Mapenzi: Kwa nini kuwa na mahusiano ya kimapenzi kazini mara nyingi huwa hakuepukiki
Si vyema kumtumia mwenzako emoji ya kukonyeza kupitia ujumbe. Ukaribu huo ambao mara nyingine unachochea mapenzi ya ofisi haukuwezekana wakati wa janga la corona, wakati wengi walikuwa wanafanya kazi nyumbani. Licha ya hayo, wafanyakazi wamepata njia ya kuendelea kutaniana na wenzao, jambo ambalo linaonesha kutoepukika kwa mahusiano ya mapenzi ofisini au mahali pa kazi. Februari 2022 data kutoka Jumuiya ya Marekani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (SHRM) inapendekeza mahusiano ya mapenzi ya mahali pa kazi yanaweza kuongezeka hata wakati wa kufanya kazi nyumbani. Theluthi moja ya waliohojiwa kati ya 550 walijibu kwamba walianza uhusiano na wenzao wakati wa janga hilo, ongezeko la 6% kutoka siku kabla ya janga la kiafya duniani. Mahali pa kazi ni msingi mzuri wa mapenzi na mapenzi ya muda mfupi, ilhali kampuni nyingi hazipendi mahusiano ya kimapenzi kazini . Wataalamu wanasema kuna sababu maalum ambazo wafanyakazi hawawezi kuacha kushirikiana na wenzao, hata wakiwa wametengwa wakati...