Posts

Showing posts from June, 2021

Zijue aina tano za mahusiano ya kimapenzi

Image
  Wanasaikolojia mbalimbali wamejaribu kuelezea aina za mahusiano ya kimapenz ambayo wapenzi wawili wanaweza kuwa wanayapitia katika kipindi flani cha mahusiano yao. Lakini kabla hatujaangalia hizi aina lazima tujue kuna vitu vitatu vinavounda na kudetermine ni aina gani ya mahusiano ya kimapenz watu wako nayo kwa mda huo. Kuna kitu kinaitwa TRIANGULAR THEORY OF LOVE yaani Intimacy,Commitment na mwisho kabisa ni Passion. Ntajaribu kuelezea kwa ufupi kila kimoja kabla sijaingia kwenye point ya msingi yenyewe. Intimacy. Hii ni hali ya kuwa karibu kihisia na mpenz wako,Kuna hali flani hivi hutokea yaani unakuta mnashare the same feelings.Sijui ka ishakutokea unataka tu kumpigia simu mpenz wako ghafla unakuta naye anakupigia,nafsi zenu zinakuwa zinaongea na unajikuta unachowaza wewe ni sawa cha mwenzi wako. Commitment . Hali ya mtu kuhakikisha uhusiano na mpenzi wake unabaki salama hata iweje.Mtu hapa anaweza kuwa katika uhusiano lakini asiwe committed kwa lolote kuhakikisha uhus...

Mambo 8 mwanamke anapaswa kufanya kabla ya kufunga ndoa

Image
  Kufanya mambo haya kutakupatia maarifa na kukufanya uwe na uwezo wa kufanya uamuzi bora zaidi maishani. Ni jukumu lako kama binti asiye katika uhusiano kufanya mambo mazuri zaidi maishani kabla ya kufunga ndoa. Kufanya vitu hivi kutakusaidia kuwa mwerevu zaidi na kujua mambo unayo na usiyo paswa kufanya. Soma makala yetu ya mambo ambayo mwanamke anapaswa kufanya kabla ya kuingia katika ndoa! 1. Jifunze jinsi ya kupika Tofauti na imani za watu kuwa kila mwanamke anapaswa kujua kupika ili ampikie bwana yake, kujifunza kupika kwa mwanamke kuna umuhimu tofauti. Ukiwa peke yako bila mchumba, una wakati mwingi, kwa hivyo katika wakati huu, utaweza kujipikia vyakula vinavyo kufurahisha zaidi. Pia, unapo pata wageni utaweza kuwa burudisha na ustadi wako wa mapishi. 2. Fanya vitu vinavyo kupendeza katika wakati wako wa ziada Unapokuwa peke yako, una wakati mwingi wa mapumziko, ni vyema kufahamu vitu unavyo vipendelea, katika wakati huu, utaweza kuvifanya badala ya kubaki kwenye nyum...

Unaweza kuolewa na mtu usiyempenda?

Image
Ni siku nyingine tunakutana kwenye kilinge. Tunajadili yale ambayo yanahusu uhusiano, uchumba na hata ndoa. Moja kati ya fikra ambazo zimekuwa zikiwatesa wanawake wengi katika mioyo yao, ni suala la kuolewa na mtu asiyempenda. Kila mmoja amekuwa na mtazamo wake katika suala hili. Kuna ambao wanaamini kwamba unaweza kuolewa na mtu usiyempenda lakini wapo ambao wanaamini huwezi. Wanaosema unaweza, huwa wanasimamia hoja ya kwamba hamuwezi kufanana kwa kila kitu. Mnakutana ukubwani, hivyo suala la mmoja kutompenda mwenzake, linaweza kubadilishika tu mbele ya safari kama vile mtu anavyoweza kumbadilisha mtu tabia yoyote ile. Wale ambao wanaoamini huwezi, huwa wanasimamia hoja moja tu kwamba utaishi katika kuudanganya moyo wako, hutafurahia ndoa yako na mwisho wa siku unaweza kuwa msaliti. Hoja hizi mbili zote zina mashiko. Kabla ya kuendelea, tusome kwanza mfano huu ambao msomaji wangu aliyejitambulisha kwa jina moja la Jack alinisimulia. “Kaka mimi naitwa Jack, nina miaka 29. Nina mtu a...