Baba alirudi nyumbani na kumkuta mkewe jikoni, akamkombatia, akamtazama sana mkewe na kumbusu kwenye lips, wakasalimiana na mkewe akampokea na kwenda nae chumbani kisha kurudi jikoni ili kumalizia kupika. Ilipofika wakati wa kula, mume alikaribishwa mezani na mkewe, pamoja na watoto. Chakula kikapakuliwa na kila mmoja kuanza kula, ghafla watoto wakaguna "MMMH". Baba anapata shauku ya kutaka kujua kilichopo ndani ya chakula, akaonja na kugundua maharage yalikuwa yameungua hivyo kutoleta radha nzuri. .. Mama akajisikia vibaya sababu alijua kilichofanya watoto wagune, akamtizama mumewe huku akisubiria kuona kile ambacho mumewe angesema, hofu ilimjaa. Mume akamtizama mkewe na kugundua wasiwasi alionao mkewe, akageukia sahani yake na kuanza kula, akamaliza sahani, akavuta hotpot na kuongeza chakula tena na kuweka maharage mengi zaidi ya mwanzo. Alipomaliza akamtizama mkewe na kumuambia "Mke wangu asante kwa chakula, umenitibu njaa yangu kipenzi''. Wat...