"Wananionea wivu mwili wangu" - Linah

 
Msanii wa Bongo Fleva, mwanadada Linah Sanga ameibuka na kujibu maoni ya watu wanaomsema mtandaoni juu ya picha mbalimbali za mwili wake anazo'post' katika mtandao wa Istagram, akisema kuwa wanamuonea wivu.

Kupitia eNewz ya EATV, Linah amesema kuwa anawashangaa watu wanaomjadili kwa picha zake kwakuwa hajaanza leo kufanya hivyo na picha hizo zinaeonesha mwili wake halisi.

"Namshukuru Mungu ameniumba hivyo, simringishii yeyote ninaonesha nilichojaaliwa na hata kuimba ninaonesha kipaji changu", amesema.

"Mimi kama msanii lazima nifanye 'photoshoot' kila siku kwa sababu ni sehemu ya sanaa yangu kwahiyo ni kitu cha kawaida kwangu", ameongeza.

Aidha Linah amezungumzia kuhusu tetesi za kumfilisi baba wa mtoto wake baada ya kuachana, ambapo amesema kuwa vitu vyote alivyokuwa akifanya kipindi wako pamoja ameachiwa yeye ndio maana wanamuona hafanyi chochote hivi sasa.



Comments

Popular posts from this blog

SHANGAZI NAE ANATAKA-07

join sugar mumy and dating whatsapp group link