MESEJI NZURI ZA KUMTUMIA MPENZI WAKO ILI AZIDI KUKUPENDA ZAIDI
- Wewe ni kila kitu kwangu.
- Nitateseka bila wewe.
- Ninataka nikwambie tu kuwa ninakuwaza muda wote.
- Ninatamani kuwa mikononi mwako muda wote.
- Ninakupenda zaidi ya unavyofikiria.
- Unafanya mapigo ya moyo wangu yaende mbio nikikuona.
- Najisikia vizuri mno nikikuwaza mpenzi.
- Ninajihisi salama nikiwa nawe.
- Nikiwa mikononi mwako ninajihisi nimefika!
- Ulishaubeba moyo wangu na sitaki uurudishe.
- Siwezi kuishi bila wewe mpenzi.
- Sitosahau usiku ule ambao tuli.
- Tabasamu lako linanipoteza kabisa.
- Unanistaajabisha kila siku.
- Nitafanya lolote ili niwe nawe.
- Ninakutamani kila saa.
- Ninaona fahari kuwa na wewe.
- Wewe ni wangu daima na milele.
- Unanifaa sana mpenzi.
- Sijui ningekuwa wapi bila wewe.
- Kila siku tunapokuwa pamoja naona ninaishi ndoto yangu ya siku nyingi.
- Moyo wangu unasisimka ninapokuwa nawe.
- Hakuna mtu aliyewahi kuwa karibu nami na akanifanya nijisikie raha kama unavyonifanya nijisikie.
- Ninahesabu muda mpaka pale nitakapo pata busu lako tamu.
- Ni kama vile uliumbwa kwa ajili yangu.
- Wewe ni mtu pekee ambaye siko tayari kukuacha.
- Kila saa wewe ndiye chaguo langu.
- Unanifanya nijiamini sana mpenzi.
- Wewe ndiye baraka kubwa niliyowahi kuipata.
- Wewe ni mzuri sana aisee.
- Nikikuwaza tu, hata niwe na siku mbaya, itageuka kuwa nzuri tu
- Moyo wangu unakuhitaji sana sasa.
- Ninatamani ungekuwepo hapa na mimi.
- Ninavyokupenda jamani, acha tu!
- Ninajihisi mwenye bahati sana kukupata wewe kama rafiki wa karibu na mpenzi pia.
- Hata milele hainitoshi kuwa na wewe.
- Natamani ungekuwepo hapa ukanishika mkono na ukanivuta kwako.
- Nimekuwaza siku nzima. Ahsante kwa usiku mzuri kama ule.
- Sikuwahi kujua kuwa unaweza kummiss mtu hata kabla hajaondoka, mpaka nilipokujua wewe ndio nikaamini.
- Maisha yetu pamoja ni tafsiri ya upendo.
- Natumai uko na siku njema, mwenzio nashindwa kuacha kukuwaza muda wote.
- Daima hujawahi shindwa kunifanya nitabasamu wakati wote.
- Najikuta nikishindwa kujizuia kutabasamu kila ninapofikiria kukuona ukirudi toka kazini.
- Wewe ni wangu, kipenzi cha nafsi yangu.
- Ninakuthamini sana mpenzi.
- Unanifanya nijisikie mwenye bahati sana kuliko wote.
- Natamani nikupe mabusu mazito kila ninapokuona.
- Nataka niamke pembeni yako siku zote za maisha yangu.
- Wewe ni mcheshi sana, unanifanya niwe mwenye furaha wakati wote.
- Ninashukuru sana nimekujua
Comments
Post a Comment