MESEJI NZURI ZA KUMTUMIA MPENZI WAKO ILI AZIDI KUKUPENDA ZAIDI
Wewe ni kila kitu kwangu. Nitateseka bila wewe. Ninataka nikwambie tu kuwa ninakuwaza muda wote. Ninatamani kuwa mikononi mwako muda wote. Ninakupenda zaidi ya unavyofikiria. Unafanya mapigo ya moyo wangu yaende mbio nikikuona. Najisikia vizuri mno nikikuwaza mpenzi. Ninajihisi salama nikiwa nawe. Nikiwa mikononi mwako ninajihisi nimefika! Ulishaubeba moyo wangu na sitaki uurudishe. Siwezi kuishi bila wewe mpenzi. Sitosahau usiku ule ambao tuli. Tabasamu lako linanipoteza kabisa. Unanistaajabisha kila siku. Nitafanya lolote ili niwe nawe. Ninakutamani kila saa. Ninaona fahari kuwa na wewe. Wewe ni wangu daima na milele. Unanifaa sana mpenzi. Sijui ningekuwa wapi bila wewe. Kila siku tunapokuwa pamoja naona ninaishi ndoto yangu ya siku nyingi. Moyo wangu unasisimka ninapokuwa nawe. Hakuna mtu aliyewahi kuwa karibu nami na akanifanya nijisikie raha kama unavyonifanya nijisikie. Ninahesabu muda mpaka pale nitakapo pata busu lako tamu. Ni kama vile uliumbw...