Umesikia mara nyingi sana kuwa “Unatakiwa kusamehe na kusahau”. Nini maana halisi ya kusamehe? Kusamehe ni kuamua kutomchukulia mtu hatua na kuondoa kinyongo moyoni mwako kutokana na jambo baya ulilofanyiwa na mtu huyo. Kusamehe kunasema hutakiwi kusikia neno “nisamehe” ndipo uendelee na maisha yako. Kusamehe kumewekwa na ni kwa manufaa zaidi kwa yule aliyekosewa. Ni wazi kuwa katika maisha kuna kukoseana kwa namna mbalimbali. Wapo watu wasiopenda suluhu wala msamaha. Ni dhahiri kuwa ni lazima wewe uliyekosea ufahamu manufaa na sababu za kumsamehe na kumsahau aliyekukosea; manufaa hayo ni haya yafuatayo. 1. Hukuweka huru Kutokusamehe kunakufanya ujisikie vibaya na kuwa kama mfungwa. Jambo baya ni pale utakapomwona yule aliyekukosea anafuraha na anaendelea na maisha yake bila tatizo. Kila wakati unalitafakari swala hilo na unahisi limetawala kila unachofanya. Hivyo ni vema ukasamehe ili uwe huru maishani mwako. 2. Hukuwezesha kuendelea mbele na maisha yako Kuna mambo mengi...