JE, UNATATIZO LA KUMALIZA PESA MAPEMA BILA MPANGILIO MAALUMU? SOMA HAPA UJIELIMISHE.
Njia pekee ya kutunza pesa ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Unachohitaji ni kujua pesa unatumia zaidi kwenye nini, hapo ndipo utakapojua ufanye nini ili kupunguza matumizi. Kila mara weka akilini kuwa yawezekana unanunua kitu kwa bei rahisi lakini jiulize ufanisi wake una umuhimu wowote au ni kutimiza wajibu tu. Tambua mahitaji yako halafu fanya hesabu za namna ya kutumia unachokipata kwa uangalifu. Tambua kuwa ili kupunguza matumizi kufanikiwe ni lazima ubadilishe mfumo wako wa maisha na namna unavyofikiria. Zifuatazo ni hatua unaweza kuzitumia kupunguza matumizi: 1.TAMBUA UNATUMIA PESA ZAKO KATIKA NINI ZAIDI Kama mpaka sasa hujui pesa zako unazitumia zaidi kwenye nini zoezi hili litakushinda. Ukiwa hujui pesa yako unatumia kwenye nini hasa, kila mara utakuwa mtu wa kushangaa tu kuwa hela yako imepungua. Na wengine wanaweza kuwalaumu wat...