Hekima itakayokusaidia kuolewa mapema
Kama ndoto zako ni kuolewa na mwanaume wa ndoto zako basi unatakiwa kujifunza kuwa lugha nzuri kwa watu wanaokuzunguka. Unatakiwa kuwa na lugha nzuri kwa sababu wapo baadhi ya watu humtasfiri mtu kutokana na kile amabacho unakizungumza. Wanaume wengi hushusha thamani ya mwanamke hususani suala la mwanamke huyu kutamka matusi mengi kwenye kinywa chake. Hivyo ikiwa una nia njema ya kutaka kuolewa unapaswa kuwa na heshima sana hususani kwenye suala la uzungumzaji. Ijenge thamani zaidi kwa kuzungumza lugha yenye kukujengenea taswira chanya kwa wale wanakusikiliza. Jifunze kuwa mnyenyekevu kwenye suala la kuzungumza, lugha yako nzuri ndiyo itakayowafanya watu wengine waone thamani yako. Na: Benson Chonya.