USITAFSIRI VIBAYA HURUMA YA MWANAMKE KAMA UDHAIFU WAKE
Hii ni kwa ajili ya wanaume wote ambao wamekuwa na tabia ya kudharau pale mwanamke anapumuonesha huruma na upole.
Mwanamke akipenda kweli yu-radhi kukufanyia lolote lile! Atakuvumilia kwa kila hali, inabidi kutambua huruma na upendo wake ili kumtia nguvu.
Atapokupa dhati ya upole na huruma yake kisha wewe ukamlipa dharau na kuona umemuweka kiganjani,basi huruma hiyo hufika ukomo.
Moyo wa mwanamke ukiamua kukatia tamaa basi tambua hakuna kitu waweza fanya ukamrejesha katika hali yake ya awali.
Thamini jitihada za mwenzi wako anazokuonesha, zichukulie kwa uzito usije ukawa wewe ndiye sababu ya kuona kuwa hafai na hajitoshelezi
Comments
Post a Comment