Ukitaka kuwa mwanaume wa shoka, epuka kula vyakula hivi
Katika makala hii hii utajifunza vyakula mbalimbali ambavyo wanaume hawatakiwi kula ili kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine unaweza kuwa unavitumia kila siku bila mwenyewe kujuwa. Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upala). Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku. Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi. Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara. Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics) lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa ki...