kama mshale, akatua na kusimama mbele huku akihamaki kwa kumkosa kwa pigo lile, lakini akili ayke ikacheza ndani ya nusu sekunde. Akiwa kwenye kasi ile ile akajirudishwa kwa serakasi ya nyuma kisha akapanuka msamba huku akitupa mkono wake wenye kisu kwa kasi ila Geza akakwepa na kisu kikampita sentimeta chache kutoka ubavuni mwake palepale sakafuni. Sasa wakabaki wakitazama pale chini na kila mtu akili yake ikimcheza mara dufu.
Wa kwanza kuifumbua akili yake kwenye ule mtazamo wao ni yule msichana, akakitupa kisu chake mbele na kumkwaruza Geza kidogo. Alipotaka kuiruhusu bastola yake ikohoe kwa Geza ilikuwa ngumu kwani Geza akiwa kama mbogo aliyejeruhiwa akamtupia konde zito yule msichana la ubavuni na hapo akatoa sauti ya maumivu ilhali kisu chake akikiachia kuwa kama kilimzidi uzito.
“Malaya mkubwa…” Geza akafoka na kujiinua pale chini ila bila kutarajia, yule msichana alijizungumsha pale mithili ya mcheza judo na kuinuka kwa kasi huku mikono yake ikiwa kama miguu. Kichwa mikono chini, miguu juu, kisha akabetuka na teke kali mfano wa mtu anayepita mpira kwa mtindo wa “Tiktaka”. Teke likampata Geza begani lakini halikuwa na uzito wa namna hiyo wa kumfikisha Geza chini. Geza akiwa kwenye kasi ileile ya mwanzo akamchota ngwala ya mikononi na msichana huyo akatoa sauti ya uchungu kwa mara ya pili huku akibamiza kichwa chake sakafuni.
takatifu. Msichana huyo alipobamiza kichwa sakafuni akajikuta akigaragara pale chini huku akilia kwa uchungu ilhali mikono yake ikiwa kichwani. Geza akasogea na kutaka kumvua ule mzura ambao alijiziba nao kichwani na kumfanya awe na muonekani kama wa kininja. Ile anavuta tu akamaka kwa sauti huku akikohoa kama aliyepaliwa na maji. Geza akajirusha kitandani na kugeuka kule aliko yule msichana. Alimuona akiwa hana mzura sasa. Sura ya msichana huyo ilikuwa ya duara, mweupe mwenye sura ya kupendeza sana, nywele zake zilizonyeusi na kulalia mithili ya mabinti wa kihindi. Geza akahamaki kwa mshangao.
“Kule kwetu Mwanza kama hujui wewe ni mali kubwa sana aisee, yaani inachapwa na ng’ombe zaidi ya hamsini laa! Huu weupe ndio naoupenda mimi”
Geza alijisemeshwa mwenyewe huku akikubaliana na uzuri wa yule mwanamke mwenye mavazi ya kininja.
“Nawe Geza unawaza nini wakati umekutana na malaika wa kifo chako eboo!”
Bado Geza alikuwa kwenye mawazo yake ya ajabu. Mawazo yote yalikuwa yanatembea ubongoni mwa Geza kwa nusu sekunde ilhali akijipigia mahesabu jinsi ya kumdhibiti msichana yule kisura.


“Oooh we fala” Geza akamaka kwa sauti ya hamaniko na kujitupa pembeni ya kitanda kile huku akiacha nafasi ya msichana huyo kutua kwa kisu kwenye kile kitanda kama jinamizi.
“Shiit bwege wee!” msichana yule akalaani kitendo alichokifanya Geza. Na kwa mara ya pili Geza aliiwahi bastola ya ya yule binti iliyokuwa imeanguka pale chini kisha akafytua risasi kadhaa zilichimba ubao wa kitanda cha mle ndani na kumkosa yule ninja wa kike.
“Dooh” Geza akafoka. Akawa anamsaka kule aliko na kubani kuwa akikuwa amesimama wima kwa mguu mmoja kwenye sakafu. Kabla hajafytua nyingine yule ninja akatereza kama nyoka aina ya mkunga na kutazama na Geza uso kwa uso pale alipo huku akimfanya Geza ashinde kunyoosha mkono wake na kumtandika risasi. Hapo hapo hakutaka kufanya makosa kwani katika moja ya pointi za ushindi kwenye harakati kama zile ni mtu amkalie mbele yake kwa sentimeta chache kama zile pasi na kumtwanga kichwa chake kilichokomaa utadhani hana nyama za kichwa.
Twangiii!!
“Yalaa” Ninja la kike likaachia ukulele huku akijitupa chini kwa nguvu. Kichwa cha Geza kilimchana sehemu ya juu ya jicho na damu zikamruka.
“Nini sasa mchumba” Geza akamaka kwa hasira sana. Hapo akapata wasaa wa kumtandika kitako cha bastola kisogoni mwa yule masichana na kimya kikatanda mle chumba. Watu watatu pamoja na maiti moja, zilikuwa zimedondoka pale chini kama utani. Geza akafanya upesu kupekua chumba kile. Kutoka kwenye mgongo wa yule msichana akaliona begi ndogo lililotuna. Akaliendea na kuanza kupekua haraka ndipo alipokutana na chupa mbili. Moja ilikuwa na rangi ya damu na wakati nyingine ikiwa na rangi ya bluu, hapo akajua fika kuwa mzigo ambao alikuwa anaupigania ndio ule. Akarusha ngumi hewani na kushangilia kwa sauti ya chinichini. Shangwe za ushindi.
Akiwa kwenye shangwe zile hakumuona MK aliyepata fahamu na kujikaza kuinuka pale chini na kuokota kisu. Geza alimpa mgongo yule hasimu wake. Kwa kitendo cha haraka akajikaza na kuanza kumfuata Geza kwa nguvu za ajabu, hakuwa na tofauti na mzimu ulioamka baada ya miaka mingi kupotea. Ila wakati anainuka pale chini simu yake iliyokuwa mfukoni ikamtoka na kuanguka sakafuni huku ikitoa mlio wa kupasuka, kitu ambacho kilimshtua vyema Geza Ulole, Msukuma halisi kutoka Mwanza.
“Oooh! Braza umeamka tayari laa!” Alihamaki na kumkwepa kwa kasi, kisha MK akapita kama upepo mbele yake huku akifoka kama nyoka.
“Shiit! wewe (akatukana tusi kubwa la nguoni)”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nini sasa braza?” Geza akahoji kwa mzaha ila MK hakuwa na utani hata kidogo. Aliziona dawa zipo mikononi mwa hasimu wake na mpango wa pesa unaenda kutawanyika. MK akiwa kwenye maruerue yake, akajikuta akipigwa teke kali na Geza na kumfikisha tena chini kama mzigo. Teke lilikuwa zito kiasi kwamba hata Geza mwenyewe baada ya kulirusha akajikuta akifikia makalio chini. Akainuka haraka kama sio yeye na kumshindilia teke kali la kisogoni na MK akatulia kimya. Muda huo huo Akazichukua zile dawa na kuzitia mfukoni mwake kisha akafungua mlango na kutoka nje kwa mwendo wa taratibu sana kama sio mtu aliyefanya tukio. Alipofika kwenye vyumba vya kwanza akaiona siku ya mezani sehemu na hapo akaiendea kisha akaingia namba kadhaa.
Alitoa taarifa polisi juu ya tukio lile lililotokea na kuwapa namba ya chumba husika pamoja na jina la hoteli yenyewe. Hapo akaanza kushusha nagzi haraka haraka na kutoka nje. Nako kulikuwa shwari watu walikuwa kwenye harakati zao. Akainggia garini na kuzitoa zile chumba mbili za dawa.
“Ni hizi kweli au?” Akajiuliza huku akizitazama wa umakini zile chupa. Dakika chache sana baadae kabla hajaondoka kwenye eneo lile la hoteli, akasikia king’ora cha gari za polisi zikiwasili nje ya jingo lile na polisi wakaanza kuwapangua watu haraka. Polisi kadhaa aliingia ndani na wengine walibaki nje wakiwa na bunduki zao.
Geza akaliwasha gari na kuondoka zake.
___________
Kwenye baa moja mtaa wa Sinza. Ulikuwa ni usiku wa saa sita. Aidan pamoja na rafiki yake walikuwa kwenye eneo hilo. Chupa kadhaa zilikuwa mezani huku baadhi zikiwa zimepinduliwa kama ishara ya kutumika. Kichwa cha Aidan hakikukaa sawa kabisa kufuatia na maisha anayopitia kwa wakati ule, hautarajia kama atakuja kuyapatia maisha na kuyachezea kiasi kile. Ni kosa kubwa alilofanya.
Wakati wanaendelea kunywa bia zao pale mezani, mara akatokea msichana aliyevalia kimini kifupi kilichoishia juu ya magoti yake, juu alivalia kijiblauzi kifupi sana kiasi kwamba kitovu chake kikionekana dhahiri. Kwenye kwapa yake kulikuwa na pochi ndogo kiasi. Alivaa viati vyenye visigino virefu, hata pale alivyotembea viatu hivyo vililia ko! Ko! Ko!
Akasogea pale mezani na kuketi pembeni yake huku akitokwa na tabasamu bila kuongeleshwa. Aidan alimuona huyo msichana japokuwa alikuwa amelewa sana. Yule mwanamke akaanza kujilegeza pale alipoketi huku akiwakonyeza Aidan na rafiki yake. Akaona haitoshi akainuka na kuanza kujibaraguza pale kwenye meza. Walibaki wakimtazama tu. Mara ajigeuze na kuchezesha makalio yake huku mara nyingine ayatoe matiti yake yawavutie wale vijana walio mbele yake.
Katika tukio kama hili ni mara chache sana kwa wanaume rijali kama Aidan lazima liwasisimue kwa kiasi fulani. Na kama utashindwa kujizuia basi lazima kifuate kitu fulani bila matarajio. Lakini kwa akina Aidan hao walikuwa wamelewa, jambo ambalo ni rahisi kufanya kitu chochote bila kujitambua. Bila matarajio wakajikuta wanamkodolea macho yule binti huku wakimeza mate ya uchu kama fisi mla mifupa. Uzalendo ukamshinda rafiki yake Aidan na hapo akajikuta akimvuta mkono yule binti kisha akainuka nae huku akiwa anapepesuka kilevi.
“Un shilingi ngapi?” Yule binti akauliza kwa sauti ya mnong’ono.
“Kwa..ani shili..ngi nga…pi?” Rafiki wa Aidana akuliza kwa ulevi ulevi.
“Elfu hamsini unayo?”
“Ya kazi gani hiyo?”
Wakati maongezi hayo yanaendelea, tayari yule binti alikuwa anamtekenyatekenya rafiki wa Aidan kwa madoido yake. Mara kadhaa aliinama na kumbinulia makalio jamaa huyo ili mradi tu amshawishi yule mtu kufanya anachotaka.
“Nina ishirini tu”
“Hamna kitu kama hicho ongeza bas mara mbili yake.. weka arobaini”
“No!”
Bado hawakuelewana kabisa na ndipo hapo msichana huyo alipotaka kuondoka ila akawahiwa kushikwa mkono na Aidan. Akamtazama kuanzia chini hadi juu yule aliyemvuta mkono wake.
“Vipi nyie kwani… kama hamna hela si mkaushe ebo!” Binti akafoka.
“Nini tatizo mrembo, unataka shilingi ngapi?” Aidan akauliza huku macho yake yakimtazama kivivu.
“Hamsini elfu”
“Sasa ndio unasepa”
“Si huyu boya wako analeta habari za kuombea kama dukani”
“Ila si biashara? Anyway nakupa sabini turushe wawili” Aidana akasaili.
Hapo sura ya yule msichana ikachanua tabasamu.
“No! Fanya laki ndio safi”
“Sina hiyo”
“Ok sawa twendeni basi”
Ni baada ya makubaliano wakaamua kuondoka eneo lile huku wakipepesuka mpaka kwenye chumba walichokodisha kwenye baa hiyo hiyo. Huko shughuli iliyowaleta kwenye eneo husika ikaanza pasi na kumbukumbu ya kinga.
Ulevi kichwani!
__________
Geza akafika nyumbani kwake na kuwakuta mateka wake wakiwa wameamka na sasa walikuwa wakitazamana kwa kukata tamaa kabisa. Mkononi akiwa amezikamatia zile chupa mbili zenye rangi mbili tofauti. Akamuonesha Swedi huku akifurahi.
“Umezipataje?”
“Nitakupa mkanda mzima dogo”
“Na hawa watu si tuwaache?”
“Hapana, yule fala wao lazima tumfikishe mbele ya sheria. Hatuwezi kukaa na watu hatari kama hawa kwenye jamii yetu. Nitamfungulia mashtaka” Geza akasaili.
“Sawa”
“Kinachofuata ni kufanya mpango wa kurejesha hizi dawa kwa raisi lakini lazima tutumie mbinu ama sivyo tutatiwa mbaroni na kuhusishwa na utekaji wa wale mabinti.” Gez akazungumz kitu na Swedi akatikisa kichwa kuafiki kile kitu anachoambiwa.
Ilitakiwa wafanye kitu tofauti katika uwasilishaji wa dawa zile huku akiwaamisha vyombo vya dola kuwa si wao ambao wamehusika na kitu kama cha namna hiyo. Hata hivyo walikuwa na nafasi kubwa ya kujitetea kwani baada ya Geza kutoka kule hotelini alipiga simu polisi, na hivyo wangeliwakamata wale jamaa aliowazimisha na kumtambua MK ambaye siku za nyuma alikuwa akijionesha kwenye kamera kwa sura yake halisi bila kujificha. Wakiaachana na ushahidi huo wa kujilinda dhidi ya kitu hicho, kule kwenye nyumba iliyo Kimara, kulikuwa ana Inspekta Makurumla pamoja na mshirika wake Bosco, wote wangelisaidia chombo cha dola kwenye uhusiano wa tukio hilo na endapo Makurumla atakama bado Geza na Swedi wameishikiria familia yake. Kwa hiyo ni vigumu kwa Makurumla kusema uongo wakati anatambua wadai wa kesi hiyo wanaweza kuiteketeza familia yake.
Ameshikika patamu sana!
Muda huo huo Geza alitaka kurudi Kimara kwenye nyumba ile ya siri ila akaingiwa na wao linguine. Apige simu na kuwataafu polisi juu ya uwepo wa watu hao waliohusika na tukio la mtekaji wa binti wa rais. Akafanya hivyo palepale. Huku akijitambulisha kama raia mwema mpenda amani nchini.
Kesho yake asubuhi sasa. Kila aina ya gazeti liliandika kile wanakijua juu ya kukamatwa kwa watu hao kwenye nyumba mbili tofauti. Baadhi ya agazeti yalisomeka kuwa ‘MAJAMBAZI WAFUMWA HOTELINI’ mengine yalichapisha vichwa vyao kuwa ‘MTEKAJI SUGU WA BINTI WA RAIS ATIWA MBALONI’ ili mradi kila gazeti liwe limeandika kitu wanachokijua kuhusiana na sakata lile.
Na ndipo Geza alipochukua moja ya gazeti hizo na kuanza kulisoma. Ila simu yake ilipoita, alipotazama akakutana na namba ambayo alihifadhi mle simuni.



Jina liliandikwa Swedi. Akaipokea na kuiskiliza. Hivyo baada ya kumaliza maongezi yake akatoka zake kwenye eneo la wauza magazeti na kwenda nyumbani kwake, ndiko anakoitwa. Hakuwa mbali sana na nyumbani kwake, akatumia dakika tano kwa umbali ule.
Akamkuta Swedi akiwa na Rayana ilhali wale mateka wao hawakuwa pale sebuleni tena bali walikuwa kwenye chumba kingine. Hawakupanga wawatoe mpaka pale watakapotimiza dhamira yao. Kitu kilichobaki kwao ni uuwasilisha mzigo kwa mlengwa wao. Mawasiliano baina yao yalifanyika huku simu kutoka ikulu ikipokelewa na George Mbasho.
“Unatuhakikishiaje kitu unachokiongea ni cha ukweli?” George akasema.
“Vielelezo vyote si nimekutajia aisee… na huyo mtu mwenye sura mbaya ndiye mimi niliyemdhibiti kule hotelini. Hta hivyo nimemdhibiti Inspekta wenu wa jeshi la polisi, naye ni mshirika mkubwa wa huyo jamaa mwenye sura mbaya hapo je?” Geza akafoka.
“Sawa ila sasa kikubwa kinachotakiwa ni upatikanaji wa hizo dawa, tutazipataje?”
“Subiri mbona una haraka wewe?”
“Hapana si kama unavyojua hali ya mabinyi ni tete”
“Sawa nahitaji tukutane mimi na rais” Geza akazungumza na kutulia zake.
“Ok, subiri niungumze nae nitakupa jibu” George akazungumza na kukata simu.
________
Majira ya saa tatu za usiku. Swedi akiwa na Rayana walikuwa kwenye gari yao kwenye sehemu moja maeneo ya Masaki. Utlivu ulikuwa wa hali ya juu sana. Hapo ni sehemu ya ahadi yao baina yao na mtu ambaye walitakiwa wampatie zile chupa ambaye ni rais. Chupa za dawa hizi zilikuwa kwenye mfuko maalumu na kuziweka kwenye droo moja la mle garini. Waliangaza huku na huko bila kuona kitu zaidi ya dakika kumi baada ya kufika sehemu ile.
Wakiwa wanaangaza angaza, wakaliona gari moja likiwajia kwa mwendo wa taratibu sana. Hapo wakamakinika na lile gari, lilitokea upande wa kushoto kwao. Lakini kabla hawajamfahamu mtu anayeendesha gari hiyo upande wao wa kulia likatokea gari nginyine, nalo lilikuwa kwenye mwendo mdogo kama lile la upande wao wa kushoto. Sasa wakawa wamebaki njia panda, waanze kuitazama gari ipi na wamalizie gari ipi. Gari la upande wa kulia likafunguliwa mlango wa mbele upande wa abiria. Akashuka mtu mmoja aliyevalia suti huku mkono mmoja ukiwa ameuficha kwenye koti lake, ni kama mtu anayetaka kutoa bastola kwa tahadhari.
Mtu yule akawa anajongea kulifuata lile gari huku akiwa makini sana. Upande mwingine wa gari ya kwanza akatoka mtu mwingine. Huyu alivaa shati la mikono mirefu pana lililochomekewa safi kwenye suruali yake pana. Naye alikuwa akilijongelea lile gari lao. Hatua chache yule jamaa wa upande wa kulia alilifikia lile gari na kugongwa kwenye kioo uapnde wa dereva ambako kuna Swedi. Moyo ukamdunda kwa woga kwani hakujua kwanini wamekuja na mtindo kama ule. Akashusha kioo taratibu na kukibakiza nusu kisha akamtazma yule jamaa. Alikuwa amevalia kofia aina ya pama.

(SEHEMU HII TUMEITOA KUTOKANA NA KUZUIA WEZI WA MITANDAONI KWA ATAKAYEHITAJI KIPANDE HIKI HADITHI ITAKUWEPO KWENYE MAGROUP YETU KWA BEI POA SANA. IKUMBUKWE TU SWEDI NA RAYANA WAMEKUTANA NA GEORGE MBASHO KUKABIDHI DAWA)...

“Hey! Subirini, kwahiyo gari yangu mbona inaachwa hapa?” Swedi akahoji na Mbasho akamjibu kuwa watarejeshwa pale baada ya kuonana na rais. Gari zile mbili zikaondoka wakiiacha gari ya Swedi huku gari waliyoipanda ikiwa imetangulia.
Kutokea nyuma yao Geza akatoka kwenye sehemu moja yenye maua na kutazama zile gari kisha akarudi tena palepale alipokuwa amejificha ilhali akiwa na bastola yake mkononi.
_________
Mwendo wa dakika kama kumi hivi, gari zile mbili ziliwachukua Swedi na Rayana zikafunga breki nje ya jingo moja refu. Wakashuka wote na George akaanza kuelekea ndani huku nyuma yake akifuatwa na Swedi, Rayana pamoja na baadhi ya watu wa George. Walipofika ndani wakaingia kwenye lifti na kupanda juu mpaka ghorofa ya tatu. Huko wakaingia kwenye kordo ndefu lililo na vyumba kadhaa, na wao wakaingiza kwenye chumba kimoja kilichojitenga na vyumba vingine mle ndani. Ndipo walipokutana na mtu waliotakiwa wakutane nae.
Rais alikuwa ameketi kwenye kiti cha kuzunguka huku mbele yake kuna meza kubwa . Chumba kile pia kilikuwa na sofa kadhaa zilizozunguka meza moja ya kioo. Juu ya meza hiyo kulikuwa na glasi kadhaa za tupu huku zikizidiwa kimo na chupa kubwa isiyofunguliwa.
“Karibuni sana wanangu, nina imani mwanangu atapona sasa” Rais alisema na kuwafanya Swedi pamoja na Rayana watazamane kisha wakaafiki kwa kutikisa vichwa vyao.
“Ok! Safi sana. Nimekuwa na wakati mgumu sana kulitatua tatizo hili kwa kweli, madhali mmekuja raia wema wenye uzalendo na nchi yenu, sina budi kuwashukuru kwa moyo huu. Hivyo sitosita kuwatunuku pongezi kwa wingi na kuwashukuru zaidi ya mara mbili vijana wangu..” Rais alizungumza mengi na maneno yaliyojawa na matumaini kwa mtoto wake. Taratibu akajikuta anavunjwa na machozi. Wakatoka pale walipokuwa na kuketi kwenye zile sofa. Na sasa walikuwa watu wane tu, rais mwenyewe, Rayana, Swedi na George Mbasho. Hapo waliendelea na maongezi mafupi kisha Swedi akachukua ule mfuko wenye vyupa na kumpatia rais. Akazichomoa na kuzitazama kwa umakini bila kuelewa kabisa.
“Mna uhakika kabisa kuwa ndio zenyewe?” Rais akahoji.
“Ndiyo mzee”
“Mmejuaje kama ndipo hizi na je labda mmebadilishiwa?”
“Tuna uhakika asilimia zote hata kama akiitwa mkemia mkuu” Swedi akazungumza kwa kujiamini sana. Rais akatazamana na George kisha akaziweka zile chupa juu ya meza.
“Ok! Nitazichukua hizi dawa na kuzipeleka kwa mkemia zikapimwe, na ikigundulika kuwa ni zenyewe, I promise you nitawapa kitu ambacho hamtakisahau maishani mwenu” Rais akajikakamua na kunena maneno hayo.
Swedi na Rayana wakatikisa vichwa vyao tena kwa kuafiki kauli ya rais wao.
Baada ya kumaliza maongezi yao, wakarudishwa mpaka sehemu waliyoacha gari yao kisha gari zilizowalet zikageuza na kuondoka zao. Geza akatoka sehemu yake ya maficho na kujiunga na wenzake kisha wakatimka eneo hilo kwa mwendo kasi.
_______
Kwenye kituo kikuu cha polisi kanda ya Dar es salaam. Maafisa kadhaa walikuwepo kwenye kituo hicho huku wakiwa na shahuku kubwa sana la kusikia maneno kutoka kwa watuhumiwa waliokuwepo kwenye kituo hicho. Kikubwa walichoshangazwa na kutaka kujua kwa undani ni juu ya uwepo wa Inspekta Makurumla kwenye sakata lile la utekaji. Hawakuamini ktiu kama hicho, walitaka wajithibitishie kwa macho na masikio yao kutoka kwa mhusika mwenyewe. Wakati huo bado walikuwa wameswekwa rumande wakisubiri mahojiano maalumu yaliyohusisha maafisa wa polisi. Ilikuwa ni asubuhi ya saa nne. Muda wa mahojiano ulitakiwa uanze baada ya chakula cha mchana na ndipo jopo la maafisa lianze kuwaandama wale watuhumiwa.
Saa, dakika na sekunde zilizidi kuyoyoma kwa kasi huku kila afisa wa jeshi alikuwa tayari kwa zoezi lililowakabiri mbele yao.
Kutoka kwenye kichumba kidogo kilichokuwa na giza la wastani kiasi kwamba kwa mtu aliyekaa nje ya chumba hicho kutoka kwenye mwanga asingeliweza kuona kilicho ndani vizuri lakini kwa aliyekuwa ndani angeliweza kumuona yule wan je kutokana na kulizoea giza kwa muda mrefu.
Ndani ya chumba hicho kulikuwa na watuhumia zaidi ya watano, kila mmoja alikuwa macho akisubiri hatima yake inakoelekea. Hofu kubwa ilitanda kwa mtu mmoja aliyeketi kwenye pembe ya chumba kile huku hofu kubwa imemtanda. Hakuwa na hakika kama atakuwa na cheo tena. Ni kesi kubwa yenye fadhaa kwake. Famili yake nayo bado haijatambua kitu kilichompata na ndio jambo kubwa analowaza. Nani atailea familia yake. Akajikuta aatoa chozi huku akiumanisha meno yake kwa hasira mno.
Ama kweli majuto ni mjukuu…
Askari aliyeshika bunduki yake ilhali akiwa wamechomekea sare zake kwa unadhifu akakurubia kwenye kile chumba na kukifungua. Akamita jina kamili ya mtuhumiwa mmoja, hapo akachomoka Inspekta Makurumla aliyejawa na huzuni usoni.
“Ongoza huku” Askari yule akamfokea Makurumla. Nae akatii bila shuruti.
Akaingizwa kwenye chumba cha mahojiano na alipopepesa macho yake akakutana na vichwa vya maafisa kadhaa pamoja na askari wengine waliopewa kazi hiyo maalumu ya kuwahoji jamaa hao. Akatikisa kichwa kwa hamaniko mno huku akiwashuhudia baadhi ya maafisa wale wengine wenye vyeo kama cha kwake.
Looo!
Yamemfika.
______
MAHABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Chupa mbili za dawa zenye rangi tofauti, zilichukuliwa na kupelekwa kwa mkemia ambaye aliaminika na serikali kwenye maabara yake. Siku hiyo aliitumia kwa kuzitasmini dawa zile kabala hazijatumika kwenye miili ya mabinti wenye sumu miilini mwao. Alishajaribu majaribia mawili bado haikumpaa jibu kamili na sasa alikuwa la tatu.
Jaribio la tatu alilifanya kifanisi huku akimini ndio jaribio linaloenda kuonesha uhalali wa dawa zile zilizoletwa na raia wazalendo na mabinti wa rais. Ila baada ya kulikamilisha jaribia hilo akajikuta anatokwa na macho pima. Hakuamini kama kweli jaribio lile limemkataa kwa mara nyingine.
Akakata tama kabisa hata kufanya jaribio linguine…


Dakika kumi tano zikapita baada ya kushindwa lile jaribio la tatu. Akaamua aache kila alichokifanya na kuketi kwenye kiti kimoja kilichopo mle maabara. Kichwa chake kilicheza mara mbili zaidi huku akitafakari cha kufanya ili kuthibitisha dawa ile.
Walihofia sana kuzitmia dawa zile kwenye miili ya wale mabinti kwani hawakujua walioleta walikuwa na malengo gani. Hivyo iliwalazimu kuleta pale kwa mtu wao waliomuamini katika kutatua utata ule. Baada ya kupumzika vya kutosha akarudi tena kwenye vyombo vyake na kuanza jaribio la nne. Aliamua kufanya majaribio mawili ya mwisho na kama itatokea kushindikana basi atatoa taarifa juu ya ufeki wa dawa zile. Jaribio hili la nne lilimchukuwa kwa dakika arobaini na hapo akaanza kuona matumaini ya mwanzo. Alitaiwa alandanishe na zile damu za wale mabinti na dawa zilizoletwa. Na kama italeta uwiano kati ya sumu ya kwenye damu na zile dawa, basi dawa hizo zitakuwa zipo sahihi na huru kutumika kwa mabinti hao.
“Yes!” Mkemia huyo akamaka kwa kihoro huku akirusha ngumi hewani. Ni baada ya kuona kile kitu alichokuwa anakitaka kwenye mitambo yake ya kimahabara.
“Ni zenyewe” Akapiga shangwe.
Akazichukua zile chupa na kuziweka kwenye brifkesi kisha akachukua simu na kuipiga. Akatumia dakika chache sana kuongea na mtu wa simuni kabla hajakata simu na kutoka nje. Mlangoni alilakiwa na walinzi wenye bunduki mikononi mwao wakihakikisha suala zima la usalama linakuwepo kwenye eneo lile. Akaingia ndani ya gari na safari ya kuondoka ikaanza.
__________
Swedi na Rayana siku hiyo walikuwa wamepumzika tu nyumani kwao. Hawakuwa na sehemu ya kwenda, hivyo waliitumia siku hiyo wacheze pamoja pale nyumbani wakitazama sinema pamoja na kucheza magemu. Michezo ilidumu kwa muda mrefu pale sebuleni na hapo wakajikuta wakitazama kwa ukaribu sana kama majogoo yaliyopigana na kuchoka.
Safari yao ya michezo ikapungua kasi na sasa Rayana alikuwa ameemkalia Swedi juu ya kiuno chake ilhali damu ikimchemka. Wakatazamana na kutabasamu kwa pamoja, ukaribu baina yao ukawa mdogo sana kwa lugha ya kiingereza huitwa “Zero distance”.
“Sweet…” Rayana akaita kwa sauti ya puani.
“Naam!”
“Nakupenda my love”
“Me too” Swedi akajibu akimaamisha upendo wake kwake upo kama ulivyo kwake. Wakagusanisha ndimi zao na kupoza joto lenye huba. Katikati ya dimbwi la huba, simu ya Swedi ikaita na aliyepiga alikuwa Geza Ulole. Kilichomfanya apige simu ni juu ya taarifu za kualikwa kwenye sherehe fupi ya binti wa rais kwenye mandhari ya ikulu.
“What!” Swedi akamaka kwa mashangao. Hakuamini masikio yake.
“Ok, si tunaenda wote?” Swedi akauliza.
“Hapana nyie nendeni tu, sisi watu wengine sio wa kuonekana ovyo hapa nchini” Geza akazungumza kwa sauti pana. Ni kawaida yake sana Geza kutojitokeza kwenye masuala kama yale. Ilikuwa lazima afanye hivyo ili kujilinda mwenyewe.
“Sawa kaka wacha sisi tuende, nadhani atatoa zawadi tu kama alivyoihaidi” Swedi akamalizia kusema na kuagana na Geza. Akabaki akimtazama Rayana aliyekuwa juu yake bado hakutaka kubanduka kifuani kwake.
“Baby, dawa zimefanya kazi tayari” Swedi akamwambia Rayana, naye akashtuka. Akakumbuka maneno ya rais baada kuthibitisha dawa zile. Ahadi ilibaki kwake.
Wakakumbatiana na kuangusha hadi sakafuni huku wakichezea kwa furaha isiyo kifani.
_________
Mahojiano yalikuwa marefu sana ila hata hivyo Inspekta Makurumla hakuwa na majibu yaliyowalidhisha maafisa wale. Hivyo alisubiri mahakama ichukue uamuzi wake ama labda ampate wakili mwenye utetezi mzuri wa hoja kuhusiana na kesi ile. Wale watuhumiwa wengine wakiongozwa na MK, walikuwa na kesi zaidi ya moja. Kwanza walikuwa na tuhuma ya utekaji, uvamizi wa hotel pamoja na mauaji yaliyofanyika kule Sun angel hotel kabla ya kufika kwa Geza.
Isipokuwa Bosco tu, huyu alikuwa na tuhuma za utekaji nyara akishirikiana na Inpekta Makurumla. Hivyo naye aliwekwa rumande bila ya dhamana. Wote walilia kwa pamoja huku kila mmoja akiwa na jambo lenye uzito ndani yake.
Yamewafika haswa…


__________
Si siku ambayo ilikuwa na sura mpya kabisa mioyoni mwa mabinti hawa wawili pamoja wa ndugu zao, mara baada ya maswahibu makubwa waliyopitia. Ilikuwa siku ya kipekee mwishani mwao, siku ambayo wasingelidhani kama itakuwa kuwepo kwao kwa mara nyingine. Dayana na Mercela, mabinti wa marais kutoka Rwanda na Tanzania baada ya kupitia kwenye ugumu wa maisha ya kutekwa na hatimaye kuwekewa sumu miilini mwao. Ila kilichokuja kuwaponya wahakuamini. Warisubiri kwa hamu sana ujio wa watu hao waliofahamika kama raia wena wenye uzalendo kwa mabinti wa marais hao. Ukumbi maalumu ulikuokuwa umeandaliwa, ulijaa kila aina ya mapambo.
Wako wapi wageni waalikwa?
Dawa zile zilitumika kwa muda wa wiki moja na siku mbili, afya za mabinti hao zikaanz akurudi kwa kasi bila kutegemea. Awali ya hapo, dawa zile zilitumika kwa kuchanganywa na zilivyekwa mara mbili kwa kutwa. Ndipo walipoanza kutapika vimiminka vyeusi kutoka tumboni na haja haja kubwa yao ilikuwa nyeusi. Sumu iliondoka kwa kasi sana hata ilipohitimu siku tano mbele, wakajikuta wakipata nguvu mpya.
Ni kama dakika thelasini mbele, gari ndogo ilionekana ikiingia kutoka getini na kuendeshwa mpaka kwenye maegesho maalumu ambako kulikuwa na magari mengine. Akashuka Swedi akiwa Rayana wake pembeni. Wote walipendeza haswa kimavazi waliovalia. Unadhifu wao ukawafanya watu wengi waliopo mle ndani wawatazame kwa mshangao sana. Baadhi ya watu hao walioshuhudia wale mapatna wawili na Dayana pamoja na Mercela.
Dayana moyo ukamdunda.
Mawazo yalimrudisha nyuma na kuvuta kumbukumbu na ndipo alipoweza kukumbuka. Ndio alishawahi kumshurutisha msichana aliye mbele ya macho yake kisa mapenzi. Alimpa vitisho haswa aachane na mtu anayeitwa Aidan.
“Ni yeye au namfananisha?” Dayana akajiuliza kimoyomoyo huku asiamini kabisa.
“Oooh mabibi na mabwana… wageni wetu muhimu kwenye sherehe hii ndio wanawasili sasa kuwape makofi” Sauti ya George Mbasho ikanguruma kwenye kipasa sauti na kuwafanya watu waanza kupiga makofi na shangwe ilhali mbele yao wakitazama na watu wawili wenye mavazi nadhifu, Swedi na Rayana.
Fadhaa ikamvaa Dayana huku asiweze kuamini kuwa wale anaowaona ni watu ambao wamechangia kwenye uponyaji wa maisha yake. Machozi yakaanza kumtoka bila kutegemea.
Bila kupoteza muda, watu wote waliingia ndani ya ukumb huku wakisindikizwa na rais. Wakafika na kuketi kwenye viti vilipagwa kwa mpangilio wenye kupendeza.Wakati wote Dayana alikuwa akimtazama msichana Rayana aliyeketi na mwanaume wake kwenye vile viti maalumu vilivyotengwa. Vilikuwa vitatu lakini mmoja wao hakuwepo. Alikuwa Geza.
Sherehe le fupi ilianza kwenye majira ya saa nne asbuhi na kumalizika saa mbili za usiku huku watu wakinywa na kufurahi kwa pamoja. Na sasa mziki laini ulikuwa unapigwa, huo ulikuwa wasaa maalumu wa watu kuchangamana na kuzungumza mawili matatu. Nafasi hiyo ndioaliyokuwa anaisubiri kwa dhati sana Dayana. Akatoka pale alipokuwa ameketi na kuwafuata Swedi pamoja na Rayana waliokuwa wanacheza pembeni mwa ukumbi ule.
“Sorry!” Dayana akawashtua walengwa wake kwa upole. Rayana alipotazam akakutana na sura ambayo dhahiri aliikumbuka kwa wepesi.
“Sorry sana. Naomba kuzungumza na wewe dada’angu walau kwa dakika chache tu” Dayana akasaili lengo lake. Rayana hakuwa na pingamizi na ndipo alipokubali na kutoka kwenye eneo lile hadi kwenye viti, wakaketi na kubaki wakitazamana tu.
“Dada unanikumbuka…?” Dayana akavunja ukimya kwa kuanza na swali hilo. Rayana akakubali kwa kutikisa kichwa. Hapo ndipo Dayana alipoanza kutoa mahubiri huku akiomba msamaha kwa kila kitu alichomfanyia. Mpaka anamaliza alikuwa anavuja machozi mashavuni lakini Rayana akambembeleza na kumfuta machozi.
“Usijari dada angu ni mambo ya ujana tu haya, usiwae kabiza kipenzi” Rayana anazungumza huku akimbembeleza Dayana. Dayana hakuamini kama kweli msichana huyo alikuwa na roho nzuri namna ile. Hakika alifadhaika sana kupita kiasi.
Baadae muda wa rais kutimiza ahadi yake ukawaidia. Watu waote wakakusanyika na kuchukua nafasi zao huku wakiwa na shahuku kubwa la kutaka kujua nini kitatolewa kwa watu wale. Rais akachukua kipasa sauti na kuanza kusema.
“Nawashukuru sana kwa ujio wenu. Pia nawashukuru vijana wangu kwa kuniponyesha wanangu. Japokuwa hawajatimia ila nimefarijika kwa kiasi kikubwa sana. Nichukue nafasi hii kuwapa zawadi maalumu kama shukurani zangu” Akatosa kikaratasi kidogo na kukichambua taratibu. “…Kijikaratasi hiki nilikiandika tangia nawahidi hapo mwanzo”
Akasoma kijikaratasi kile kwa sauti. Mpaka anakuja kumaliza kutaja zawadi ile Swedi na Rayana hawakuamini masikio yao. Kilikuwa kitu cha ghafla sana kwa muda ule.
________
Siku tatu baadae, Geza, Swedi pamoja na Rayana waliamia kwenye nyumba zao zilinunuliwa na rais kama moja ya zawadi zao kwa kitu walichokifanya. Sio tu nyumba peke yake, hata kwenye kadi za ya benki zilizajwa pesa za kutosha zitakazowawezesha kuanzisha biashara zao au kitu chochote wakitakacho.
“Haha pesa hizi naenda kuoa kifaa cheupe mpaka Mwanza mzima watambue” Geza alizungumza huku akitabasamu na uwafanya Swedi na Rayana waangue kicheko kikubwa. Walikuwa kwenye ufukwe wa bahari ya hindi wakipigwa upepo utokao baharini. Ni baada ya zoezi lao kwisha Geza akapitisha uamuzi wa kuachia familia ya Inspekta Makurumla.
Walidumu kwenye ufukwe huo na kwa muda wa masaa karibu tano kuanzia saa tatu ya asubuhi huku wakibadilishana mawazo. Ndipo ilipohitimu saa nane za mchana, wakaamua kuondoka wakiwa na gari la Swedi. Walipitia nyumbani kwa Geza na kumuacha kisha wao wakaendelea na safari ya kwao. Njiani wakajikuta wakishangaa kitu wanachokiona mbele yao. Ni kona mbili kabla hawajafika nyumbani kwao, ndipo kundi la watu lililokuwa linapiga kelele za mwizi zikija sehemu ya gari ya ilipo.
Amaa!
Wakiwa kwenye taharuki ya aina yake, wakawaona watu wawili wakichomoka kwa kasi sana huku wakikoswa mawe pamoja na marungu na kikundi cha watu kilichokuwa nyuma yao.
“Eeeh jamani Aidan” Rayana alimaka kwa sauti kubwa huku akijaribu kufungua mlango ili akamsaidie Aidan aliyekuwa anakimbia huku akipiga kelele.
Atamsaidiaje mbele ya wananchi wenye hasira kali?
Wakiwa wamehamanika tukio lile, wakashuhudia kundi linguine likitokea mbele ya akina Aidan. Wakawekwa kati na mkong’oto ukaanza kutembea.
La haula!
Lilikuwa ni tukio la kutisha sana. Kushuhudia mtu akipigwa mawe kama nyoka ni jambo ya kutisha sana. Rayana akaanza kulia mle ndani na kutaka kuchomoka lakini Swedi alimshika asifanye kile kitu anachotaka kukifanya. Msichana kama yule angelifanyaje mbele ya wale wananchi wenye hasira kali?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda huo huo walishuhudia gari ya polisi ikifunga breki pale kwenye eneo la tukio na kuwafanya watu wakimbiane kwa fujo huku wengine wakigongana. Ilikuwa vurugu mtindo mmoja. Wakashuka polisi na kuwachukua wale wapigwaji na kuwatia ndani ya gari lao kisha likatimua kwa kasi.
__________
Egemeo la Inspekta Makurumla kwa wakili wake halikuzaa matunda, akajikuta akitosa jela na kupoteza kazi moja kwa moja. Ni kama ilivyo kwa wale watuhumiwa wengine, mawakili wao walishindwa kufanya vizuri kwenye kesi iliyokuwa inawakabili.
***MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI***

**MWISHO**





Comments

Popular posts from this blog

SHANGAZI NAE ANATAKA-07

join sugar mumy and dating whatsapp group link